Changamoto za kilimo cha machungwa msimu wa mwaka 2017

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,047
Reaction score
1,832
Mimi ni mkulima mdogo wa machungwa niko Muheza Tanga. Ila kwa mwaka huu wakulima wa machungwa tumeangukia kabisa kwani machungwa yanaoza wanunuzi hawaonekani Tumezoea ikifika mwezi huu wa Tisa mkulima ulikuwa unaringa kwani bei ya chini ni TSh 80 mpaka 100 shambani na wanunuzi wanakuwa ni wengi ila kwa mwaka huu mpaka sasa hivi mtu wa kununua japo Tsh 40 unamtafuta kwa na machungwa yanazidi kuoza na machungwa ya vuli nayo yameshakuwa tayari. Kweli kilimo kinachangamoto. Tunaomba serikali ituangalie na sisi wakulima wa machungwa(matunda) kama inavyoangalia mazao mengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jitahidi uanzishe kiwanda kidogo cha juice, nenda SIDO upate ushauri zaidi
 
We hujui kuwa Mr pombe kaua kilimo sasa tuko na viwandaaaaaaa,japo nilipo sasa namiliki viwanda kumi hongera siri Kali kwa kutuwezesha sisi maskini kumiliki viwanda,Nina cherehani 40 ukigawa kwa 4 unapata viwanda 10

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo kijiji gani mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…