#COVID19 Chanjo ya Corona Dar es Salaam na muitikio mdogo

wekeni picha na sio kuleta blah blah
 
Hakuna aliloanzisha likaffaulu..kuanzia wamachunga hadi usafi...now chanjo
 
hii hali ikiendelea na huu mkanganyiko watuchanje tusichanje basi wananchi hawatajitokeza kabisa kuchanja.

Mkuu wa mkoa kafeli mno katika kuhamasisha wanadsm wajitokeze ilitakiwa leo ndio iwe slama kwa taifa kua dsm watu wamejitokeza wengi
Nchi imekosa uongozi madhubuti hii. Ukishakuwa na rais ambaye hana vision usitegee matokeo chanya. Rais alikosea sana kuendelea na wale wale walioboronga mwanzoni.
 
Hatutaweza kuwa na akili za
matibabu kama nchi haina university Teaching hospital,.
 
Mkuu we si umeshachanja?Hiari yako uliyotumia na wengine nao wanaitumia.

Tusilazimishane Wala kuhamasishana....suala la afya na uhai Ni jukumu ya kila mtu na utashi wake
 
Tozo za Simu, mara kodi ya jengo. Unaanzaje kupata utulivu wa Akili kwenda kuchanja.
Bora kwenda kutafuta pesa Au kwenda kwenye Ibada kuliko kwenda kuchanja.
Chanjo zenyewe ziaharibike tu.
Kabisa na ziharibike tu
 
Matangazo Kwa kweli yalikuwa kidogo sana media nyingi hazikutangaza kabisa ndio maana mwitiko umekuwa hafifu
 
Kwakweli kwa ile clip niliyoiona Leo molel akiongea wakati wa magufuli kuwa chanjo ni mbaya ikiingia kwenye mwili wa mwanadamu!
Sina hamu,ndo maana Gwajima amewalipua
 
Ndugu yangu nakushauri kama upo above 40yrs old nenda kachanje hata kama upo strong kiasi gani nenda kachanje huu Ugonjwa hauwezi kwesha leo wala kesho.
Wazazi wangu washastaafu Dr na nurse,na wana hospital yao kwa sasa mkoani huko!mama alishaumwa last yr na alipona tunamshukuru Mungu! lakini wametuambia tusichanje na wao hawachanji! Na sbb za kitaalamu nimepewa,sa Dorothy aniambie nichanje?bila sbb za kujitosheleza, [emoji16]masihara.
#mi na familia yangu pamoja na huo umri tulionao hatuchanji na tuko salama,Mungu aliyetuvusha awamu ya 1,ya 2 ndo atatuvusha na awamu hii!

So kigezo cha umri bado sio ishu kabisa!
 
Unaweza ukakuta hata wanao wachanja wenzao hawataki kuchanja.
 
Umekwenda uwanjani leo?
Radio One taarifa ya habari ya saa mbili wanasema mwitikio ulikuwa mkubwa. Wewe unasema mdogo. Kipi ni kipi?
 
Umekwenda uwanjani leo?
Radio One taarifa ya habari ya saa mbili wanasema mwitikio ulikuwa mkubwa. Wewe unasema mdogo. Kipi ni kipi?
Ulitegemea waseme muitikio ulikuwa mdogo?
Ni kweli muitikio ulikuwa mdogo sana, Sasa imebidi waongeze na siku ya kesho.
Wakati sababu ya kuweka leo ilikuwa kutokana na watu kukosa muda siku za kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…