Changamoto ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kufilisika haiwezi kutatuliwa kwa mipango ya Ummy Mwalimu

Changamoto ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kufilisika haiwezi kutatuliwa kwa mipango ya Ummy Mwalimu

DaudiAiko

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
372
Reaction score
310
Wanabodi,

Katika kipindi hiki ambacho Shirika la Bima ya Afya Tanzania (NHIF) linafilisika, ni vyema kufahamu jitihada zinazo chukuliwa na serikali kuhakikisha kwamba watanzania walio jiunga na mfuko huu wanaelendea kupata huduma.

Kwanza kabisa tujaribu kuangalia athari ya shirika hili kufilisika. Kwa sasa ni ngumu kufahamu idadi ya watu waliojiunga na mfuko huu ila kama shirika likishindwa kuwa hudumia wanachama wake basi mamilioni ya watu ambao wamekuwa wakipata matibabu kupitia mfuko huu watakosa huduma.

Tofauti na hilo, hospitali zote zinazodai malipo kutoka NHIF zitayumba kwasababu utaratibu uliopo ni kwamba wagonjwa wanapata huduma hospitalini kwanza na malipo kutoka NHIF yanafuata baadaye. Famasi ambazo hazipo hospitalini na huhudimia wagonjwa wa NHIF nazo zitayumba kama bado hazijapata malipo kutoka NHIF. Kama hospitalini, famasi hizi hutoa huduma kwanza na hutegemea malipo kutoka NHIF baadaye.

Malipo haya hufanywa kila baada ya miezi mitatu ikimaanisha kwamba katika wakati wowote, famasi inayo hudumia wagonjwa wa NHIF huwa ina malimbikizo ya malipo ya miezi mitatu kutoka Shirika la Bima ya Afya.

Waziri wa afya Mhe. Ummy Mwalimu ameeleza changamoto mbalimbali zinazo sababisha shirika hili kuanguka na amependekeza mabadiliko kadhaa. Changamoto moja inahusu wanao jiunga kwenye mfuko huu wakiwa tayari ni wagonjwa.

Kutokana na kauli hiyo, inawezekana kwamba NHIF haifanyi uchunguzi wa kina wa wanojiunga kwenye mfuko huu. Kwa kawaida, kwenye bima zingine za afya, lazima ijulikane kama mwanachama mpya anaumwa magonjwa mbalimbali kama kisukari, presha au magonjwa mengine ambayo haya ambukizi.

Uchunguzi huu huchangia kwa kiasi kikubwa gharama ya kifurushi cha kujiunga na kiasi cha matibabu ambacho bima humlipia mgonjwa huyu. Kwa mara nyingi, matibabu yoyote huwa hayafanywi mpaka muhusika achangie bima kwa muda wa miezi sita.

Kitu kingine ambacho Mhe Ummy Mwalimu alijaribu kutoa ufafanuzi ni kwamba wanachama ambao hawaugui mara kwa mara huwa lipia ambao huugua mara kwa mara na kwasababu hiyo, kuwa na wanachama wengi zaidi kunaweza kuka ongeza mapato mengi zaidi kwa shirika.

Hili linaweza likawa kweli lakini ni muhimu kwa shirika hili kuweza kujiendesha kwanza liki hudumia wanachama waliopo kwanza na kuweza kulipa madeni yake yote kwanza. Kwa maelezo ya Mhe. Waziri, itahitaji idadi kubwa sana ya wanachama wapya kuweza kulikomboa shirika.

Yaani michango hii haiwezi kutosha kuliwezesha shirika kulipa madeni yote na kumudu kuwahudumia wanachama wapya wote kwa wakati mmoja.

Hoja nyingine ambayo Mhe Ummy Mwalimu alijenga ni njia ambayo serikali itatumia kuhakikisha kwamba NHIF inapata wachangiaji wapya. Mhe Ummy Mwalimu alisema kwamba hakuta kuwa na sheria inayo mlazimu mtu yeyote kuwa na bima ya NHIF kwa ulazima ila wananchi hawataweza kupata huduma mbalimbali bila ya kuwa na bima ya afya.

Kwa mfano, kadi ya nida, laini ya simu, n.k, mapendekezo hayo yanategemewa kupitishwa bungeni ili mabadiliko hayo yatekelezwe. Ni rahisi sana kutambua kwamba vipangamizi hivi havina tofauti sana na sheria na hata kama malengo ni mema, huwezi kumlazimisha mtu atumie fedha zake kama wewe unavyotaka.

Ili kuifufua NHIF, lazima serikali iingilie kati kwa kutoa fedha za kutosha baada ya tathmini ya kina kuhusu sababu ya shirika hilo kuanguka kufanyika. Michango ya ziada kutoka kwa wanachama wapya haiwezi kukidhi mahitaji ya shirika hili katika kipindi hiki.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.



 
Bima ya afya kwa Wote ni sera ya Chadema

Serikali iwashirikishe kwenye utekelezaji
 
Ukweli hawataki kuuzungumza kabisa hawa watu.
IMG-20220901-WA0001.jpeg
 
Yaani akili zao wanachofikiria watu wengi watakaojiunga ni wale ambao HAWAUGUI SANA ( au WASIOUGUA KABISA ) ili pesa zao wazitumie KUREKEBISHA MAMBO YAO.

Hii nchi bana 🤣🤣🤣🤣
 
Wanabodi,

Katika kipindi hiki ambacho shirika la bima ya afya Tanzania (NHIF) linafilisika, ni vyema kufahamu jitihada zinazo chukuliwa na serikali kuhakikisha kwamba watanzania walio jiunga na mfuko huu wanaelendea kupata huduma.

Kwanza kabisa tujaribu kuangalia athari ya shirika hili kufilisika. Kwa sasa ni ngumu kufahamu idadi ya watu waliojiunga na mfuko huu ila kama shirika likishindwa kuwa hudumia wanachama wake basi mamilioni ya watu ambao wamekuwa wakipata matibabu kupitia mfuko huu watakosa huduma. Tofauti na hilo, hospitali zote zinazodai malipo kutoka NHIF zitayumba kwasababu utaratibu uliopo ni kwamba wagonjwa wanapata huduma hospitalini kwanza na malipo kutoka NHIF yanafuata baadaye. Famasi ambazo hazipo hospitalini na huhudimia wagonjwa wa NHIF nazo zitayumba kama bado hazijapata malipo kutoka NHIF. Kama hospitalini, famasi hizi hutoa huduma kwanza na hutegemea malipo kutoka NHIF baadaye. Malipo haya hufanywa kila baada ya miezi mitatu ikimaanisha kwamba katika wakati wowote, famasi inayo hudumia wagonjwa wa NHIF huwa ina malimbikizo ya malipo ya miezi mitatu kutoka shirika la bima ya afya.

Waziri wa afya Mhe Ummy Mwalimu ameeleza changamoto mbalimbali zinazo sababisha shirika hili kuanguka na amependekeza mabadiliko kadhaa. Changamoto moja inahusu wanao jiunga kwenye mfuko huu wakiwa tayari ni wagonjwa. Kutokana na kauli hiyo, inawezekana kwamba NHIF haifanyi uchunguzi wa kina wa wanojiunga kwenye mfuko huu. Kwa kawaida, kwenye bima zingine za afya, lazima ijulikane kama mwanachama mpya anaumwa magonjwa mbalimbali kama kisukari, presha au magonjwa mengine ambayo haya ambukizi. Uchunguzi huu huchangia kwa kiasi kikubwa gharama ya kifurushi cha kujiunga na kiasi cha matibabu ambacho bima humlipia mgonjwa huyu. Kwa mara nyingi, matibabu yoyote huwa hayafanywi mpaka muhusika achangie bima kwa muda wa miezi sita.

Kitu kingine ambacho Mhe Ummy Mwalimu alijaribu kutoa ufafanuzi ni kwamba wanachama ambao hawaugui mara kwa mara huwa lipia ambao huugua mara kwa mara na kwasababu hiyo, kuwa na wanachama wengi zaidi kunaweza kuka ongeza mapato mengi zaidi kwa shirika. Hili linaweza likawa kweli lakini ni muhimu kwa shirika hili kuweza kujiendesha kwanza liki hudumia wanachama waliopo kwanza na kuweza kulipa madeni yake yote kwanza. Kwa maelezo ya Mhe Waziri, itahitaji idadi kubwa sana ya wanachama wapya kuweza kulikomboa shirika. Yaani michango hii haiwezi kutosha kuliwezesha shirika kulipa madeni yote na kumudu kuwahudumia wanachama wapya wote kwa wakati mmoja.

Hoja nyingine ambayo Mhe Ummy Mwalimu alijenga ni njia ambayo serikali itatumia kuhakikisha kwamba NHIF inapata wachangiaji wapya. Mhe Ummy Mwalimu alisema kwamba hakuta kuwa na sheria inayo mlazimu mtu yeyote kuwa na bima ya NHIF kwa ulazima ila wananchi hawataweza kupata huduma mbalimbali bila ya kuwa na bima ya afya. Kwa mfano, kadi ya nida, laini ya simu, n.k. Mapendekezo hayo yanategemewa kupitishwa bungeni ili mabadiliko hayo yatekelezwe. Ni rahisi sana kutambua kwamba vipangamizi hivi havina tofauti sana na sheria na hata kama malengo ni mema, huwezi kumlazimisha mtu atumie fedha zake kama wewe unavyotaka.

Ili kuifufua NHIF, lazima serikali iingilie kati kwa kutoa fedha za kutosha baada ya tathmini ya kina kuhusu sababu ya shirika hilo kuanguka kufanyika. Michango ya ziada kutoka kwa wanachama wapya haiwezi kukidhi mahitaji ya shirika hili katika kipindi hiki.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania
View attachment 2347151
View attachment 2347152
View attachment 2347153
View attachment 2347154
Mfuko wa bima wa afya umechotwa pesa nyingisana
 
Mwisho wa siku NHIF itagoma tibu magonjwa yasiyoambukizwa
 
Kuna mwaka Bima ya Afya walimzawadia Naibu Waziri (enzi hizo) NISSAN Patrol mpyaaa
 
Back
Top Bottom