Changamoto ya PF3 kwa miaka 15+ [2008-2024] Tafsiri yake ni nini ?

apk

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2023
Posts
260
Reaction score
555
Habari za muda wakuu.
Kwenye kupitapita humu mtandaoni nimekutana na uzi wa wadau mbalimbali katika nyakati tofauti tofauti

Ukizungumzia upatikanaji wa huduma ya afya ambayo ni muhimu sana kwa majeruhi wowote iwe ni wa ajali,wizi, nk ambayo inalenga kuwapatia taarifa za majeruhi na tukio husika alilokumbana nalo.

Kwa ufupi ni kwamba hata kama mtu ameiba amepigwa huko akifika hospitali atibiwe kwanza hata kama mtamfunga pingu au kuwa chini ya usalama cha msingi arudi katika hali ya unafuu ndipo taratibu zingine za kiusalama ziendelee.

Kuwepo kwa nyuzi za PF3 tangu 2008-2024 ni dalili tosha kwamba suala hilo halijashughulikiwa ipasavyo.

Kupoteza muda kufuatilia PF3 wakati mtu anapambania uhai ni jambo la kikatili sana ambalo linaonyesha ni namna gani wahusika hawana utu kufikiria hata kuna ndugu zao wanaoweza kukumbana na changamoto ya kudaiwa PF3 wakati wako katika hali mbaya kiafya.

Sijawahi kukutana na changamoto hii au ndugu yangu wa karibu lakini kwa nyuzi nilizosoma za wadau zinaumiza sana kuona ni kwa namna gani ambavyo tuko nyuma ya wakati.

PF3 sio discusion ya kukaa miaka 16+ ni suala linalogusa afya na uhai wa watanzania moja kwa moja ambao tayari wana matatizo kibao yanawaandama na ugumu huu wa maisha mtu anajifia hospitali mkishuhudia kisa PF3.

Mdau mmoja anaongea kwa uchungu kwamba "PF3 ni kiungo gani " kwa sababu inapewa kipaumbele sana bila kujali uhai wa majeruhi.

Tafsiri yake ni kwamba wahusika hawaoni umuhimu wa kufanya mabadiliko yoyote katika sheria inayogusa suala la PF3 simply kwa sababu haiwagusi au hawajali tu ?
Na hili linamaanisha kama document moja tu inasumbua hivi je masuala mengine tutaweza kweli?
Ama tafsiri yake ni kwamba wapiga kura tumechokwa kiasi hiko?

Ninaamini kabisa hili suala linaweza kuwekwa sawa kwa pande zote mbili amba
1.Kuokoa uhai[Kubwa kuliko yote]

2.Kufuatilia taarifa uhalali/uhakika wa taarifa zinazotolewa na majeruhi/mashuhuda na kufanya maamuzi sahihi wakati tayari wameshaokoa uhai.

Ushauri wangu kwa wahusika.
Kama bado kuna changamoto hiyo tunaomba wahusika waifanyie kazi kwa sababu kuna watu wanapoteza ndugu/marafiki/wazazi/walezi/watoto kwa sheria ambazo kwa wazi kabisa zinakatili uhai ambao ni haki yao kikatiba.
 
Attachments

  • Screenshot_20241212-223052~2.png
    Screenshot_20241212-223052~2.png
    50.3 KB · Views: 5
  • Screenshot_20241212-223212~2.png
    Screenshot_20241212-223212~2.png
    76.8 KB · Views: 4
  • Screenshot_20241212-223233~2.png
    Screenshot_20241212-223233~2.png
    87.7 KB · Views: 5
  • Screenshot_20241212-223233~3.png
    Screenshot_20241212-223233~3.png
    68.9 KB · Views: 4
  • Screenshot_20241212-223104~2.png
    Screenshot_20241212-223104~2.png
    82.7 KB · Views: 5
  • Screenshot_20241212-223827~2.png
    Screenshot_20241212-223827~2.png
    83.5 KB · Views: 4
  • Screenshot_20241212-223827~2.png
    Screenshot_20241212-223827~2.png
    83.5 KB · Views: 3
Habari za muda wakuu.
Kwenye kupitapita humu mtandaoni nimekutana na uzi wa wadau mbalimbali katika nyakati tofauti tofauti ukizungumzia upatikanaji wa huduma ya afya ambayo ni muhimu sana kwa majeruhi wowote iwe ni wa ajali,wizi, nk ambayo inalenga kuwapatia taarifa za majeruhi na tukio husika alilokumbana nalo.
Kwa ufupi ni kwamba hata kama mtu ameiba amepigwa huko akifika hospitali atibiwe kwanza hata kama mtamfunga pingu au kuwa chini ya usalama cha msingi arudi katika hali ya unafuu ndipo taratibu zingine za kiusalama ziendelee.
Kuwepo kwa nyuzi za PF3 tangu 2008-2024 ni dalili tosha kwamba suala hilo halijashughulikiwa ipasavyo.
Kupoteza muda kufuatilia PF3 wakati mtu anapambania uhai ni jambo la kikatili sana ambalo linaonyesha ni namna gani wahusika hawana utu kufikiria hata kuna ndugu zao wanaoweza kukumbana na changamoto ya kudaiwa PF3 wakati wako katika hali mbaya kiafya.
Sijawahi kukutana na changamoto hii au ndugu yangu wa karibu lakini kwa nyuzi nilizosoma za wadau zinaumiza sana kuona ni kwa namna gani ambavyo tuko nyuma ya wakati.
PF3 sio discusion ya kukaa miaka 16+ ni suala linalogusa afya na uhai wa watanzania moja kwa moja ambao tayari wana matatizo kibao yanawaandama na ugumu huu wa maisha mtu anajifia hospitali mkishuhudia kisa PF3.
Mdau mmoja anaongea kwa uchungu kwamba "PF3 ni kiungo gani " kwa sababu inapewa kipaumbele sana bila kujali uhai wa majeruhi.
Tafsiri yake ni kwamba wahusika hawaoni umuhimu wa kufanya mabadiliko yoyote katika sheria inayogusa suala la PF3 simply kwa sababu haiwagusi au hawajali tu ?
Na hili linamaanisha kama document moja tu inasumbua hivi je masuala mengine tutaweza kweli?
Ama tafsiri yake ni kwamba wapiga kura tumechokwa kiasi hiko?

Ninaamini kabisa hili suala linaweza kuwekwa sawa kwa pande zote mbili amba
1.Kuokoa uhai[Kubwa kuliko yote]
2.Kufuatilia taarifa uhalali/uhakika wa taarifa zinazotolewa na majeruhi/mashuhuda na kufanya maamuzi sahihi wakati tayari wameshaokoa uhai.

Ushauri wangu kwa wahusika.
Kama bado kuna changamoto hiyo tunaomba wahusika waifanyie kazi kwa sababu kuna watu wanapoteza ndugu/marafiki/wazazi/walezi/watoto kwa sheria ambazo kwa wazi kabisa zinakatili uhai ambao ni haki yao kikatiba.
Nasikia wale walipohangaika wakienda kucheza walianza tiba kwanza, mengine hayo mmh , baadaye !
 
  • Thanks
Reactions: apk
Moja ya upumbavu ambao huwa sielewi kwanini tunaundekeza ni hii PF3 na sijajuaga umuhimu wake mpaka Leo hii... Hii nchi inahitaji reformation sehemu nyingi sana kwakweli

CCM tokeni tumewachoka,
 
  • Thanks
Reactions: apk
Back
Top Bottom