SoC01 Chanjo ya COVID-19: Yote unayohitaji kufahamu

SoC01 Chanjo ya COVID-19: Yote unayohitaji kufahamu

Stories of Change - 2021 Competition
Status
Not open for further replies.

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Kampuni ya Kitabibu ya Moderna imetangaza nia yake ya kuomba kibali cha kuthibitishwa kwa chanjo yake ya COVID-19 kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Marekani.

Moderna sasa inaungana na kampuni nyingine mbili za kitabibu zinazosubiri kuthibitishwa kwa chanjo zao na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini humo: Kampuni za Pfizer na BioNTech ambazo zimeomba vibali vya dharura vya kuthibitishwa kwa chanjo zao mapema mwezi huu.

1608098667399.png

Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Marekani imesema kuwa inafikiria kufanya maamuzi ya kuthibitisha chanjo ya kampuni ya Pfizer ndani ya muda wa majuma machache yajayo, ikisubiri kikao kinachotarajiwa kufanyika Desemba 10.

Moja kati ya kampuni hizo ikithibitishwa kutoa chanjo ya virusi vya corona, itatakiwa kutengeneza chanjo zaidi ya milioni 40 kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba. Kampuni kubwa zilizo katika mbio za kutengeneza chanjo ya corona ni pamoja na Pfizer-BioNTech, Moderna, AstraZeneca, Novavax na Johnson & Johnson.

Lakini kuna tofauti gani kati ya chanjo zinazotolewa na kampuni hizo?

Mfumo wa utengenezaji wa chanjo ya virusi vya corona unafanana kwa karibu chanjo zote zilizopatikana mpaka sasa: chanjo za AstraZeneca, Novavax, CSL, Pfizer-BioNTech, nk.

Chanjo hizi hufanya kazi kwa kutumia vinasaba vya protini ambayo, baada ya kuingizwa mwilini, hutengeneza protini inayofanana na virusi vya corona, hivyo kuulazimisha mwili kutengeneza kinga ukijua kuwa protini iliyotokana na chanjo si salama kwa mwili. Hii husaidia mwili kuwa na kinga pale virusi vya corona vinapoingia mwilini kutokana na kinga ya awali iliyotengenezwa baada ya vinasaba vya protini kuingizwa.

Nchi/kampuni zilizotengeneza chanjo ya virusi vya corona

China ni nchi ya kwanza duniani kutengeneza chanjo ya virusi hivyo, chanjo ambayo ilianza kufanyiwa majaribio mwezi Aprili, lakini haikuwekwa katika programu ya kuzalishwa kwa ajili ya matumizi ya umma. Nchi hiyo ilitengeneza, kwa mara ya kwanza, chanjo ya virusi hivyo mapema mwezi Aprili, kwa ushirikiano kati ya maabara ya kijeshi pamoja na taasisi ya utafiti wa kibaiologia ya CanSino.

Tangu kutengenezwa kwa chanjo hiyo, China imeendelea kuboresha na kutengeneza chanjo nyingine za virusi vya corona huku ikidai kuwa na mafanikio mazuri kwa zaidi ya watu 700 waliofanyiwa majaribio.

Kampuni ya Dawa ya Johnson & Johnson ni moja kati ya kampuni za mwanzo kabisa nchini Marekani kujitosa katika mbio za kutengeneza chanjo ya COVID-19. Kampuni hiyo ilisema kuwa kufikia mwaka 2021, itakuwa imeshatengeneza chanjo milioni 600 hadi 800 za corona, ikitegemea kuanza majaribio yake mwezi Septemba mwaka huu. Baadaye, kampuni hiyo ilisogeza muda wa kuanza kutoa chanjo hiyo na kusema kuwa itaanza kutoa chanjo yake ya Ad26.COV2-S katikati ya mwezi Julai mwaka 2021, ikisema kuwa majaribio ya awali ya chanjo hiyo hayakuonesha madhara yoyote kwa wagonjwa.

Mapema mwezi Agosti, Rais wa Urusi, Vladimir Putin alitangaza kuwa nchi yake imekuwa ya kwanza duniani kugundua na kuthibitisha chanjo ya virusi vya corona. Rais Putin alitangaza mafanikio hayo ya Urusi kupitia televisheni ya taifa akisema kuwa kuwa chanjo hiyo inafanya kazi vizuri, licha ya mataifa mbalimbali duniani kuonesha wasiwasi wao kuhusu usalama wa chanjo hiyo, akiongeza kuwa mmoja kati ya binti zake wamepatiwa chanjo hiyo. Chanjo hiyo ya Urusi haijaanza kutumika kwa matumizi ya umma, licha ya kudaiwa kuwa na uthabiti wa asilimia 92 baada ya kufanyiwa majaribio kwa watu 16,000 waliojitolea. Chanjo hiyo inatumika kwa matumizi ya dharura tu nchini Urusi.

Chanjo inayotengenezwa na kampuni za Ujerumani na Marekani za Pfizer na BioNTech imeripotiwa kuwa na uthabiti wa zaidi ya asilimia 90, takwimu zinazotokana na majaribio yaliyofanywa kwa zaidi ya watu 43,000 katika nchi sita tofauti duniani, ikiwamo Afrika Kusini. Katika taarifa iliyotolewa Novemba 9, kampuni hizo zinasema kuwa watakuwa na uwezo wa kutoa dozi milioni 50 kufikia mwisho wa mwaka huu, na dozi bilioni 1.3 kufikia mwisho wa mwaka 2021, huku mtu mmoja akitakiwa kupata dozi mbili ili kuwa na kinga kamili dhidi ya virusi vya corona.

Wiki moja baada ya kampuni za Pfizer na BioNtech kutangaza mafanikio ya zaidi ya asilimia 90 ya chanjo ya Corona, kampuni nyingine ya kitabibu nchini Marekani, Moderna, ikatangaza kuwa chanjo yake dhidi ya virusi vya corona ina uthabiti wa asilimia 94.5.

Wakati chanjo zote mbili, chanjo ya Pfizer na Moderna, zilionekana kuwa na hali zinazofanana za kiusalama, chanjo ya Moderna imeonekana kuwa na unafuu kutokana na uwezo wake wa kustahimili kuhifadhiwa katika eneo lenye baridi kidogo ikilinganishwa na chanjo ya Pfizer. Chanjo ya Pfizer inahitaji jotoridi la nyuzi 75 chini ya sifuri wakati chanjo ya Moderna ikihitaji kuhifadhiwa katika jotoridi la nyuzi 20 chini ya sifuri, jambo linalorahisisha uhifadhi katika majokofu ya kawaida yanayopatikana kwa urahisi. Chanjo ya Moderna pia inaweza kuhifadhiwa kwa siku 30 tofauti na chanjo ya Pfizer ambayo inaweza kuhifadhiwa kwa siku 5 pekee.

Kwa sasa chanjo zote hazijaanza kutolewa kwa matumizi ya umma. Upo uwezekano mkubwa kwa kampuni nyingi kujitokeza kutengeneza chanjo zaidi za kupambana na virusi vya corona. Licha ya kusubiriwa kwa matumaini katika mataifa mengi duniani yaliyoathiriwa na virusi vya corona, mapokezi ya chanjo hizi katika baadhi ya nchi kama vile Brazil si mazuri, jambo linaloweza kukwamisha juhudi za kupambana na virusi vya corona.

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuwa kwa sasa haiwezi kuthibitisha upatikanaji wala usalama wa chanjo yoyote ya virusi vya corona iliyopatikana kwa kuwa chanjo hizo bado zipo katika hatua za majaribio.
 

Attachments

  • covid-vaccine2.jpg
    covid-vaccine2.jpg
    88.9 KB · Views: 8
Upvote 0
Ni asilimia 51 tu ya Wamarekani ambao wako tayari kupata chanjo hiyo na 49% wakiwemo madaktari na manesi wengi wakihofia kupata chanjo hiyo kwa kuwa side effects zake za muda mrefu hazijulikani. Wengi wanataka Makampuni husika yaweke data zaidi hadharani. Pia haijulikani chanjo hizo zitakuwa effective kwa muda gani kama kinga ya COVID19.
 
Ni asilimia 51 tu ya Wamarekani ambao wako tayari kupata chanjo hiyo na 49% wakiwemo madaktari na manesi wengi wakihofia kupata chanjo hiyo kwa kuwa side effects zake za muda mrefu hazijulikani. Wengi wanataka Makampuni husika yaweke data zaidi hadharani. Pia haijulikani chanjo hizo zitakuwa effective kwa muda gani kama kinga ya COVID19.
?[emoji848]
 
Kuna jamaa mmoja bila aibu anasema chanjo inakwenda ku- rewrite human DNA - kwamba eti baada ya kizazi kadhaa binadamu anaweza kuzaa kitu cha ajabu ajabu..

Unajua kama hujafanya utafiti na wewe ni mvivu wa kusoma basi ni vizuri ukabakia kimya, hii ni pure Science brother ina prove..haya si mahubiri ya kuibia watu sadaka!!

Chanjo na zije tu - wananchi tupo tayari!!
 
Kuna jamaa mmoja bila aibu anasema chanjo inakwenda ku- rewrite human DNA - kwamba eti baada ya kizazi kadhaa binadamu anaweza kuzaa kitu cha ajabu ajabu..

Unajua kama hujafanya utafiti na wewe ni mvivu wa kusoma basi ni vizuri ukabakia kimya, hii ni pure Science brother ina prove..haya si mahubiri ya kuibia watu sadaka!!

Chanjo na zije tu - wananchi tupo tayari!!
Isijekuwa ni yule mheshimiwa mbunge mchungaji anayefufua wafu wasiofufuka! Unafanya tupige ramli Mkuu...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom