Channel Ten ilikuwa Mali ya CCM kuanzia lini?

Channel Ten ilikuwa Mali ya CCM kuanzia lini?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Wakati wa Magufuli ..siku moja alienda kutembelea Mali za chama akaenda kutembelea kituo maarufu cha TV cha Channel ten.

Ndo tukatangaziwa kuwa na chenyewe ni Mali ya Chama Cha Mapinduzi...

Wanaojua historia ya channel ten na kampuni iliyokuwa inamiliki hiyo channel
ya African Media Group..pamoja na channel zingine kama Dtv na baadae CTN..tulibaki mdomo wazi..

Swali langu lini CCM ilinunua hiii kampuni?
Au ndo moja ya 'uporaji 'uliofanywa?

Kuna mwenye maelezo ya kina??

Cc Pascal Mayalla ..wewe umewahi fanya kazi African Media Group.. Unajua lolote??
 
Ccm ilikua Ina hisa kwenye kampuni hii kupitia kwa aliekuwa mweka hazina wa CCM ndugu Rostam Aziz

Alipoingia Magufuli akateua kamati kufuatilia Mali za CCM, ikagundulika hisa za CCM bado zipo mikononi mwa Rostam. Rostam alipoambiwa akaziachia mara moja na kuifanya CCM kuwa mmiliki halali
 
[emoji848][emoji848]View attachment 1755116
Screenshot_20210418-062648.jpg
 
CCM kuwa na hisa kupitia mweka hazina maana yake ndio nini?

Zilikuwa Hisa asilimia ngapi??
Ccm ilikua Ina hisa kwenye kampuni hii kupitia kwa aliekuwa mweka hazina wa ccm ndugu Rostam Aziz
Alipoingia Magufuli akateua kamati kufuatilia Mali za ccm,ikagundulika hisa za ccm bado zipo mikononi mwa Rostam
Rostam alipoambiwa akaziachia mara na kuifanya ccm kuwa mmiliki halali
 
CCM kuwa na hisa kupitia mweka hazina maana yake ndio nini?

Zilikuwa Hisa asilimia ngapi??
Ni uamuzi wa kamati kuu chini ya mkapa
Ccm pia ilikua na hisa Vodacom kupitia Rostam lakini bahati mbaya Tena😭😭
Ndio Mana Kuna kipindi chadema walianzisha kampeni ya kususia Vodacom,kwa sababu inamilikiwa na ccm
Matokeo yake Rostam akauza hisa zake kwa Tsh Bilioni 450!
 
Back
Top Bottom