kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Ubora wa chanjo unaendana na kufuatilia taratibu za uhifadhi. Kama chanjo imeelekezwa kutumika kwa kipindi flani lazima iwe hivyo, Kama imeelekezwa kutunzwa kwenye joto la ngazi flan lazima iwe hivyo na Kama imeelekezwa kuwekwa kwenye ubaridi pia inabidi iwe hivyo.
Kampeni inayoendeshwa Mikoani imetia doa ubora wa chanjo kwa sababu tatu kuu;
1. Kampeni imejikita katika mashindano ya Mikoa na Wilaya bila kujali ubora na ufuatiliaji wa taratibu husika za chanjo
2. Kampeni imeondoka kwenye lengo la msingi la hiari imeanza kutangazwa Kama lazima na wataalamu wa afya wameelekezwa na wanasiasa kuondoka ofisini nakwenda kuchanja Kijiji kwa Kijiji au mtu kwa mtu. Tukumbuke umbali, ukosefu wa vifaa vyakuhifadhi dawa na umuhimu wa kujua afya ya unayemchanja
3. Serikali imekiri kupitia mkuu wa mkoa wa Pwani kwamba upo uwezekano dawa ikaexpire kabla ya kuisha....tukumbuke hizi ni dozi milioni moja labda Kama zimeongezeka. Kama zinakaribia kuisha upo uwezekano Wataalamu wa afya wakawajibishwa na wanasiasa kwa kupelekea dawa kuaribika hivyo lazima mbinu mbadala zitumike wataalam walinde vibarua vyao. Ikumbukwe hakuna uwezeshwaji wa kutosha kwao.
4. Wataalamu hawana nguvu yakupingana na siasa, hivyo hata pale masharti ya uhifadhi yanapokiukwa upo uwezekano wa wataalamu kukiuka viapo vyao kwa kuogopa wanasiasa. Na hapa inaweza kutikia hatua wakachoma chanjo kinyume Cha masharti yaliyowekwa.
Nini KIFANYIKE: Usalama wa chanjo, uwezeshwaji wa watendaji na utengenezaji wa miundombinu ya itoaji chanjo uzingatiwe