Changamoto za Ajira Portal

Academic qualification, unaanza kuweka shule au chuo na mwaka ulioanza na kumaliza.. Kule mwsho unaweka cheti ..

Proffesional unqtaja proffesional yako ila uwe umesajiliwa...

Kama engineer unapaswa usajiliwe na erb...
Kwahiyo sehemu ya professional naweza nikaacha wazi.?
 
Wakuu, kuhusu ku-attach certificate imekubali nadhani ishu ilikuwa ni mtandao unazngua...
Kijana, application letter inakuwa attached mwishoni kabisa pale unapotaka kuatyla maombo yako ya kazi ndio hiyo interface inapokuja.
 
Kijana, application letter inakuwa attached mwishoni kabisa pale unapotaka kuatyla maombo yako ya kazi ndio hiyo interface inapokuja.
Inatakiwa iwe imeandikwa kwa mkono au typing.?
 
1. Application letter andika kwa mkono "Usiandike kifupi hasa kwenye subject mfano "Ref: APPLICATION FOR PROJECT MANAGER POSITION AT TANZANIA BROADCAST COMPANY" mwisho usisahau signature

2: Hakikisha vyeti vinakuwa certified na mwanasheria, kuhusu verification certificates ni kwa wale waliosoma nje

3: Weka passport size upande wa kushoto juu kuna sehemu ya kuweka

4: Delete hiyo transcript ya pili

NB: Wengi huwa wanakosea kwenye barua Ajira Portal ukilipua na wao wanakulipua
 
Unadelete vio cheti ulichoapload tayari...????
 
Nilifungua acc karibu mwezi saaa ila nikilogion naambia INACTIVE ACC..!
 
Usisahau na namba ya kadi ya chama
 
Habari zenu wadau.

Kuna tatizo limeikuta akaunti yangu, kila ninapoapply ninapata automated answer ambayo inanionyesha siendani na academic qualification za hiyo ajira.

Ila tatizo ni kwamba niliwahi apply kwa post kama hiyo na nikaitwa hata kwenye interview ila katika post hii ndiyo napata hilo jibu.

Post ninayojaribu kuiomba ipo kwenye category ya Sociology, Political Science and Community Development. Nimehuisha taarifa via National Identification Number nimeweka kozi yangu katika category husika lakini bado napata hiyo feedback.

Nimejaribu kuwapigia kwa namba zao za help desk na malalamiko ila hazipatikani tangu Ijumaa, na nipo mbali na mkoa wa Dar so nashindwa kwenda ofisini kwao. Last resort nimeamua kuja kuomba msaada humu kwa yeyote anayeweza kunisaidia.

Natanguliza shukrani.
 
Pole sana mkuu, ngoja wazoefu waje
 
Dar hakuna ofisi za utumishi, zimeamishiwa Dodoma-UDOM.
 
Tatizo la mfumo limekuwa kero sasa hivi ulivyoboreshwa. Kwenye nafasi ya kazi kama wanahitaji Afisa maendeleo ya jamii. Kama kwenye sifa wakiweka tu awe amesoma Community Development basi wewe wa Sociology, wewe wa Social Work imekula kwako.
Zamani walikuwa wakiweka Afisa maendeleo ya jamii, au Afisa ustawi wa jamii au Mtendaji wa kata, hadi mtu aliesomea Lawa anaapply.
Mimi ndicho kilichonikuta kama hiko hiko na zamani nilikuwa naenda hadi kupiga interview ila kwa sasa naishia tu kuona tangazo linanigomea kisha basi.
Subiri labla wadau wanaweza kukupa suruhu.
Lakini tangazo likiandikwa course ile ile iliyosomea au zikiandikwa zote za kundi husika linaweza ila kukubali japo sijajua vya kutosha
 
Dah ebwana hii ishu ni utata. Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…