Mkulima na Mfugaji
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,047
- 1,832
Mimi ni mkulima mdogo wa machungwa niko Muheza Tanga. Ila kwa mwaka huu wakulima wa machungwa tumeangukia kabisa kwani machungwa yanaoza wanunuzi hawaonekani Tumezoea ikifika mwezi huu wa Tisa mkulima ulikuwa unaringa kwani bei ya chini ni TSh 80 mpaka 100 shambani na wanunuzi wanakuwa ni wengi ila kwa mwaka huu mpaka sasa hivi mtu wa kununua japo Tsh 40 unamtafuta kwa na machungwa yanazidi kuoza na machungwa ya vuli nayo yameshakuwa tayari. Kweli kilimo kinachangamoto. Tunaomba serikali ituangalie na sisi wakulima wa machungwa(matunda) kama inavyoangalia mazao mengine.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app