Tetesi: Chanjo za Corona zimetua nchini rasmi

Tetesi: Chanjo za Corona zimetua nchini rasmi

Kivumishi Kielezi

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2019
Posts
1,028
Reaction score
2,451
Vipi, mbona zimeingizwa kinyemela sana?

Wamesubiri wakati ambapo sakata la sabaya limekolea na wao wakachomekeamo na chanjo humo humo!

Kama chanjo ni kitu chema, mbona wanakificha ndani ya habari za akina sabaya? ili watu wasitilie maanani ama?

Mimi nilifikiri ujio wa chanjo ulipaswa kuwekwa wazi ili kila mtu atambue kwamba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ameridhia kuchanja watu wake!

Hii ingewapa watu ari ya kudungwa hizo chanjo kutoka ulaya ili tudhibiti gonjwa hatari la corona.

Kwanini wameamua kuziingiza chanjo kupitia vichochoroni tena wakati ambapo umma wa watanzania umejikita na drama za sabaya?

Hakuna japo kavideo cha Rais kutoa tamko na kuhimiza watanzania wadungwe chanjo?
IMG-20210604-WA0005.jpg
 
Sasa wewe ulitaka zile live coverage za kujimwambafai kwa kila hatua ,au uchokozi tu.uzuri hivi sasa hakuna wasiojulikana na wengine wameanza kushughulikiwa
Tutajuaje kama chanjo zimeingia bila kupata taarifa rasmi ya umma?

Hako kahabari wamekaposti facebook huko kwenye kaukurasa cha Gerson Msigwa!

Watu watajuaje?
 
Hii thd yako umeandika kama TETESI halafu unadai chanjo zimesha letwa? Ukaweka na hiyo taarifa kwa vyombo vya habari toka Ikulu ambayo ukiisoma kwa makini inaonyesha kabisa kua kuna mpango wa kuletwa chanjo na sio kwamba chanjo zimeshafika,

Hivi hua mnapata faida gani kukimbilia kuanzisha thd zisizokua na kichwa wala miguu? Kama upo free sana tafuta shughuli yeyote ya halali ili uwe busy.
 
Hii thd yako umeandika kama TETESI halafu unadai chanjo zimesha letwa? Ukaweka na hiyo taarifa kwa vyombo vya habari ambayo ukiisoma kwa makini inaonyesha kabisa kua kuna mpango wa kuletwa chanjo na sio kwamba chanjo zimeshafika,

Hivi hua mnapata faida gani kukimbilia kuanzisha thd zisizokua na kichwa wala miguu? Kama upo free sana tafuta shughuli yeyote ya halali ili uwe busy.
Unalia nini wakati taarifa ya ikulu inajieleza yenyewe!
 
Back
Top Bottom