Changamoto za uke wenza

Black Rose

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2011
Posts
243
Reaction score
171
Shosti wangu analalamika sana kuhusu kuishi maisha ya uke wenza.Mumewe alimuolea mke mwenza na toka wakati huo maisha yao ni ya shida tupu.

Kiwango cha maisha kimeshuka sana. Hakuna maelewano baina yake na mume, ukiachilia mbali mke mwenzie. Nyumbani kumekua kama kituo cha polisi.

Kwa wale wenye uzoefu na mitala, hebu mwageni siri ya mafanikio yenu tafadhali maana shosti anakaribia kupata wazimu!

========



Ndoa ya mitara ni ndoa ya aina gani?

Ndoa ya mitara ni ndoa kati ya watu wawili ambao mmojawapo ana au anaweza kuwa na mwenzi au wenzi wengine pia (mitara au upali), hususan ndoa ya mwanamume mmoja na wanawake zaidi ya mmoja.

Ndoa ya mitara ni ndoa ambayo ipo kwa baadhi ya makabila ya Afrika na kwa upande wa watu wenye dini ya Kiislamu. Ndoa hii humruhusu mwanamme kuoa mke zaidi ya mmoja.

Hata hivyo, ruhusa hiyo ya wanaume imegeuka kuwa shubiri kwa wanawake ambao kwa kawaida hakuna anayefurahia kuona kwamba mumewe anaongeza mke wa pili. Tafsiri ya uke wenza ni mume kuoa zaidi ya wake wawili ambapo wanawake hao wanalazimika kuishi pamoja kwa kupata huduma zote kutoka kwa mume mmoja.

Historia katika vitabu mbali mbali vitakatifu inaonesha kwamba Nabii Ibrahim hakusalimika na mikasa ya wanawake na uke wenza ambapo mke wake wa kwanza Bibi Sara ndiye aliyemshawishi kuoa mke wa pili kwa ajili ya uwezekano wa kupata mtoto baada ya wao wawili kuishi muda mrefu bila ya mafanikio.

Hata hivyo Bibi Sara wakati akiwa katika uke wenza huo na bibi Hajra, alipambana na vituko vingi ambapo wivu ni moja ya matatizo makubwa katika uke wenza kwa wanawake wawili. Kwa nini wanawake wengi wa Kiislamu wanachukizwa na tabia ya kuishi uke wenza ambao ndio chanzo cha kuyumba kwa ndoa na baadaye kuvunjika huku watoto wakikosa matunzo ya baba na mama na wengine kuingia katika ajira ngumu za watoto?

Mama mmoja ambaye amepewa talaka na mumewe aliyeishi naye kwa zaidi ya miaka 15 na kubahatika kupata watoto 6 alisema mwanamume anapooa mke wa pili ambaye anakuwa mpya wanakuwa na dharau kwa mke wa kwanza ambaye anaonekana kama aliyechakaa.

Alijitolea mfano, akisema mumewe aliamua kwenda kuoa mke wa pili baada ya yeye kuwa na watoto wengi huku mumewe akidai kwamba hapati muda wa kustarehe au utulivu wa hali ya juu kutokana na kelele za watoto.

“Unajua wanaume ni watu wa ajabu sana ukiwa hujapata mtoto ni sababu kubwa ya kupewa talaka, lakini wakati mwingine wanaamua kuoa mke wa pili kwa sababu tu mke wa kwanza amekuwa na ulezi wa watoto wengi na yeye hudai kukosa muda wa kufanya starehe au utulivu katika nyumba,” alisema.

Lakini alisema wanawake wengi hawapendi uke wenza kwa sababu wanaogopa ushirikina, ambao unatokana na ushindani wa mapenzi kwa wanawake wawili au watatu hadi wanne waliopo katika ndoa moja. Kauli hiyo iliungwa mkono na na mama mwingine mkazi wa kijiji cha Nungwi ambaye alidai kwamba ndoa yake ilivunjika mara alipoingia katika uke wenza, ambapo alipambana na vitimbi vya ushirikina.

“Sisi wanawake wengine tunaposikia mume wako kaoa mke wa pili basi tupo tayari kudai talaka kwa sababu uke wenza hutawaliwa na uswahili wa ushirikina wa ushindani wa mapenzi,” alisema. Karani wa Makahama ya Kadhi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Asma Fransic alisema kesi nyingi zinazofikishwa katika mahakama hiyo ni wanawake kudai talaka kutokana na wanaume kuongeza mke wa pili na matokeo yake kuanza kutelekezwa.
Asma alisema katika mwaka 2012 zaidi ya ndoa 10 zilisambaratika kwa talaka kufuatia wanawake kulalamika kuingia katika ukewenza ambapo malalamiko ya matunzo na kutelekezwa yaliibuka. “Ndoa nyingi zinavunjika kutokana na malalamiko ya wanawake kuishi katika ukewenza huku wakikosa huduma muhimu za matunzo na watoto kutelekezwa,” alisema.

Alisema mapema mwaka 2012 wanaume 5 walipigwa faini na Mahakama ya kadhi na kutakiwa kuwasilisha fedha za matunzo kwa watoto wao baada ya kutengana. Mhadhiri mwandamizi wa Chuo kikuu cha taifa Zanzibar (SUZA), Dk Issa Haji Ziddy alisema wanaume wengi wanaamua kuongeza wake bila ya kuzingatia masharti yaliyowekwa katika Quran ambapo unatakiwa kuzingatia suala zima la matunzo kwa mwanamke na watoto.

Alisema wanaume wanaamua kuoa wake zaidi ya watatu lakini hawazingatii masuala ya uwezo katika kuwahudumia wanawake na watoto. “Wanawake wengi wanachukia uke wenza kwa sababu wanaume wanapoamua kuongeza wake hawazingatii masharti ikiwemo uwezo wa kuwahudumia wake na watoto,” alisema.

Dk Ziddy alisema upo umuhimu wa kuwepo kwa mkataba wa ndoa ambao utaweka masharti kwa wanandoa ikiwemo suala la kutunza watoto pamoja na mgawanyo wa mali ili kuepuka wanawake kutelekezwa wakati wanaume wanapoamuwa kuongeza mke.

“Zipo nchi za kiarabu tayari wanao utaratibu wa mkataba wa ndoa ambao unaweka masharti ya ndoa mwanamme kabla ya kuoa mke wa pili kwanza anatakiwa kwenda mahakama ya kadhi ambapo ataulizwa anaongeza mke wa pili kwa sababu gani na vipi atamtunza mke wa kwanza pamoja na watoto,” alisema Ziddy.

Ofisa mwandamizi wa taasisi ya Save Children Fund Zanzibar, Mubaraka Maaman alisema kusambaratika kwa ndoa ndiyo chanzo kikubwa kwa watoto kuingia katika ajira ngumu na kuacha shule.

Maaman alisema utafiti uliofanywa na Shirika la Save Children Fund umebaini kwamba zaidi ya watoto 20,000 Unguja na Pemba wamejiingiza katika ajira ngumu ya watoto ambayo chanzo chake ikiwemo kusambaratika kwa ndoa na wanaume kutelekeza wake zao.

Alisema migogoro ya ndoa kwa wanaume kuacha wake zao ndiyo chanzo cha kusambaratika kwa ndoa na watoto kujiingiza katika ajira mbaya ya watoto ambayo hatimaye watoto kuacha shule. “Ajira mbaya za watoto chanzo chake kikubwa ni kusambaratika kwa ndoa kwa wanaume kutelekeza watoto zao na kukosa haki za msingi ikiwemo elimu,” alisema.

Kadhi mstaafu wa wilaya ya mjini Mwanakwerekwe Ali Suleiman alikiri kuwepo kwa tatizo la wanaume kuamua kuongeza mke wa pili au watatu bila ya kutekeleza masharti ya ndoa ikiwemo matunzo kwa mke na watoto. Alisema hiyo ndiyo moja ya sababu kubwa kwa wanawake kuamua kudai talaka kwa sababu kwa wanaume wengi wanaamua kuongeza mke wa pili baada ya kuanza kumchoka mke wa kwanza kwa sababu mbali mbali.

“Sheria ya ndoa ipo wazi sana mwanaume anapoongeza mke wa pili, kwanza anatakiwa kutoa kutoka nyumba zawadi ya aina yoyote ile lakini pia anatakiwa kutoa taarifa kabla kwa mke wa kwanza kuhusu mipango yake ya kuoa mke mwingine,” alisema. Lakini alisisitiza na kusema suala la uwezo ni muhimu sana ambapo linakuja moja kwa moja katika matunzo ya mke na watoto ili kuepuka utekelezaji wa familia.

Kadhi wa wilaya ya Kaskazini Unguja ambaye hufanya kazi zake katika Mahakama ya Mfenesini, Khamis Kassim Haji, alisema katika kipindi cha miezi saba jumla ya talaka 26 zimetolewa ambazo zimedaiwa na wanawake kwa sababu ya kukataa kuishi katika mazingira ya uke wenza.

“Ni kweli wanawake wengi hawapendi kuishi katika mazingira ya ukewenza kwa sababu mbalimbali, lakini moja kubwa wanaume wanaamua kuongeza mke wa pili kwa ajili ya kumkomoa mke wa kwanza tu,” alisema. Baadhi ya wanaume wanadai kwamba wanalazimika kuongeza mke wa pili au wa tatu kutokana na visa vya wanawake ikiwemo wivu wa kupindukia pamoja na kushindwa kutekeleza huduma za ndani ya ndoa.

Utafiti mdogo wa kihabari uliofanywa na TAMWA kutembelea Mkoa wa Kaskazini Unguja huko Nungwi, wanaume wanadai kwamba wanakosa huduma za mapenzi ambapo wanalazimika kuoa wake wengine zaidi. Ali Juma mkazi wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja alisema wanaume wengi wa kijiji hicho wamelazimika kuoa wake kutoka mkoa jirani wa Tanzania Bara huko Tanga kwa ajili ya kupata utulivu wa mapenzi.

“Unajua sisi wake zetu wa hapa kijijini hawatupi mapenzi na utulivu na ndiyo maana tunalazimika kwenda Tanga kuoa wake wa huko ambao ni mafundi katika mapenzi ya ndani,” alisema. Kombo Faki mkazi wa Potoa alisema wanaume wanaoa wake zaidi ya wawili au watatu kwa ajili ya kupunguza jeuri au kiburi cha mwanamke kinachotokana na wakati mwingine dharau ambayo inatokana baada ya kuishi kwa muda mrefu na kuzoeana.

“Ni kweli ukitaka kupunguza jeuri ya mwanamke basi muolee mke wa pili ataacha mara moja kiburi chake na kuanza kurudisha mapenzi ya mumewe,” alisema Kombo. Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Hassan Othman Ngwali alithibitisha kuwepo kwa tatizo la uke wenza na kuwepo chanzo cha talaka pamoja na wanawake kutelekezwa na watoto.

Alisema sheria ya kadhi ipo wazi ambapo mwanamume anatakiwa kulinda matunzo ya watoto na kudhibiti tatizo la utelekezaji wakati anapooa mke mwingine au uke wenza. “Uke wenza kwa kawaida hauna matatizo isipokuwa wanaume ndio wenye matatizo ambao wanashindwa kutekeleza masharti ya ndoa, matokeo yake wanawake wanaogopa au wengine hudai talaka mara tu wanaposikia au kupewa taarifa ya uke wenza,” alisema.

Baadhi ya changamoto za uke wenza

1.Ushirikina

Hii inasababishwa na wivu wa kimapenzi kwa kuwa kila mwanamke anakuwa anataka kupendwa zaidi na mme wake na apatiwe haki na matunzo hivyo hushawishika kutafuta mbinu ya kufanikisha hitaji lake.

2. Kushuka kiuchumi
Kutokana na kuongezeka kwa familia mara nyingi mwanaume huelemewa na mzigo wa matunzo wa familia zaidi ya moja na hivyo kujikuta uchumi ukishuka.

3. Magonjwa ya zinaa
Mara nyingi wanawake walio kwenye ndoa hizi hulazimika kutafuta wanaume wengine wa kuwa nao pindi mme anapokuwa kwa mke mwingine ili aweze kujikimu haja za mwili wake kwa kipindi ambacho mwanaume anakuwa kwa mke mwingine.

4. Chuki na visasi
Wanawake wengi walioolewa pamoja huwa hawapendani na hivyo huwa na chuki na kulipizana visasi jambo ambalo huhatarisha amani ya familia.

5. Magomvi baada ya mme kufariki dunia
Mara nyingi mme akifalriki dunia watoto wa marehemu na wake zake huingia kwenye mgogoro mkubwa wakati wa kurithi mali kwani kila mmoja huona yeye ndie ana haki ya kurithi mali.

Michango ya wadau:
----
----
 
Sina uzoefu ila nna swali. . . Yeye alipokubali aongezewe mke mwenza alitegemea nini? Ofcourse lazima kiwango cha maisha kishuke kwasababu mume kaongeza mtu mwingine wa kumhudumia.
 
Ukewenza unakuwepo kwa sababu nyingi lakini daima huwa ni ndani kwa wandoa wenyewe aidha mme au mke lakini mara nyingi huwa kama si tamaa ya mme basi mke hatimizi ipasavyo wajibu wake kama mke. Ushauri wangu wa bure ni huyo shosti wako awe mkweli kwa kubainisha chanzo cha mme kusepa nje na kama ni yeye basi akiri mapungufu yake kwa shemejio na aomyeshe kwa matendo kuwa anajuta na kujirekebisha.
 
Daah siwezi kugawana mapenzi huku nikijua!

Hivi ukiwa unaolewa, kile cheti cha ndoa si kuna mahali unajaza ndoa ni ya mke mmoja ama wengi.....sasa kama yeye alikubalina na kuwa itakuwa ya wake wengi basi she volunteered her own injury!

Btw; kwa wale wenye kuruhusiwa mke zaidi ya mmoja, si unaweza pia kusema ni ya mke mmoja kama huna lengo la kuoa wengi! Black Rose hapa utanisaidia najua hapa una uelewa ziadi yangu.
 
Sina uzoefu ila nna swali. . .
Yeye alipokubali aolewe mke mwenza alitegemea nini? Ofcourse lazima kiwango cha maisha kishuke kwasababu mume kaongeza mtu mwingine wa kumhudumia.

I think, yeye alikuwa wa kwanza; mumewe akaongeza mwingine, if l got her right!
 
Ngoja FaizaFoxy aje akupe maujuzi, sisi wengine it is unthinkable!
 
Maisha ya watu wawill ni magumu... Maisha ya watu watatu ni balaa.. Maisha ya watu wanne ni kiama..

Kikubwa..shosti wako ajiulize alifuata nini kwenye mitala kwa kisingizio cha mapenzi.. kwani ni vigumu kutushawishi eti kuna mapenzi yanaweza kugawanywa kwa watu zaidi ya wawili...

Kama mambo yalikuwa ni uchumi.. basi ajipige moyo na kujikwamua kiuchumi mwenyewe..Kila kitu kinawezekana ni kujiamini kuwa utaweza.. kumbuka chanzo cha furaha ni yeye mwenyewe na kujiamini kuwa anaweza yote kwa kumtumaini Mola.. Aachane na huyo vampire..
 
Mila inahusu hasa hapo.
Kwa waliotoka kwenye makabila polygamy, wanaishi sana
Ila lazima mme awe MWANAMME, kama ni kivulana hiyo nyumba ni kvumbi na jasho.

Hata hivyo kuna chalenji zake
Hasa WIVU kwa wakewenza, ndo usiseme
 
I think, yeye alikuwa wa kwanza; mumewe akaongeza mwingine, if l got her right!

Ndio niliyomaanisha Kaunga. . . sijui ndio nilitakiwa kutumia neno gani hapo.
 
Kama ni urgent sana kama ulivyosema kwenye kichwa cha habari bora arudi kwao.
 
Huyu dada kama ni ndoa ya kiislam, hapo imani ndio inatakiwa kwani mwanaume ameruhusiwa kuoa wanawake 4, Hii ni kulingana na sheria ya dini ya kiislam.

Lakini mwanake kama mwanamke unaweza kuta kuna mambo ambayo umeyasababisha mpaka mumeo akaamua kukuolea mke mwenza, Labda ungejiuliza wewe mwenyewe ni vipi mpaka mmeo akafikia hatua hiyo.

Kwa sababu kama mwanaume alieishika dini barabara, mwanamke hata afanye nini hakuachi, sana sana takuongezea mke mwingine.

Sasa dada labda shogaako kuna alilolifanya kwa mumewe mpaka akaolewa mke mwingine.
 
Sina uzoefu ila nna swali. . .
Yeye alipokubali aongezewe mke mwenza alitegemea nini? Ofcourse lazima kiwango cha maisha kishuke kwasababu mume kaongeza mtu mwingine wa kumhudumia.

Dini ya kiislam inaruhusu, hata na zaidi. Na kuna taratibu za kufuata kama unapata pingamizi kutoka ktk familia
 
Kama yeye ni mke mkubwa basi asijipe BP kwani ukubwa dawa,na alipo olewa na huyu mume alitakiwa ajipange sababu dini yao inaruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja na kwani mume alimwambia kua atakua peke yake maisha?

Kama kakubali matokeo atulize akili yake ashukuru mungu aendele na kupewa zamu leo yeye kesho mwenzie alee wanawe la hawezi nadhani bora arudi nyumbani akapumzike kidogo ili akili yake ikae sawa na nyumbani wazee watamuelimisha, mpe pole manake kama namuona roho inavyouma.
 
Uke wenza siyo maisha,mapenzi hakuna,hujui hata mwanaume kalala wapi,dharau huwa nyingi,hata uwezekano wa kupata marazi ni mkubwa sana. Kama anajiweza aanze mdogo mdogo.
 
Kama dini inaruhusu anatakiwa akubali yote yaliotokea, cha msingi hawe mvumilivu tu nakujikita zaidi kuangalia watoto, wake kama mume ajampa talaka bado ni mume wake, anachotakiwa asijipe presha ingawa ni ngumu mwisho wa siku meme anarudisha mapenzi si hunajua tena kule bado penzi bichi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…