Kig
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 1,076
- 458
Napenda sana kununua gari inaitwa SUZUKI KEI yenye CC650 hadi CC660 (Angalia picha hapo chini). Lakini naamini kila aina ya Gari ina uzuri na matatizo yake hasa kwa mazingira ya Bongo. Pia huwa naamini kabla ya kufanya jambo lolote ni vizuri kupata ushauri toka kwa watu wenye uzoefu na utalaamu kwenye jambo husika. Kwa hiyo Tafadhalini wenye uzoefu na hizi gari SUZUKI KEI mnipe mwangaza juu ya uzuri na matatizo yake ili niisingie kichwakichwa halafu nikaishia kujuta. Natanguliza shukrani kwa michango yenu. Asanteni