KERO Changamoto zinazoendelea kwenye hospitali ya Wilaya ya Ubungo, zinazohitaji kuchunguzwa na kutatuliwa

KERO Changamoto zinazoendelea kwenye hospitali ya Wilaya ya Ubungo, zinazohitaji kuchunguzwa na kutatuliwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

maestro26

New Member
Joined
Dec 11, 2024
Posts
1
Reaction score
1
Kuna changamoto kadhaa zinazoendelea katika hospitali hii ambazo zinahitaji kufanyiwa uchunguzi na kuchukuliwa hatua:

1. Ucheleweshaji wa malipo ya wafanyakazi
Wafanyakazi hawajalipwa malipo ya muda wa ziada (overtime) tangu mwezi Novemba hadi sasa. Wanapouliza uongozi, wamekuwa wakielezwa kuwa kuna changamoto za kifedha, huku baadhi ya shughuli nyingine zikiendelea. Pia kuna malalamiko ya kutolipwa mishahara kwa walinzi na wahudumu wa kujitolea (volunteers).

2. Usimamizi wa fedha za wanafunzi wa mafunzo kwa vitendo (field)
Kuna madai kuwa fedha zinazolipwa na wanafunzi wa field hukusanywa kwa njia ya mkono na baadhi ya watendaji wa hospitali badala ya kulipiwa kupitia mfumo rasmi wa serikali wenye namba ya malipo (control number).

3. Malipo kwa wajawazito wanaopata huduma
Kuna malalamiko kuhusu kulazimishwa kwa baadhi ya wajawazito kulipia huduma, ambapo wanaojifungua kawaida hudaiwa Sh70,000 na wanaofanyiwa upasuaji (operation) Sh250,000. Wanapouliza, huambiwa kuwa wanaweza kupewa rufaa kwenda hospitali nyingine kama hawakubaliani.

4. Uwepo wa wahudumu wasio na sifa rasmi
Kuna madai ya kuwepo kwa baadhi ya volunteers wanaofanya kazi bila leseni, pamoja na tuhuma za upendeleo wa kindugu katika baadhi ya idara kama famasi na uuguzi.

5. Malalamiko ya unyanyasaji na upendeleo kazini
Baadhi ya wafanyakazi wa kujitolea na wauguzi wanadai kunyanyaswa na baadhi ya viongozi wa hospitali, akiwemo matron, katibu na mratibu wa kliniki. Pia kuna madai ya upendeleo katika utoaji wa nafasi na tuhuma za baadhi ya viongozi kuwapa vyeo watu wanaowapendelea kwa maslahi binafsi.

6. Upungufu wa dawa hospitalini
Kuna malalamiko ya ukosefu wa dawa mara kwa mara, hali inayodaiwa kusababisha wagonjwa kuelekezwa kununua dawa katika famasi za nje. Inadaiwa kuwa changamoto hii inatokana na usimamizi usioridhisha wa huduma za famasi na mahusiano yasiyo rasmi na baadhi ya famasi binafsi.

Tunaomba mamlaka husika zifanye uchunguzi wa kina kuhusu tuhuma hizi ili kuhakikisha uwajibikaji, uadilifu na utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.
 
Naomba kujua location ya hii Hospital
 
Back
Top Bottom