A
kwahiyo chuo kimewaingiza chaka?Kwa kifupi ni kuwa umesomea ualimu huwezi kuwa mhandisi, bali yule aliyesomea uhandisi kisha akarudi chuo kusomea ualimu kama wewe anaweza kuwa mwalimu au Mhandisi. Kama hujaelewa pitia huu uzi utapata majibu.
Wanafunzi ambao tumesoma Bachelor of Technical Education in Mechanical Engineering, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) tumeshindwa kusajiliwa na Engineers Registration Board(ERB) baada kuhitimu chuo na wakati tuna sifa zote.
Na kipindi tukiwa chuoni tuliambiwa tumekubaliwa kusajiliwa na ERB lakini sasa hivi tunapojaribu kufuatilia chuoni na kwa board yenyewe hatupati majibu.
Tunaomba kujua shida ni nini?
- Anonymous (ce6e)
- changamoto course education erb must wanafunzi
- Replies: 32
- Forum: Jukwaa la Ajira na Tenda
Kawaida sana hayo makozi mengi yanaanzishwa kuwapa pesa wakufunzi tu na nk jambo baya sana hili , kuna kipindi laboratory ilikuwa aina watu moja ya kozi iliyoanzishwa ilikuwa ni laboratory biotechnology wahitimu wako deep sana na waliajiliwa hadi wizara ya afya mahospitalini lakin baadae wizara ikawakataa kwaiho ni shidaNimesoma katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na nilihitimu miaka mitatu iliyopita katika programu ya Bachelor of Technical Education in Civil Engineering.
Mwanzoni tulielezwa kuwa programu hiyo ingekuwa na faida mbili; mhitimu angeweza kuwa na sifa za uhandisi (Engineer) pamoja na sifa za kufundisha katika vyuo vya ufundi (VETA) au shule za ufundi.
Hata hivyo, baada ya kuhitimu tumekutana na changamoto kubwa. Programu hii haitambuliki na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), hivyo wahitimu wake hawasajiliwi kama wahandisi. Pia, katika baadhi ya vyuo vya kati hatutambuliki kama wakufunzi wenye sifa zinazohitajika.
Tumeendelea kupewa ahadi kuwa suala hili litafanyiwa kazi, lakini hadi sasa hakuna suluhisho lililopatikana. Kinachotuchanganya zaidi ni kuona MUST mwaka huu imeanzisha programu mpya ya Bachelor of Civil Engineering with Technical Education, ambayo inaonekana kumpa mhitimu sifa za uhandisi pamoja na uwezo wa kufundisha.
Hali hii imewaacha wahitimu wa programu ya awali wakiwa na maswali kuhusu hatima yao, kwa kuwa bado wapo wengine waliomaliza baada yetu na wengine wanaoendelea na masomo katika programu hiyo hiyo.
Changamoto si ajira pekee, bali hata kujiajiri imekuwa ngumu kwa sababu hatuna utambulisho wa kitaaluma unaotambulika rasmi; hatuwezi kusajiliwa kama wahandisi wala kutambulika kikamilifu kama walimu wa ufundi.
Tunaiomba Wizara husika, MUST na mamlaka za kitaaluma kutolea ufafanuzi suala hili na kutafuta suluhisho litakalowapa nafasi wahitimu hawa kutambulika na kutumia taaluma yao ipasavyo.
View attachment 3673856