#COVID19 Chanjo ya UVIKO-19: Wasiotaka kuchanjwa wafunguliwe kesi ya kutaka kujiua

#COVID19 Chanjo ya UVIKO-19: Wasiotaka kuchanjwa wafunguliwe kesi ya kutaka kujiua

Joined
Apr 12, 2021
Posts
33
Reaction score
24
Wadau,

Dunia sasa linaingia katika wimbi la nne (fourth wave) ya maambukizi ya korona, kama tunavyosikia na kuona kupitia vyombo vya habari vya kimataifa, Ujerumani maambukizi yamefikia takriban 52,000+ ndani ya masaa 24 ambacho ni kiwango kikubwa ukilinganisha na waves zilizopita huko nyuma, na kwamba wengi wa waathirika ni wale ambao wanapinga kupewa chanjo.

Jana tumesikia jirani zetu kenya wametangaza ifikapo Desemba mosi kuwanyima access ya kuingia mahotelini na kwenye mabasi ya abiria wale ambao hawajapata chanjo.

Tukumbuke kuwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, Tanzania kwa sasa ni majira ya joto, na kwamba historia inatuonyesha changamoto za uviko-19 inaiathiri nchi yetu na majirani zetu tunapoanza kuingia majira ya masika/baridi kuanzia Mwezi March hadi June.

Tumeona jitihada za serikali na vyombo karibu vyote vya habari zikihamasisha wananchi kupata chanjo ili kujiwekea kingamwili kupambana na corona. Hata hivyo tunaona mwitikio wa watu bado mdogo.

Kwakuwa wananchi ndiyo rasilimali ya kwanza kwa serikali, na kwamba serikali ina wajibu mkubwa kuwalinda na kuwapigania raia wake wawe wenye nguvu na afya njema wakati wote, napendekeza yafuatayo:

1. Suala la chanjo liwe la lazima kwa watu wote wenye sifa ya kupata chanjo
2. Asasi za serikali na taasisi binafsi wapewe wajibu kuhakikisha wafanyakazi wao wanapewa chanjo
3. Wale wanaokataa kupewa chanjo wafunguliwe kesi ya kutaka kujiua kwa makusudi.

Huu ni mtazamo na maoni ya mdau Sema Kimeumana, Sauti ya Mtu aliaye Nyikani.
 
Na waliochanjwa halafu wanafariki kwa Corona mtawalipa fidia familia zao?

Kwenye swala la Corona mnatulinganisha na Ujerumani na Marekani, tukija kwenye demokrasia mnasema huko ni ulaya hatufanani.
 
Wale wanaokataa kupewa chanjo wafunguliwe kesi ya kutaka kujiua kwa makusudi.
====
Tuombe Mungu maelezo yaliyo ndani ya link hiyo hapo juu yawe fake news.
 
====
Tuombe Mungu maelezo yaliyo ndani ya link hiyo hapo juu yawe fake news.
Kuna mahali niliona kuwa MD wa kampuni fulani inayotengeneza chanjo moja maarufu, hajachanjwa!
 
Kama umepata Chanjo ni wewe, mwili na akili yako ipo kwenye maandaliza ya ujio wa kiongozi wenu
 
Unamshitaki vipi mtu ambaye anatakakujiua mwenyewe?,pengine anatakakuwahi nafasi ya kuwa mwenyekiti wa malaika mbinguni.
Kutaka kujiua ni kosa kisheria. Ni jitihada za kutaka kupunguza rasilimali watu katika taifa.
Ni hujuma.
Haikubaliki.
 
Acha upumbavu..
Uviko Bongo HAKUNA

TEMBELEA CLUBS uona wanavyojazana bila barakoa
 
Back
Top Bottom