Changamoto za biashara ya nyumba ya wageni

Changamoto za biashara ya nyumba ya wageni

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Hii biashara ina faida sana, ukiwa na vyumba 10 kwa 20,000 chumba kimoja na vyote vikapata wateja, una uhakika wa 200,000 kwa siku. Nyumba hizi hustiri wengi wenye uwezo wa kati na wa chini. Wale wasio kudumu hoteli kuanzia 100,000 kwa siku.

Changamoto moja kubwa ni ustaarabu, watu wengi hawajastaarabika. Mgeni akiondoka unagundua aliacha kinyesi au mkojo kitandani, wakati choo kipo chumbani. Kama una matatizo ya kukojoa ukiwa unelala ni kheri kusema wakati unachukua chumba.

Wizi, rafiki yangu aliweka portable A/C wageni walitambaa nazo, sijui walitoka nazo vipi lakini alikuta zimeibiwa. Fikiria alizitoa nje ya nchi moja karibu £150 bado gharama ya kufikisha Tanzania. Wizi wa shuka ni kawaida, wengine wakitoa 20,000 kama shuka ni nzuri ana kunja na kuweka kwenye bag.

Kutupa condoms chooni kunasababisha vyoo kuziba. Utaita wazibua vyoo kila siku na kati ya wateja 10, nane watatupa condoms na wadada wengine wanatupa tampons kabisa.

Tupeane changamoto zaidi.
 
Baadhi ya nyumba za wageni hutumika kama madanguro, unaingia huko ndani unanusa harufu za kondomu tu yaani hadi unakereka
 
♦️ Wamiliki wengi wa nyumba za wageni, hawasimamii ipasavyo, ukarabati wao wanawaza makusanyo tuu

♦️ Wafanyakazi wa usafi ni wa sanii wa kubwa na utaligundua pale ukichukua chumba mfululizo zaidi ya siku moja, shuka wanazirudia zile zile

♦️ Nyumba za kulala zinatakiwa zitengenezewe sound proof. Kuna mafirauni , madeva , wafanyakazi wanaokwenda semini, kazi yao ni kubeba magumegume yaliyokubuhu, ili ku justify fedha nyingi yanakuwa yanapiga kelele kama mashetani usiku kucha, sasa kama upo safarini umepumzika kwa uchovu utakoma usiku ule.sauti yote inaishia kwako
 
Hiki la kelele aluminium windows pia zinasaidia sana
 
Baadhi ya nyumba za wageni hutumika kama madanguro, unaingia huko ndani unanusa harufu za kondomu tu yaani hadi unakereka
Ukiwa na nyumba ya wageni reception lazima uwe na condoms za kuuza kama huna vending machine. Wateja wengine wanatafuta condom saa nane usiku.
 
usimamizi ndio kila kitu!

kimsingi inatakiwa mteja anapoachia chumba na kukukabidhi funguo ni vyema ukakagua chumba na yeye akiwepo ili kama kuna uharibifu wowote umetokea awajibike
 
Ukiwa na nyumba ya wageni reception lazima uwe na condoms za kuuza kama huna vending machine. Wateja wengine wanatafuta condom saa nane usiku.
Ni vizuri sana kwa wenye hizi nyumba kununua washing machine. Kuna jamaa alikuwa anafanya kazi ya kufua shuka za nyumba ya kulala wageni kwa mikono aliniambia kuna changamoto sana. Washing mashine itasaidia hata usafi wa matandiko uwe wa hali ya juu muda wote.
 
Kila baada ya miezi sita nunua shuka angalau 100 kama si 200.

Ukiwa unapiga pasi shuka zenye madoa na matobo tupa tu kama si kuwasaidia wenye uhitaji.

Uwe na laundry room yenye washing machine na meza za kupigia pasi.
 
Back
Top Bottom