Chanjo ya Malaria ipo njiani; je, utakubali kuchoma chanjo hiyo?

Chanjo ya Malaria ipo njiani; je, utakubali kuchoma chanjo hiyo?

Wenzetu wanahangaika kupata tiba za kila maradhi ila sisi kwanza lazima tubishe ndio tukubali baadae kama sio wale

Ni kawaida yetu kupinga na kuhoji sana ingawa ukiuliza chanjo wanazopewa watoto zimefanyiwa utafiti lini? Hutapata jibu

Na Oxford baada ya kufanikisha kutengeneza dawa ya Covid wameombwa watengeneze ya Gono sugu (Super Gonorrhoea) na ipo njiani

Na pia zinakuja vidonge vya covid pia wakati sisi bado tunapiga miluzi tu
IMG_0815.jpg
 
Chanjo ya malaria ilianza kufanyiwa majaribio miaka mingi nyuma hata kabla Covid kuingia. Hiyo chanjo ubora wake ulikuwa asilimia 55 na hii waliyoisema leo Ni asilimia 77 ndo Maana imeleta tumaini Kwamba Ni chanjo yenye nguvu.

Africa walikuwa wanafanya majaribio Kenya, Malawi na Ghana.
Mwaka 2019 nlikuwa Kenya walikuwa wanatoa chanjo ya Malaria kwa Watoto wa Umri wa miezi 6 kwenye "County" huku tunaweza kuita mikoa iliyoathirika zaidi na Malaria.

Na hii chanjo inatolewa kwa Watoto Kama ilivyo za surua, polio, TB etc
 
Kwa miaka karibu 100, hapakuwa na juhudi kubwa katika kutafuta chanjo ya Malaria, bali makampuni yalijikita zaidi kwenye kutengeneza dawa, maana ilikuwa inalipa zaidi.

Ghafla baada ya kuzuka Corona na wakaweza kuja na ‘Chanjo’ ndani ya miezi michache, na baada ya Afrika kuigomea chanjo hiyo, sasa wamekuja na ‘Chanjo’ ya Malaria, na wamelenga kuwapa waAfrika tu, maana ndio kuna malaria zaidi wanadai.

Je, utakuwa tayari kudungwa chanjo hiyo endapo ikiletwa?

View attachment 1761343
BILA CHANJO NIMEISHI MIAKA 30 BILA MALARIA ! HIYO CHANJO SICHOMI NG'OOOO
 
Kwa miaka karibu 100, hapakuwa na juhudi kubwa katika kutafuta chanjo ya Malaria, bali makampuni yalijikita zaidi kwenye kutengeneza dawa, maana ilikuwa inalipa zaidi.

Ghafla baada ya kuzuka Corona na wakaweza kuja na ‘Chanjo’ ndani ya miezi michache, na baada ya Afrika kuigomea chanjo hiyo, sasa wamekuja na ‘Chanjo’ ya Malaria, na wamelenga kuwapa waAfrika tu, maana ndio kuna malaria zaidi wanadai.

Je, utakuwa tayari kudungwa chanjo hiyo endapo ikiletwa?

View attachment 1761343
Tuwakilisheni
 
Back
Top Bottom