Changamoto za biashara (kiwanda cha tooku) EPZ - Dar

Silicon Valley

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2012
Posts
1,092
Reaction score
1,118
Wakuu salama?!

Naomba tujadili hili swala kwani sera iliopo sasa ni ya viwanda kwa ajili ya kuongeza ajira, wafanyakazi maisha yako juu, mishahara haitoshi, kwa upande wa pili uongozi wa kiwanda ushindani wa bidhaa sokoni mkali sana, kutishia kufunga kiwanda.

Wafanyakazi mshahara sh 100,000 @ mwezi nauli, chakula kazini juu yake WANAGOMA ili kuongezwa mshahara na meneja anasema hawezi ongeza hakuna wanachopata anaweza kuongeza 2.5% tu ili mshahara uwe 102,500=.. kweli kabisa hiyo ni 25 % tu ya gharama za maisha ya mfanyakazi wa hali ya chini kabisa lakini pia wapo watu wasio pata hata sh 50,000 tu @ mwezi.

Watanzania kwa malezi yao ya ujamaa wanawaona hao wawekezaji kama WANYONYAJI na HAWAAMINI kabisa wanachosema na kuwatishia Amani na maisha yao, aidha kwenda kuwashitaki mahakamani, Tuico n.k

Mwisho mwekezaji anachomoa pesa yake na kufunga kiwanda, hawezi kushitakiwa na PESA yake mwenyewe (yaani kwa kutumia pesa yake anawekeza halafu hiyo Investment yake inapeleka mahakamani na hajakiuka sharia kwani kima cha chini ni sh 80,000=)

Na sera ya mhe. Rais ni VIWANDA through Private sector in the same high competitive market?

Naomba TUJADILI
 
shida ni tija kwenye kilimo ni ndogo hivyo chakula kinachukua sehemu kubwa kuliko inavyostahili kwenye pato la mtanzania wa kawaida.
 
ni vizuri ingesema hao tooku wanazalisha nini kwanza, kusema tu soko ni la ushindani haitoshi.
 
kiukweli ukitaka kujua ugumu wa biashara au kampuni... anzisha ya kwako mwenyewe.. mda mwingine wawekezaji wanakuwa na hali ngumu... sokoni bidhaaa hazina market
 
Kiini cha tatizo ni hao wenye dhamana.Wanaruhusu bidhaa hadi zilizopo humu nchini kutoka nje. Haingii akilini sabuni za mche zinatoka hapo Kenya as if hatuna viwanda vya sabuni. It is a shame.
 
kiukweli ukitaka kujua ugumu wa biashara au kampuni... anzisha ya kwako mwenyewe.. mda mwingine wawekezaji wanakuwa na hali ngumu... sokoni bidhaaa hazina market

I salute you brother! Yaani ni shida sana, hususan biashara ambayo soko Lake ni la kutafuta. Unaweza ukakata tamaa kabla ya kufikia chochote
 
Usitetee wawekezaji kila kitu laza kiwe win win situation hasa wawekezaji wa kichina wanyonyaji sana unapotala kuanzisha investment yoyote lazima awe ameshafanya feasibility ya kutosha ikiwemo mishahara ya wafanyakazi kufanya kazi kiwandani kwa huo msharahara basi wewe na wawekezaji wako hatuwataki
 
Kiini cha tatizo ni hao wenye dhamana.Wanaruhusu bidhaa hadi zilizopo humu nchini kutoka nje. Haingii akilini sabuni za mche zinatoka hapo Kenya as if hatuna viwanda vya sabuni. It is a shame.

Nguo zao wanauza nje. Haziuzwi nchini. Unajua wakati nasikia EPZ nilijua kuna viwanda vya maana. Kumbe wanashona nguo tu, vitambaa wanatoa nje. Wanatengeneza kwa order.
 

kwako ni sawa HUWATAKI HAO lakini mwenzio hana ajila ya kumlipa hata hiyo 100,000 ana survive kwa hicho kiajira cha kichina uchwara na anawashukuru
 
Given all our high cost ya production, una uhakika kama mwenye kiwanda anatengeneza faida?
 
Nguo ni moja ya mahitaji ya lazima kwa mwanadamu (basic needs) hivi kweli kiwanda cha kuzalisha nguo kikose soko? Na wasi wasi na marketing strategies zao
 
Nguo ni moja ya mahitaji ya lazima kwa mwanadamu (basic needs) hivi kweli kiwanda cha kuzalisha nguo kikose soko? Na wasi wasi na marketing strategies zao

Kama jibu ni rahisi hivi basi vyetu vya tz visinge kufa .
Fikiri kwa upana kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…