Changamoto za wanufaika wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)

Changamoto za wanufaika wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)

Tony Laurent

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Posts
5,606
Reaction score
7,032
NHIF NI KILIO KINGINE CHA WATUMISHI

Kwanza nianze kwa kuishukuru serikali kwa kuanzisha huduma za bima kwa njia ya bima yaani NHIF ambapo watumishi umma kwa LAZIMA hukatwa bima ya afya bila chaguo la aina ya bima, nashukuru kwa sababu inatusaidia tofauti na kutoa hela zetu mfukoni hata kama tumetoa fedha zetu inadvance.

KERO
Kwa miaka kama mitatu mfululizo sasa NHIF wamekuja na utaratibu ambao kwa watumishi wa umma wa kitanzania imekuwa ni kero saaana kwa sababu unatuumiza wafanyakazi hasa walivyobadilisha masharti bila kuomba maoni yetu.

Awali mfanyakazi alikuwa anaweza kumuunganisha MME,MKE, WATOTO, WAKWE,NA NDUGU WENGINE Alimradi hazidishi idadi ya Watu 6 kwenye bima yake. Jambo hili halikuwa na shida kwa watumishi kabisa kwa sababu ilikuwa inajibu changamoto watumishi hawa.

NHIF ijue kuwa watumishi wa Tanzania waliowengi wamesomeshwa na ukoo yaani baba, mama kaka, dada, mjomba, baba mdogo, binamu nk.hivyo mfumo wa awalia ambao haukuwa unawabana namna ya kuwaunganisha wanufaika ulikuwa unamruhusu mtumishi kulipa fadhila kwa ukoo/ndugu waliowasomesha.

1: Kwa sasa imekuwa kinyume kwa sababu mfumo huu mpya uliobadilishwa bila kuhusisha watumishi wala vyama vya wafanyakazi kama TALGWU unatutesa watumishi kwa sababu unatunyima fursa ya kusaidia waliotusaidia wakati tunasoma. Mfumo huu unaruhusu MME, MKE, WATOTO, WAZAZI NA WAKWE TU bali ndugu wengine nje ya hao waliotajwa hapo juu hawaruhusiwi.

2: Mfumo wa awali ulikuwa hauna ukomo wa Watu ulioamua kuwaunganisha mpaka mnufaika utakapoamua kubadilisha mtegemezi. Lakini sasa kuna ukomo wa wategemezi hasa watoto haohao niliowazaa mtumishi mwisho miaka 18 haijalishi anasoma au laa. Watoto hawa waliowengi wapo sekondari na vyuo wanalazimisha mzazi kukata au kulipia bima tena huko vyuoni wakati mtumishi huyu anakatwa na inawezekana hata bima yake haijatumika hata mara moja analazimika kutoa hela yake ya mfukoni kukata bima. Jambo hili linatuumiza sana wafanyakazi na linatufanya tuone bima hii haipo kwa ajili ya kusaidia bali kutuumiza.

USHAURI WANGU KWA NHIF
1: Kwa kuwa bima analipa mfanyakazi, NHIF kaeni na watumishi waamue ni watu gani waingizwe kwenye bima yake msiwapangie kwa nadharia zenu mlizonazo. Mlipokuwa mnakata hela hamkumuuliza mtumishi huyu kama anataka akatwe hicho kiasi au laa hivyo mwacheni aamue mtu wa kuwa mtegemezi wake.

2: Suala la umri wa wategemezi pia waachieni watumishi waamue ni umri gani kwao huyu mtegemezi atoke kwenye bima maana wao ndio wanaumia pindi mtoto huyu akipata matatizo ya kiafya.

Serikali pia inatakiwa kuingilia kati juu ya umri wa watoto. Kwa mfumo wa ajira wa sasa watoto wetu wanamaliza vyuo na kukaa hadi miaka 5 au zaidi hawajapata ajira popote na wakati wote wanakuwa kwa baba na mama zao, wazazi tunawajibika kwa lolote kipindi chote anapokuwepo nyumbani halafu mnakata bima akiwa na miaka 18 huu ni uonevu kabisa, NHIF mnatakiwa kujirekebisha mtuachie watumishi tuamue umri wa kumtoa watoto kwenye utegemezi. Mapendekezo yangu ingekuwa angalau miaka 25 baada ya kumaliza vyuo angalau digrii ya kwanza.

OMBI KWA WABUNGE
Najua humu ndani kuna wabunge mnatusaidia kutunga sheria, naomba mtusaidie kuliona hili maana tunaoteseka siyo sisi pekee yetu, wapiga kura wenu na hata nyie kwa namna moja mnateseka kama watumishi, tunaamini mmeungwa kwenye bima hii so maumivu tunayapata wote.

Ahsante.

NB: Nimeinakili mahali fulani nikaona niilete huku ili wanaohusika wachukue hataua stahiki.
 
Acha kuunga-unga yaan kwenye bima yako umuunge mpaka MKWE?
 
Changamoto kubwa ya NHIF ni wahudumu wa hospital kudharau wenye kadi za NHIF na wanaohitaji huduma. Kuna haja wapewe funzo kuwa ile kadi haimaanishi unatibiwa bure, maana wamejiwekea mtazamo kuwa kila mwenye kadi ni kama anaepewa msaada tu.

La pili ni mambo ya kuambiwa dawa hii ama huduma hii haipo kwenye BIMA. Sasa unajikuta una BIMA lakini bado unatoa pesa kupata dawa ama huduma husika, nadhani hili linakwenda kinyume na maana halisi ya kuwa na BIMA ya afya kama ikibidi kutoa pesa zaidi ya ile ambayo ushakatwa kwenye mshahara wako.

Kwa kifupi ukita huduma angalau yenye unafuu kwa kutumia kadi za NHIF ni uende hospitali kubwa ila hivi vizahanati vinavyoweka mabango makubwa kuwa wanakubali NHIF unaweza jikuta unalipia mpaka panadol kwa kisingizio haipo kwenye BIMA.
 
Mi nikajua unaongelea changamoto ya huduma na dawa?

Unataka ujaze mpka ndugu kwenye hiyo bima, kama walifanya hivyo walikosea sana. Hiyo bima inapaswa kuwa kwa mhusika, mume/mke na na watoto tena under 18.

Kwani ni kila mtu anafikia hiyo degree, na akifika 25 anakuwa kapata ajira?

Mifumo ya kijinga kama hii ndo inafanya watu wawe wazembe wazembe.

Watu wafanye kazi na wajitegemee habari ya kujaza wajomba na mashangazi kwenye bima ni ujinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bima ya afya inapoteza maana pale ambapo haijihusishi na magonjwa makubwa makubwa[emoji134][emoji134][emoji134]
 
Bima ya afya inapoteza maana pale ambapo haijihusishi na magonjwa makubwa makubwa[emoji134][emoji134][emoji134]
Hilo ndo jambo hasa la kupigia kelele, huwa sioni mantiki ya bima kuanza kuchagua dawa na magonjwa.
 
Namba 1 uko sahihi. Haiwezekani hela yangu halafu unipangie mtu wa kumhudumia. Hii nchi hii kuna vitu watu wanaviweka hadi unajiuliza aliyeviweka ana akili timamu kweli!
 
Back
Top Bottom