Timu ya Chuo Kikuu cha Oxford iliyohusika kutengeneza chanjo ya Oxford-AstraZeneca Covid-19 imetengeneza chanjo dhidi ya malaria inayofikia kiwango cha juu cha ufanisi kwa 75% ya Shirika la Afya Ulimwenguni. Chanjo hiyo imepewa jina la R21
Chanjo ya kwanza kugundulika ni RTS mwaka 2015 ambayo Ufanisi wake ilikuwa 29.9% kwa kipindi cha kwanza cha majaribio ya kliniki na 57.7% kwa malaria kali.
Kulingana na matokeo ya awali kutoka kwa jaribio la kliniki lililochapishwa Aprili 22, 2021 imeonesha R21 ni mafanikio makubwa dhidi ya vita ya malaria, ambayo ni chanzo kikubwa cha vifo duniani.