Changamoto za biashara: Ajuza amenitapeli laki 3 ya tigo pesa kizembe sana

IKIRIRI

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2018
Posts
2,734
Reaction score
3,023
Mimi ni moja ya wafanya biashara wa simu pesa airtel money ,tigo pesa n.k.
Hii biashara zamani ilikuwa inalipa sana,kwa sasa move imepungua sana
1.wakala wako wengi sana
2.utapeli mwingi hasa km uliyemuweka hayuko makini.
Mwaka huu nimetapeliwa kizembe sana uwezi amini tena nilikuwa mimi mwenyewe.,niko makini sana na matapeli ila nimepigwa kizembe.

Alikuja bibi mtu mzima sana,kanipa simu nimsaidie kutoa laki4 ,simu yake ya techno inasamani kama elfu40 hivi.
Wakati niko kwenye mchakato kaniambia nipe laki3 nikampe mjukuu wangu yule pale na kweli nilimuona mjukuu wake,alidai anataka kusafiri haraka.

Kwa wakati ule nilikuwa na wateja so sikuzingatia sana na nilimwamini yule bibi.
Baadae nakuja kukumbuka bibi simuoni.
Nikasubiri kama 30 saa hivi ,nikaamua kuikagua simu ,nikakuta ina namba1 tu ,nilivyopiga haikupatikana mpaka sasa ninavyoandika hapa.
Wadau wenzangu nipeni uzoefu jinsi matapeli wanavyofanya.

Nimemsamehe coz najua nikifuatilia nitatumia zaidi ya laki3.
 
mimi pia nina biashara hii lakini mteja siwezi kumpa hela pasipo kuona msg kwa cm yangu pia nikiwa na mashaka nae namwomba niangalie msg kwa cm yake mpaka nijiridhishe ..nikiona ana haraka namwambia maduka yapo mengi unaweza kwenda mteja usimwamini hata kidogo hata awejee
 
Pole mkuu, matapeli nao huwa wanazeeka.
 
Mimi nilidhani uliiona balansi ndio ukatoa laki 3 yako mkuu, kumbe kushika simu ukaamini kuna milioni ndani
Ndio kaniambia nisaidie kutoa,ndani ya second akaomba nimsaidie laki3 atoa kwa mjukuu mara1
 
Mimi niko hivohivo kosa langu kumwamini ajuza
 
ogopa mteja anayejifanya ana haraka.ogopa mteja anayekuja na hela umwekee then anaghairi sekunde kadhaa anarudi umwekee.ogopa mteja anayetaka code au number zako za awakala ili amtumie mtu atoe hapo( may be unajuana naye na unajua pakumpata)
 
ogopa mteja anayejifanya ana haraka.ogopa mteja anayekuja na hela umwekee then anaghairi sekunde kadhaa anarudi umwekee.ogopa mteja anayetaka code au number zako za awakala ili amtumie mtu atoe hapo( may be unajuana naye na unajua pakumpata)
Real
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…