A
Anonymous
Guest
Nimesoma katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na nilihitimu miaka mitatu iliyopita katika programu ya Bachelor of Technical Education in Civil Engineering.
Mwanzoni tulielezwa kuwa programu hiyo ingekuwa na faida mbili; mhitimu angeweza kuwa na sifa za uhandisi (Engineer) pamoja na sifa za kufundisha katika vyuo vya ufundi (VETA) au shule za ufundi.
Hata hivyo, baada ya kuhitimu tumekutana na changamoto kubwa. Programu hii haitambuliki na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), hivyo wahitimu wake hawasajiliwi kama wahandisi. Pia, katika baadhi ya vyuo vya kati hatutambuliki kama wakufunzi wenye sifa zinazohitajika.
Tumeendelea kupewa ahadi kuwa suala hili litafanyiwa kazi, lakini hadi sasa hakuna suluhisho lililopatikana. Kinachotuchanganya zaidi ni kuona MUST mwaka huu imeanzisha programu mpya ya Bachelor of Civil Engineering with Technical Education, ambayo inaonekana kumpa mhitimu sifa za uhandisi pamoja na uwezo wa kufundisha.
Hali hii imewaacha wahitimu wa programu ya awali wakiwa na maswali kuhusu hatima yao, kwa kuwa bado wapo wengine waliomaliza baada yetu na wengine wanaoendelea na masomo katika programu hiyo hiyo.
Changamoto si ajira pekee, bali hata kujiajiri imekuwa ngumu kwa sababu hatuna utambulisho wa kitaaluma unaotambulika rasmi; hatuwezi kusajiliwa kama wahandisi wala kutambulika kikamilifu kama walimu wa ufundi.
Tunaiomba Wizara husika, MUST na mamlaka za kitaaluma kutolea ufafanuzi suala hili na kutafuta suluhisho litakalowapa nafasi wahitimu hawa kutambulika na kutumia taaluma yao ipasavyo.