A
Watendaji wapo bize kupambana na magaidi (upinzani). Hawajishughulishi na shida zetuMimi ni mkazi wa Newala -Mtwara, kila Mara Tumekuwa na changamoto ya kukatika umeme , tunashindwa kufanya kazi zetu zinazotumia umeme; mda mwingine siku mbili mfululizo bila kupewa taarifa yoyote, kwa Leo pia Toka jana usiku Kucha na Leo mchana kutwa hakuna umeme, tunatamani kujua tatizo ni nini?
Habari ndugu mteja,sio Newala pekeyake, mikoa ya Lindi na Mtwara umeme unasumbua sana kwa takribani miaka kumi sasa. ni nadra siku ikaisha bila umeme kukatika. Gesi inayozalisha umeme inatoka Lindi na Mtwara lakini umeme wa shida. Viongozi wapo tu na hakuna anayejali. Mwaka 2012 vurugu kubwa ya "gesi ya Mtwara" ilitokea kupinga dhulma kama hizi lakini watu waliishia kuuawa na kufungwa jela tu. Watu wamekata tamaa, wametulia tuu