Changamoto za kumiliki gari "unique"

Vocal Fremitus

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2016
Posts
1,287
Reaction score
6,648
Nakumbuka mwaka 2019 nilikuwa na Nissan Wingroad niliagiza kutoka Japan, nilikuwa nafanya kazi mkoa wa Ruvuma kijiji cha Namtumbo. Kijiji kizima kilikuwa kinaishangaa gari yangu, ilikua unique sana kwa wakati ule na ilikuwa inavutia. Sikuwa mdau sana wa speed.

Siku hiyo nimetoka nalo kwangu niende job, asubuhi kulikuwa na ukungu wa baridi barabarani. Haikuwa rahisi kuona mbele mpaka ufute fute kioo kwa ndani. Nikapambana mdogo mdogo kumbe mbele yangu kuna jamaa alikuwa anatoka msituni na mzigo wa kuni kawabebesha punda nashtuka paap hawa hapa. Kanyaga break nikamvaa punda mmoja. Mlango wa pembeni upande wa abiria wote chini, tairi upande huo huo nalo likachomoka. Kushuka nikagundua nimekata "bearing na hub yake yote"

Ikabidi safari iishie hapo. Tukamalizana na yule mkulima kisela. Nikaita fundi, gari ikapelekwa gereji. Kimbembe kikaanza ktk upatikanaji wa ile bearing kule Songea. Kila duka nililokuwa nazunguka nikiwatajia aina ya gari hawanielewi, wanaishia kuniuliza tu, wingroad? Ndio gari gani? Zunguka sana kona zote wapi. Nikaagiza Dar ambapo pamoja na gharama za usafiri mpaka inafika Namtumbo iliteketea kama 250k, inshort mpaka gari inarudi njiani na kufunga tairi nilimaliza kama 350k wkt ingekua hizi gari zingne hata 200k nisingefikisha.

Nilikaa nalo miezi mitatu mbele akatokea mkulima mwenye wenge la magari baada ya kuuza ufuta. Nikamsukumia.
 
Mi changamoto niliyoipata kwa mazda cx 5, ni kioo cha mbele nilitafuta sana aisee, baadae nikawa nimepata kioo pale mitaa ya gerezani kwa jamaa mmoja hivi muhidi halafu bei ya ikawa kironga 400k tu nikaweka kipya maisha yameendelea

Ukweli naenjoy sana kuwa unique tofauti na kufanana na wengine, kuna muda nikipata watu wanadhani gari ya ubalozi kwa unyama ilionao, tusiogope kuwa wa tofauti.
 
Hongera mzee. Ila kwa usawa huu pesa ilivyokuwa ngumu sitamani tena hizi rare cars. Nitakomaa na tako la nyani tu.
 
Kuna mwamba mmoja mzee wa mashauzi classic sana yupo mji kasoro Meli alinunua ka-ford focus kake miaka kama 5 iliyopita hivi, kanafanana fanana na Nissani xtrail hivi, kakaja kufa sensa ya kwenye switch, akiiwasha gari inawaka kidogo halafu inazima.

Mwamba kazungurukaaaaaaaaaaaaaaaaaa weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, mwisho akaambiwa atachongeshewa kwa laki 9 kwani maduka ya spea ya Dar, Moro na Chuga kote alikosa.

Ikabidi afuate ushauri wa kuchongesha kwa vishoka wa mjini, alivyochongesha sasa kuijaribu kagari kanawaka halafu hakadumu hata dakika moja kanazimika, laki kweli si pesa, laki 9 ndio ikawa ndio imekwenda hiyo.

Akampata muhindi mmoja akamwambia waifungue hiyo switch orijino waitume kiwandani China wakaifyatue nyingine, gharama yake akatajiwa Mil3, amesanda amelifunika na turubai gari lake akiwaza hiyo mil 3 anaweza kabisa kununua kavitz OLD model cha kitaa na akavimba vizuri tu.

UNIQUENESS ni NZURI ILA UWE NA MAPENEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
 
Hahahaaaa inaelekea mwamba alikua anawaoshea saaana na Ford yake bila kujua anatembea na chuma ulete. Mimi naona kibongo bongo bado tuna mda mrefu sana mpaka tuweze kua na variety ya spares za magari yote madukani kama ilivyo Nairobi. Gari nyingi unique upatikanaji wa spare madukani ni tatizo
 
Hahaaaaa,hakika aiseeeeeeee,sasa hv akiliangalia gari lake anabaki kusonya tu
 
Daah wakati Nairobi angepata kwa 180k
 
Nairobi wako mbele sana.
Kuna jamaa zangu wa Congo huwa wakikwama spare suluhu huwa nawalekeza Nairobi...huko wajanja wengi na wana kila aina za gari za kifahari.
 
Nairobi wako mbele sana.
Kuna jamaa zangu wa Congo huwa wakikwama spare suluhu huwa nawalekeza Nairobi...huko wajanja wengi na wana kila aina za gari za kifahari.
Nairobi, South Africa hata angeanzia hapo CMC ni agents za Ford.

Angeagiza hata huko UK. Asingeweza kukosa. Na bei ni rahisi kuliko huku bongo tunakoibiana.
 
Nina simu hapa display imekufa nilidondosha.Aisee simu ni kali,ila sijui ni aina gn?

Ukiweka laini texts na calls zinaingia lakini huoni ni nani?
Nimezunguka sanaaaaaa but wapiii,ndo basi tena nimeiweka tu sijui cha kufanya
 
Ukiwa na gari kama hizi lazima uwe unajua magari kweli! La sivyo utakutana na majanga kama haya.
 
Mimi Nilipo Gari Niliyonayo Zinahesabika Sasa Changamoto yake ni Kuwa Inachemsha.

Gari ni BMW 320i ya Mwaka 2002.

Hii Gari Ina Changamoto ya Kuchemsha yaani unatoka vizuri asubuhi utaona inaanzakupoteza nguvu na mvuke unatoka.

Gari ipo mkoani nyanda za Juu Kusini, Kwasasa Nimeiacha Garage Fundi anashauri nibadilishe Engine.

Kwa mwenye Uzoefu na haya magari na Aliyewahi Kupata Hii Changamoto kwa Haya magari.

Msaada Hata wa mawazo.
 
Hapa unahitaji msaada zaidi wa kina RRONDO na wajerumani wenzake [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…