Wadau natumai mu-wazima, nimeupitia huu uzi wote, maana mimi pia nilikua napata shida kila nikimtumia mtu maombi ya udereva inaandika neno failed kama ilivyokua ikimtokea mdau aliyepost huu uzi (kwenye Ajira Portal, utumishi).
kwenye upande wa hii account, huyu mdau nilimjazia taarifa zake zote muhimu za elimu ya secondary, basic driving, leseni yake ya udereva nili-upload na kozi zingine alizosomea NIT nilizi-upload hapa kwenye category ya Academic qualification. kipindi cha nyuma ilikua nikimtumia maombi yanakubali lakini tangu utumishi walivyoupdate system nikituma maombi huwa yanagoma, yanaandika failed
sasa baada ya kupitia huu uzi, naombeni msaada wenu wa mawazo (1)Je nimjazie tena taarifa zake za udereva kwenye category ya professional kama wadau wanavyosema kwamba udereva ni professional labda inaweza kukubali? (2) Je haitokua shida taarifa zake kuwa kwenye category mbili za academic na professional? maana siku hizi mtu hauna access ya kuedit taarifa kwa kuzi-delete
naombeni msaada wenu, mwisho wa kutuma maombi ni date 16/09. pia nimejaribu kuwapigia simu utumishi via help desk namba zao hazipatikani.