Habari,
Kipimo cha mimba cha mkojo,kina pima uwepo wa homoni moja inayozalishwa na kondo la nyuma la mtoto mimba inapotungwa. Lakini homoni hii huweza kutengenezwa mwilini kwa sababu zingine zisizohusiana na mimba, ama ikaendelea kuonekana kwenye mkojo hata baada ya mimba kuharibika.
Kipimo cha uhakika kama mtu ni mjamzito ni picha ya Ultrasound, hiyo ikisema mimba ipo, unakuwa na uhakika ni kweli ipo. Na pia,inaweza kuonyesha mtoto kama yuko hai (akifariki tumboni, ataonekana hakui japokuwa miezi inaenda)
Jaribu kupima picha ya tumbo la uzazi, Ultrasound.