Changia mawazo hapa. Pia jifunze toka kwa mawazo ya wengine

Kig

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2012
Posts
1,076
Reaction score
458
Napenda sana kununua gari inaitwa SUZUKI KEI yenye CC650 hadi CC660 (Angalia picha hapo chini). Lakini naamini kila aina ya Gari ina uzuri na matatizo yake hasa kwa mazingira ya Bongo. Pia huwa naamini kabla ya kufanya jambo lolote ni vizuri kupata ushauri toka kwa watu wenye uzoefu na utalaamu kwenye jambo husika. Kwa hiyo Tafadhalini wenye uzoefu na hizi gari SUZUKI KEI mnipe mwangaza juu ya uzuri na matatizo yake ili niisingie kichwakichwa halafu nikaishia kujuta. Natanguliza shukrani kwa michango yenu. Asanteni
 
Attachments

  • IMAG0648.jpg
    IMAG0648.jpg
    294.8 KB · Views: 66
  • IMAG0649.jpg
    IMAG0649.jpg
    433.4 KB · Views: 73
  • IMAG0650.jpg
    IMAG0650.jpg
    362.8 KB · Views: 53
  • IMAG0651.jpg
    IMAG0651.jpg
    368.4 KB · Views: 55
Safi sana Mkubwa!
Hakika humu jamvini kuna kila aina ya member!
Hebu tuwasubirie wadau waje!
 
Hizi gari nzuri sana. hazili mafuta, kabisa maana cc ndogo. Kama vipi nunua tu mkuu.

umeongelea utumiaji wa mafuta tu,vipi upatikanaji wa vipuli,na mambo mengine muhimu!!dadavua kiongozi watu tule shule!
 
mi sina uzoefu nalo ila nakushauri angalie uimara wake kulingana na mazingira uliyopo na shuhuli unazofanya.
Pia jaribu kuzunguka ktk maduka ya spea ktk maeneo uliyopo ulizia kama vifaa vyake vinapatikana na bei zake.
Wengine watachangia zaidi.
 
angalia mwaka lilotengenezwa,spare parts kama zinapatikana,utalitumia kwa sshughuli gani?kama its for the family ,je itakutosha wewe na familia?,,barabara unazotumia mara kwa mara,je gari hilo litastahimili?,,pia nakushauri utafute mtu mwenye gari kama hilo,atakuwa na ujuzi zaidi na uzoefu kuhusu hilo gari....nakutakia kila la kheri
 
Gari ambazo wenzako wameshazichoka Japani, wewe nunuwa tu likikutesa utajuwa kwanini wao walilipeleka mnadani.
 
zomba unanchekesha! Bongo magari yanayopita barabarani 98% ni mtumba, 2% ni ya mafisadi na majini (v8) ya sirikali yako tukufu!

Kijana, ingia google, angalia users' reviews, comments juu ya hiyo gari yako tarajiwa. Utapata majibu yote kutoka watumiaji dunia nzima. Hongera kwa kutaka kujikwamua.
 
Last edited by a moderator:

Siku tukiacha kununuwa mitumba ndio siku Tanzania itakapo anza kuendelea. Nakuhakikishia anza leo kuacha kununuwa mitumba, uwe wa nguo uwe wa gari, utaona unavyopiga hatua za kimaendeleo.

Think big to become big. Mitumba inatudumaza.
 
Very Low!
Industrial revolution ndo mwanzo wa kuendelea, sio kununua brand new car, shirt, underpant, tie, fishing gears etc from europe.
 
Na hiyo industry itakutengenezea mitumba? Think!
 
Economic growth haiji kwa ability to purchase but ability to produce. . . . Unless maendeleo unayoyaongelea wewe ni maendeleo ya kuongezeka kwa foleni kwasababu ya magari mengi.
The indicator that has been used by your darling several times,
 
Ungeelewa hayo usingepinga kauli yangu ya kuachana na mitumba. Ni lini utaanza kutengeneza wakati akili yako iko kwenye mtumba? wale wanakuuzia mitumba ili wapate kutengeza vipya kwenye viwanda vyao. Hivi mbona uko finyu sana, umesoma shule ipi? St. Nyerere?
 
Gari ambazo wenzako wameshazichoka Japani, wewe nunuwa tu likikutesa utajuwa kwanini wao walilipeleka mnadani.

acha ujinga wewe ... too much ... nani hajui kwamba hayo magari yameshatumika

Je zile meli mbili zilizoua wanzibari mfululizo mv. Islender na hii ya juzi zilinunuliwa mpya au mitumba ?
 
Ndio muache kununuwa mitumba, mjifunze kujivunia vipya ikiwa mnataka kubadilika. Mifano mizuri umeiweka mwenyewe ya hizo meli, zinawaua, nyie bado tu.
 
Gari ambazo wenzako wameshazichoka Japani, wewe nunuwa tu likikutesa utajuwa kwanini wao walilipeleka mnadani.

Mbona una dharau sana mkuu. Mbona unajivuna sana na utajiri/uwezo wako wa kununua magari mapya? Kama huna hoja ya kuchangia mawazo kaa pembeni ili wenye nia njema na maada hii wachangie mawazo
 
Badilika, sio dharau. Ishi bila kuteseka, kwanini ukanunuwe mtumba wa wajapani? au nguo alishovaa mzungu, zinanuka jasho? Halafu huyo huyo kesho utaandika kuwa mzungu mbaya huku shati ulilovaa limetumiwa na yeye na ndio unatamba nalo.

Kuwa mzalendo. Bora ununuwe pikipiki mpya kuliko mtumba wa gari. Au ukashoneshe gwanda la khaki jipya kuliko kwenda manzese kununuwa gwanda la aliyekufa ulaya.

Zamani mitumba tulikuwa tunaita "Kafa Ulaya".

Halafu tunataka maendeleo!
 
Halafu tunataka maendeleo![/QUOTE

Tatizo unafikiri kila gari used toka Japan ina kasoro/matatizo. Kwa maana hiyo kila gari mpya hakina kasoro. Ungejua hata gari mpya zina kasoro nyingi tu ndio maana kuna usemi " KIPYA KINYEMI INGAWA KIDONDA". Unaposema niwe mzalendo una maana gani? Dhibitisha kama Kununua gari jipya ni uzalendo? Hata hivyo nimekusoma hapa mwishoni naona unafanya promotion ya pikipiki (yaani jeneza la wabongo). Sijui una duka la kuuza pikipiki mpya. Mimi sipendi pikipiki.
 
Back
Top Bottom