Changamoto za biashara zinafanana

Changamoto za biashara zinafanana

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Leo napenda nizungumzie kuhusu changamoto za biashara hasa wakati wa mwanzo kabisa."Niweke angalizo kwamba changamoto za biashara ni zile zile haijalishi ukubwa au udogo wa biashara".

1. Changamoto ya kwanza ni wateja - Kupata wateja sio jambo rahisi katika biashara.mara nyingi tunafikiri ni jambo rahisi lakini wapo watu ambao hufikia hatua ya kutumia ndumba ili tu waweze kujaribu kuvuta wateja katika biashara zao na wengine hujikuta wakipoteza mtaji kabisa na kukata tamaa kwa sababu hio hio ya kukosa wateja.

2. Changamoto ya pili ni usimamizi wa muda:Hii ni changamoto kubwa hasa kutokana na ukweli kwamba ukitoa ujuzi, Muda ni asset ambayo inaongoza kwa kutumika vibaya na wajasiriamali wengi.Hata wafanyakazi maofisini nao huangukia katika tatizo lakutumia muda vibaya.

Karibu tujadili changamoto nyingine za kibiashara ambazo zinachangia biashara nyingi ama kufa au kuzorota.
 
Binafsi naona changamoto kubwa ni ukosefu wa ushirikiano ( hapa aliyeturoga wabongo katuweza ) na hulka ya kujichuchukulia perfectionists
 
Back
Top Bottom