Mathias kilongo
Member
- Jul 26, 2022
- 9
- 9
Kwenye maisha yetu ya kila siku usalama na haki ya kuishi ni jambo muhimu sana kuliko mahitaji yote lakin kwa dunia ya Leo swala la usalama wa maisha linazidi kuwa changamoto kila kukicha. Ni wazi utakubaliana na mimi kwamba dunia ya Leo kiujumla na kwa nchi moja moja zinakabiliana na matishio mengi sana ya usalama wa kuishi, serikali karibu zote dunian zinatenga bajeti kubwa kwa ajili ya kulinda raia wao na nchi zao kwa ujumla dhidi ya watu wenye nia ovu ama nchi nyingine kuivamia nchi nyingie na kusababisha vita ambavyo hugharimu maisha ya watu wengi wasio kuwa na Hatia.
mfano halisi ni juu ya kinachoendelea kati ya urusi na Ukraine zote hizi ni changamoto za KIUSALAMA, ukija africa karibu kila nchi kuna vita vya hapa na pale nenda kongo ndio usiseme miaka na miaka, nenda Africa ya kati, nenda Somalia ndio kila siku watu wanakufa tena wengine ni watoto ambao Hawajui na hawana Hatia yeyote ile hata hapa kwetu kumeshaanza kuwa na vyanzo ama viashiria vya kutaka kutupeleka kwenye changamo kubwa ya KIUSALAMA nani hajui kuhusu panya Road na makundi kama hayo ambayo siwezi kuyataja yote hapa
CHANZO NI NINI
Kwa mtazamo wangu kuna sababu nyingi sana zinazosababisha matatizo ya KIUSALAMA hapa duniani kwa kifupi nitaelezea machache muhimu hapo chini.
1- Ni tamaa za viongozi wengi kutaka kubakia madarakani kwa manufaa yao binafsi hata kama wanajua wazi wananchi hawawapendi Na wala hawawaungi mkono : hili tatizo ni kubwa sana hasa kwa nchi za kiafrika viongozi wengi wa kiafrika imekua ni Kama tamaduni zao kulazimisha kubakia madarakani hata kwa kubadili katiba za nchi husika hii hupelekea watu walioshindwa kuwaondoa hao viongozi kwa njia ya kura kuanza kuunda vikundi ambavyo huanza kushambulia baadhi ya watu wanaowaona wao ni moja ya wanaowaunga mkono hao viongozi waliong'ang'ania madarakani hii hupelekea kuwa na mvutano kati ya vyombo vya dola (polisi nk) ambayo mwisho wa siku ni kuanza kushambuliana kwa namna yeyote watakayoona wao inafaa iwe kisu ama bunduki na raia wengi wasiokua na hatia wameuwawa kwenye mazingira kama hayo.
2- Umasikini na kukosekana kwa ajira : hili nalo ni tatizo kubwa ambalo husabisha matatizo ya KIUSALAMA vijana wengi wanamaliza vyuo vikuu lakini ajira hakuna inafika mahali wanahisi kuna upendeleo na hii hupelekea vijana wengi kukata tamaa kitu ambacho huwapelekea kuamua kujiingiza kwenye makundi ya kihalifu kama ujambazi, uvutaji madawa ya kulevya na hata kujiunga na makundi ya kigaidi kwa takwimu zisizo rasmi inasemekana vijana kutokea nchi za Kenya na Tanzania wanaenda kujiunga na kundi la alshabab kwa kuahidiwa ahadi za kupata malipo mazuri hivyo hupelekea vijana kwenda kuungana kikundi hicho ambao baadae huleta madhara makubwa Africa na dunia nzima jaribu kukumbuka tukio la West Gate hapo Kenya je ni wangapi wasiokuwa na hatia waliuwawa!?.
3- Ni kuzagaa kwa silaha kiholela : watu wengi naamini mnajiuliza je waasi wanapata wapi silaha!? Ni lazima tujiulize lakini ukweli ni kwamba kuna watu wenye nia ovu wanafanya biashara ya silaha kinyume na sheria na huwauzia hao hao waaasi kwa lengo la kujipatia fedha bila kujali hizo silaha zitatumika kwa namna gani, si mara moja tumeona watu kutoka nje ya Africa (wazungu) wakikamatwa na silaha ambazo walizileta kwa lengo la kuziuza visivyo halali hili nalo ni tatizo la KIUSALAMA linaloisumbua dunia ya Leo
4- Ni malezi mabovu pamoja na kukua kwa teknolojia : Dunia ya leo ukitaka kujifunza namna ya Kutumia silaha yeyote huhitaji kwenda jeshini wala wapi ni kufungua you tube umemaliza kila kitu hio ina maana kwamba watu wanajifunza silaha kirahis na kutamani kuzitumia kirahis , kuhusu malezi watoto wengi sisi ni mashahidi wanaacha shule na kujiingiza kwenye vikundi vya kihuni ambavyo huingia mitaani na kuanza kukaba watu kupora watu na hata kuua watu hii ndio tunakuja kukutana na makundi kama panya Road n. K na kwa hili nawashauri sana jeshi la polisi kuwaangalia kwa jicho la tatu hawa vijana ukiangalia nchi kama msumbiji Leo majeshi ya Rwanda yapo pale kutoa msaada kutokana kuwepo kwa makundi ya kigaidi lakini chanzo ilikua ni vikundi kama hivi vilianza kidogo kidogo lakin wakapuuza Leo yanawatesa. Kuhusu malezi : wazazi wengi wameacha wajibu wao wa kuwasimamia watoto wao ipasavyo hii imepelekea kuwepo kwa watoto wenye makuzi ya ajabu na yasiyokua na misingi mema mema ya kuwaandaa kuwa watu wema ama kuwa viongozi waadilifu wa baadae hili nalo ni tatizo kubwa linalohitaji kufanyiwa kazi, mzazi mlee mwanao kwenye maadili ambayo kesho na kesho kutwa hayata kufanya uhuzurie vituo vya polisi ama mahabusu kumpelekea chakula na sabuni bali vikufanye uhudhurie mahafali ya kupanda cheo na kuapishwa viapo vitakatofu.
5- Ni mali : nchi kama kongo inateswa na mali zake yenyewe madini yamekua kama laaana hii nayo ni moja ya chanzo kikubwa cha Usalama kudhorota , Libya, iraq zote ziliponzwa na mali wakubwa walitamani mafuta na kuanzisha vita ambavyo vilipekea kuumiza watu wengi na mpaka Leo hakuna amani ni vurugu tupu.
SASA NINI KIFANYIKE
(1) - Viongozi waache kutaka kubaki madarakani milele ni lazima wafuate katiba za nchi zao na wakubali kubadilishana madaraka kwa njia ya amani.
(2) - ni muhimu vijana kuelimishwa elimu ya kujiajiri toka shule ya msingi ili hata wakimaliza vyuo vikuu waweze kuajiri wenzao na sio kuwaza kuajiriwa, serikali zifanye kila namna kuvumbua vyanzo vipya vya ajira ili kusaidia upatikanani wa ajira kwa wingi hii itasaidia vijana wengi kupata ajira na kumudu gharama za maisha.
(4) - nchi zilizoendelea ni lazima ziangalie na kuzuia uuzaji wa silaha kiholela hasa kwa makundi ya kigaidi kwa kuwa zinasababisha mauaji ya kiholela duniani kote.
Ahsanteni. Naomba kura yako

Upvote
7