Vocal Fremitus
JF-Expert Member
- Oct 20, 2016
- 1,287
- 6,648
Nakumbuka mwaka 2019 nilikuwa na Nissan Wingroad niliagiza kutoka Japan, nilikuwa nafanya kazi mkoa wa Ruvuma kijiji cha Namtumbo. Kijiji kizima kilikuwa kinaishangaa gari yangu, ilikua unique sana kwa wakati ule na ilikuwa inavutia. Sikuwa mdau sana wa speed.
Siku hiyo nimetoka nalo kwangu niende job, asubuhi kulikuwa na ukungu wa baridi barabarani. Haikuwa rahisi kuona mbele mpaka ufute fute kioo kwa ndani. Nikapambana mdogo mdogo kumbe mbele yangu kuna jamaa alikuwa anatoka msituni na mzigo wa kuni kawabebesha punda nashtuka paap hawa hapa. Kanyaga break nikamvaa punda mmoja. Mlango wa pembeni upande wa abiria wote chini, tairi upande huo huo nalo likachomoka. Kushuka nikagundua nimekata "bearing na hub yake yote"
Ikabidi safari iishie hapo. Tukamalizana na yule mkulima kisela. Nikaita fundi, gari ikapelekwa gereji. Kimbembe kikaanza ktk upatikanaji wa ile bearing kule Songea. Kila duka nililokuwa nazunguka nikiwatajia aina ya gari hawanielewi, wanaishia kuniuliza tu, wingroad? Ndio gari gani? Zunguka sana kona zote wapi. Nikaagiza Dar ambapo pamoja na gharama za usafiri mpaka inafika Namtumbo iliteketea kama 250k, inshort mpaka gari inarudi njiani na kufunga tairi nilimaliza kama 350k wkt ingekua hizi gari zingne hata 200k nisingefikisha.
Nilikaa nalo miezi mitatu mbele akatokea mkulima mwenye wenge la magari baada ya kuuza ufuta. Nikamsukumia.