Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Katika Taifa hili naamini kabisa kuna watu bora ambao wanauwezo wa kubadili mwelekeo wa Taifa hili kama wakipewa nafasi.
Wanaoamini katika Taifa hili na uwezo wake wa kufika mbali ikiwa jitihada mahsusi zitawekwa ili watu wa Taifa hili watoke hapa tulipo. Katika maisha yangu yote nimeendelea kuamini toka nilipopata akili zangu katika uwezo wa Taifa hili kukua na kutoka hapa tulipo. Kwanini tusifanikiwe kama tukiamua kwa dhati kuleta mageuzi katika nchi yetu? Mabadiliko yanawezekana ni maamuzi yetu tu ya dhati.
Kama Taifa kamwe hatutakuwa na furaha kama hatutawekeza juhudi zetu kuleta mageuzi katika Taifa hili.
Tutakuwa na furaha kama tukiwa na mipango ya pamoja kisha kuwekeza fikra na nguvu zetu kufanikisha mipango hiyo. Taifa hili ni Taifa la watu wasiokuwa na furaha kwasababu kama Taifa hatujafanikiwa kitu chochote kikubwa cha kujivunia. Ni muhimu kuwekeza juhudi zetu ili kuandika historia katika dunia. Na hili hatutafanikiwa kama hatutakuwa wamoja kama Taifa. Ni muhimu kutambua hili, tuna kitu cha kukijenga kama watu tunaoishi pamoja. Kitu hicho ni nchi yetu. Tukiijenga nchi yetu vizuri tutajivunia. Lakini hatutaweza kuijenga vyema nchi hii pasipo kwanza kujenga mahusiano yetu.
Kama tutapendana sisi wenyewe kwa wenyewe tutakuwa na nafasi kubwa ya kulijenga Taifa hili. Ni lazima tulipende Taifa hili ama sivyo hatutakuwa na nguvu ya kulijenga. Kwahiyo lazima tuelewe hapa ni sehemu pekee ambako tunaweza kupaita nyumbani. Kwahiyo ni lazima juhudi mahsusi zifanyike kuwaleta watu pamoja ili tulijenge Taifa hili kwa pamoja.
Najua kuna matatizo ya corrupt leaders ambao ndio chanzo cha mgawanyiko uliopo. Lazima tuwaambie ukweli. Kwamba wana haribu mwelekeo wa Taifa hili na future yake. Lazima waelewe wao wamekuwa viongozi kwa lengo moja tu, kuleta umoja wa watu wa Taifa hili na kulitoa Taifa hili kutoka hapa lilipo. Lazima wajue cheo ni dhamana na wana majukumu ya dhati ya kulijenga hili Taifa na sio kinyume chake. Roho ya uzalendo ya watu wetu imepotea sababu yao. Ni lazima wajue historia itawahukumu. Watazania wana kiu ya kusonga mbele kama Taifa na hili halitowezekana kama tusipokuwa wamoja. Taifa limekosa uongozi wenye maono na hili ni Tatizo kubwa sana ambalo naliona. Naona msambaratiko katika familia, katika dini na katika ukabila. Hivi vitu vyote vinahitaji kuunganishwa na kuwa kitu kimoja. Ili tujenge Taifa imara. Wajibu wa mtu kwa familia yake, kwa jamii yake na kwa Taifa lake. Sisi sote tuko pamoja katika ujenzi wa Taifa hili. Kama ni nyumba tunatakiwa tuinyanyue pamoja na kuiezeka pamoja.
Tukifikiria au tukiwa na fikra ya kwamba uongozi ni sehemu ya kupatia mali au kutajirikia tutakuwa hatulipendi Taifa hili na baadae yetu itakuwa matatani. Muono huo ambao uko akilini mwa viongozi wengi ni hatari kwa uhuru na mustakabali wa watu wa Tanzania. Uongozi sio sehemu ya kutafutia ufahari au sifa. Uongozi ni kitu kingine kabisa na unahitaji mtu mwenye maono na mwenye busara kwakuwa unahusiana na uhuru na maisha ya watu, una husiana na haki za watu. Ukiwa na Taifa la viongozi wa namna hiyo nchi haitokalika na haki haito tamalaki. Taifa huunganishwa kwa haki. Order na harmony katika Taifa italetwa na haki tu.
Tutakuwa na Taifa lenye watu ambao watakuwa wanagombania kama fisi Mali ya Taifa, tutakuwa na vurugu na fujo na maskini hawatopata chochote, tukiwa na viongozi walifuata mali katika siasa haki itatendekaje? Tunahitaji kiongozi atakaye tufikisha salama katika safari yetu. Kiongozi huyo sio mwingine bali ni mwenye busara na maono.
Msidhani DRC imelaaniwa na Tanzania itaendelee kubarikiwa ikiwa Viongozi wetu wataendelea kuabudu mali. Hatua ya kwanza ya serikali yeyote kuwa ya kiimla ni pale inapoanza kuwa ya kifisadi na yenye tamaa ya mali. Ni lazima itagandamiza watu wake. Kubadilisha mawazo kutoka kutumikia watu kuja kujilimbikizia mali ni hatua ya kwanza ya ugandamizaji dhidi ya raia. Wananchi wana haki ya kulinda uhuru wao dhidi ya serikali yeyote ya kidhalimu ambayo haizingatii maslahi ya umma. Kwahiyo kundi dogo litahodhi utajiri na kujikusanyia mamlaka na kudhani ya kwamba wana haki ya kutawala wengine, uongozi utakuwa wa kuridhishana. Kutakuwa na maskini wengi mno na matajiri wachache.
Watanzania ni lazima wafikirie upya uhuru wao ambao kwasasa unaonekana uko mashakani au umewekwa reheni na kikundi kidogo cha watu kilicho hodhi utajiri mkubwa usio halali, kundi hilo ni la viongozi. Watanzania wana haki juu ya bunge, mahakama na serikali. Ambavyo vyote vinaonekana viko corrupt. Na imani ya wananchi juu ya vyombo hivyo ni ndogo. Raia wowote wale popote pale duniani wana haki ya kuiondoa serikali yeyote iie isiyo kidhi matarajio yao na matumaini yao ya kujenga jamii huru na yenye matumaini. Watu wa Taifa hili wana hamu ya maendeleo lakini wanazuiwa na rushwa na viongozi waliokosa dira na will power ya kulinyanyua Taifa hili kutoka hapa lilipo.
Nchi hii kamwe haitojengwa kwa propaganda na uongo bali itajengwa kwa haki na ukweli. Nchi hii haitojengwa kwa porojo bali kwa juhudi za dhati za watu wake kujiletea maendeleo yao wenyewe. Ni ukweli usiopingika kuna upuuzi mwingi unaendelea katika Taifa hili ambao hauvumliki kwa mtu ambaye ana hamu ya kuliona Taifa hili likinyanyuka. Vijana wa Taifa hili wanahitaji kuona Taifa hili likiendelea. Hatutuwezi kuendelea na viongozi waliopo. Lazima uje wito mpya katika Taifa hili wa uongozi na uadilifu. Vijana wa Taifa hili lazima wajengwe upya kulipenda Taifa lao ni wao tu wenye uwezo wa kulinyanyua Taifa hili kutoka hapa lilipo. Vijana wa Taifa hili wanahitaji heshima kwa Taifa lao. Hatuwezi kuendelea kujenga Taifa hili kwa porojo. Lazima tulijenge Taifa hili kwa akili na ukweli. Raia wana haki ya kuambiwa ukweli kuhusu nchi yao.
Ni lazima tujenge msingi mpya wa Taifa hili na tusonge mbele. Hatutaweza kama hatutakuwa wamoja katika akili na roho. Hatutaweza kama hatutajenga uaminifu na kuheshimiana miongoni mwetu.
Kila wakati nimekuwa nikiamini hatua ya kwanza kwa Taifa lolote kupiga hatua ki maendeleo ni kwa raia wao kulipenda Taifa lao. Ni lazima tulipende Taifa letu. Ni lazima tuzalishe watu wetu bora ambao watetembea kifua mbele duniani kote. Hili lazima litokee na hii ndio itakuwa furaha yetu. Sisi kama Taifa ni lazima tukue. Kuna chaguzi mbili tu. Tukubali na kutia juhudi kufanikisha ndoto yetu ya kwamba tuna uwezo wa kuwa Taifa kubwa kama tukijipanga na kutia juhudi au tusiamini na tubaki hapa tulipo kwenye udhaifu wetu? ''This need bold decision and courage'' but we must move forward like trained Army. We must move forward. We have the power to move this Nation forward. Hatuwezi kuendelea kuwa watu wanaotafuta kwenda kupata mali kwenye uongozi. Tunahitaji viongozi watakao lisongesha Taifa hili. Those who will uplift the spirit of the ''Nation''. We must have our core '' beliefs'' . Tuna viongozi ambao they lead us no where. Watu wa taifa hili wanahitaji muongozo na dira. Wanahitaji jua la asubuhi liwamulikie na matumaini yawajae mioyoni mwao. Tumaini ambalo litajenga Taifa hili. Tunahiaji viongozi wanaoamini kwamba Taifa hili lazima lisonge mbali kwa damu na kwa jasho. Tukiwa wamoja nothing shall be impossible to us. Tunahitaji kongozi atakayeanzisha movement hii. Kiongozi mkweli na mzalendo.
We must build spirit of love and admiration toward this country. Our children must love this NATION. We have ability to grow and to become greater kuna msemo ambao tunauzungumza sana; ''Hata mbuyu ulianza kama mchicha'' . There is the truth on this. Kama tukiamua leo kwa dhati kabisa za nafsi zetu kulijenga Taifa hili nani atatuzuia kuwa Taifa kubwa? Ni juhudi zetu tu na umoja wetu na uaminifu katika kulijenga TAIFA hili. Taifa lolote litakuwa huru pale litakapo jitambua na watu wake watakapojitambua, ni lazima tujitambue sasa.
Those who are educated must initiate change and growth.
Ni lazima tujenge watoto wetu katika utaifa na katika uzalendo. Ni lazima waamini katika Utanzania.'Tutakapo badilisha mawazo ya watu kutoka katika ubinafsi kuja kwenye utaifa ni hatua ya kwanza ya maendeleo.
We need honest leaders who speaks from their hearts, who are ready to sacrifice everything for the Nation growth.We need a leader who will move our cause forward. We must set a Nation dream and handover that dream in each generation. I want you to believe this; our country can grow and become a great Nation on the earth. If we want to move this country forward we must forget ourselves and focus on building this country.
CHANGE IS POSSIBLE.