Changia elimu kuwasaidia wengine

Changia elimu kuwasaidia wengine

TYPIN ERRAH

Member
Joined
Mar 9, 2013
Posts
41
Reaction score
23
Habar wakuu humu ndani...

Mimi ni mdau wa elimu katika shule ya sekondari kwemdimu iliyopo wilaya ya Korogwe. Tuna shida ya vitabu upande wa somo la elimu ya dini ya kiislamu kwani tuna idadi ya wanafunzi zaidi ya mia tatu lakini tuna vitabu vinne tu kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato cha nne.

Hivyo somo tunahitaji msaada wa hiari kwa anaeweza kuhisi kutusaidia maana imekuwa changamoto kwetu kwa idadi ya wanafunzi.

Somo hili kwa sasa upande wa vitabu bado serikali haijatia nguvu ingawa inlitambua somo hili kufundishwa mashuleni...

Uhitaji wetu sisi no vitabu na wala sio pesa, kwa yule atakaehitaji kutusaidia basi tuko tayari kushirikiana nae kumuelekeza vitabu vinapatikana wapi, kama anajua vinapatikana wapi basi ni bora ila kwa ufupi kila kitabu kimoja kinauzwa TSH. 9000/= KARIBUNI
 
Back
Top Bottom