KERO Changamoto ya vifaa vya kufundishia kwa course ya Ordinary Diploma in Heavy Duty Equipment Engineering inaferisha vijana kwenye soko la ajira

KERO Changamoto ya vifaa vya kufundishia kwa course ya Ordinary Diploma in Heavy Duty Equipment Engineering inaferisha vijana kwenye soko la ajira

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Ubuju

Member
Joined
Mar 23, 2026
Posts
25
Reaction score
110
Habari wakuu,

Course ya Ordinary Diploma in Heavy Duty Equipment Engineering inayotolewa katika chuo cha ufundi arusha (ATC) ambayo ina miaka 5 toka iyanzishwe inapitia magumu sana kwa wanafunzi wanayosoma kwasababu hakuna mitambo ya kujifunzia uliopo ni fuvu tu haifanyika kama ilivyo hapo.

Tunaomba mamlaka husika kwa maana ya wizara ya elimu na chuo cha Arusha technical college watafute wadau ambao wataweza kutuletea mitambo mbalimbali pamoja na simulator za kujifunzia ili tuweze kuendana na soko course ni kubwa na ninzuri ila haina mazingira rafiki kabsa .

Mfano kama mitambo ikiletwa haitakuwa faida tu kwa course ya mitambo pekee ake pia course kama civil and highway,civil and irrigation mechanical, electrical na solar nazo zitapata fulsa kupitia miradi mbalimbali ambayo inafanyika kwa kushirikiana na Tanroad, Tarura, wizara ya maji na kilimo lakini pia itasaidia kuongeza kwa shortcourse kama za operator za mitambo pamoja na foreman kwa kazi za civil

Tunaomba mamlaka husika kuona hili kama fulsa kubwa kwa kusaidia kupunguza changamoto ya ajira kwenye kipengele cha uzoefu mwanafunzi akimaliza awe wa mitambo au civil anakuwa amepata uzoefu unaonekana lakini pia course ya ufundi wa mitambo hata kwa soko la nje bado ipo vizuri zaidi.

Industrialisation ya kweli huanza na wazawa na wakiwa na mazingira mazuri na rafiki.

1000223638.jpg
1000223647.jpg
1000223639.jpg
 
Back
Top Bottom