KERO Changamoto ya Mifumo Kutosomana kati ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Laoshi Laoban

New Member
Joined
Jul 26, 2025
Posts
1
Reaction score
0
Mimi ni yatima wa wazazi wote wawili. Tangu tarehe 16 Julai 2025 nimekuwa nikijaribu kuomba mkopo wa elimu ya juu (ngazi ya shahada) kupitia mfumo wa HESLB, bila mafanikio hadi sasa ninapoandika ujumbe huu.

Nikiwa Karagwe, nilianza mchakato wa maombi kwa njia ya mtandao. Kila nilipoingiza RITA verification number ya cheti cha kifo cha mama yangu, kilichotolewa na RITA, mfumo wa HESLB hunijibu kwa ujumbe usemao "Detail not found".

Baada ya kukumbana na changamoto hiyo, nilijitahidi kukusanya nauli kwa shida ili kuja Dar es Salaam na kufuatilia tatizo hilo ana kwa ana. Nilianza RITA, ambapo waliielekeza hoja hiyo kwa HESLB. Nilipokwenda ofisi za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, nao walidai kuwa tatizo linatoka RITA. Niliporudi tena RITA, nikaelezwa kuwa kuna tume ya pamoja kati ya RITA na HESLB iliyoundwa kushughulikia changamoto kama hizi.

Nilipouliza ni lini tume hiyo itakamilisha kazi ili niweze kuendelea na maombi, niliambiwa hawajui. Wakati huo huo, muda wa mwisho wa kuwasilisha maombi ya mkopo unakaribia.

Nimekwama. Sina msaada wa makazi wala malazi jijini Dar es Salaam. Niko hatarini kukosa fursa ya udhamini wa masomo kutokana na uzembe wa mifumo na mawasiliano duni kati ya taasisi hizi mbili.

Mimi ni yatima mpambanaji, niliyesoma shule za serikali bila msaada wa wazazi, na kufaulu kwa kupata Division One – Point 4 (PCB) katika mtihani wa Taifa kidato cha sita mwaka huu. Ndoto zangu sasa ziko hatarini kuzimika kwa sababu ya kikwazo hiki ambacho siyo cha kiakili wala kimatokeo, bali cha kiofisi.

Naomba sauti ya wanyonge (The voice of voiceless people)- JamiiForums na wadau wengine — kunisaidia kupaza sauti hii. Naamini si mimi peke yangu niliyeathirika na tatizo hili.
 
Hii ni issue kwa wanafunzi wa vyuo wasio na uwezo wa kujisomesha.Itakulazimu tu upambane mpaka mwisho kwa kusumbua hizi taasisi.Kama ni malazi omba hata marafiki ulionao karibu hapo wakuhifadhi kwao ukitafuta solution au nenda ripoti chuo ukisubiri hii habari ikae sawa.
 
MFUMO HUU WA KUOMBA SCHOLARSHIP HESLB UNASUMBUA UKIJAZA RITA VERIFICATION NUMBER INALETA UJUMBE 'Error occured Please try again later' na namba ni sahihi, nimejaribu zaidi ya 100 times usku na mchana ila bado.
 
MFUMO HUU WA KUOMBA SCHOLARSHIP HESLB UNASUMBUA UKIJAZA RITA VERIFICATION NUMBER INALETA UJUMBE 'Error occured Please try again later' na namba ni sahihi, nimejaribu zaidi ya 100 times usku na mchana ila bado.
Suluhisho lake linaweza kuwa nini, umeshafanikiwa?
 
hawa jamaa kweli wanazingua, mimi mwenyewe nimekwama kwenye hicho hicho kipengele na siweze kuendelea na maombi huku muda una yoyoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…