Changia Yanga ni aibu kubwa sana

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,117
Reaction score
1,966
Sasa hivi kuna kuna namba inatembea kwenye vyombo vya habari kuwa wanaomba kuchangiwa

Haya ni maajabu mengine kwa club Kongwe kutembeza bakuli la omba omba

Hivi club Kongwe Afrika mashariki na kati kwa miaka zaidi ya 80 hawana chochote wanachokifanya ili kuwaingizia kipato?

Yanga,Yanga,Yanga ni aibu kubwa sana

Omba omba Fc a.k.a Vyura Fc aibu tupu mitaani ,si bora vilabu vichanga vilivyopanda daraja wangeomba kuchangiwa lakini siyo Yanga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashara imepanda daraja msimu huu lakini haitembezi bakuli...
Yanga imezidiwa hata na mbao fc kweli?
Yanga ina wanachama wengi na watu wakubwa tu huko serikalini, hao hawaijui hali ya timu?!
Pengine hii isije ikawa ni mradi au mazingira ya utakatishaji wa fedha yanaandaliwa...
 
Inabidi waundiwe tume ya uchunguzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikikumbuka matusi yao na mbwembwe na zaidi kuingiza watu bure uwanjani nafikiria sijui wale viongozi walikiwa wanafikiria kwa kutumia kiungo gani
Hamjielewi nyie,sisi wapenzi wa Yanga tunachanga mbona nyie mnalambwa midole na kanjibahai .kesho natume dola 5,000 za kimarekani.Tunataka ushindi tuu,umemuona Feisal? Makamboo jee?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oya usiwafananishe biashara na yanga hebu tutake radhi watu Wa Mara tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe kama waona aibu kuchangia pita mbali, acha wenye mapenzi ya kweli kwa timu yao wachange. Si unaona sasa timu inabadilika kila uchao, hadi wale wa upande wa pili wanaanza kuweweseka. Wenye moyo safi na timu yao tafadhari changia bila kuchoka, kitaeleweka tu, na watakoma mwaka huu.
 
Hiki kitendo kinanikera kweli, wangetafuta vyanzo vingine vya mapato kuliko kuombaomba. Huu ndo wakati wa kupima uwezo wa viongozi. Yanga ni brand kubwa kwanini wasitengeneze hata bidhaa zenye nembo ya yanga wakauza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasubiri Mo awatose kama kawaida yake. Hawezi kumaliza mwaka. Mbagala Market sasa ni African Lyon, Singida United. Ni zamu ya Simba sasa.
Fedha zenyewe mashamba yetu ya mikonge kaweka dhamana ma bank ya nje ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…