"uchunguzi wa awali" dereva alishindwa kulimudu gari kwenye mteremko mkali.
Huyo dereva ni mgeni kwenye hiyo Barabara? Huyo dereva ni mgeni kwenye kazi ya udereva?
Kama anapita kila siku kwanini leo ashindwe kulimudu hilo kwenye huo mteremko anaopita mara kwa mara?
Uchunguzi wa kina unapaswa kufanyika na kuja na majibu yalinyooka yenye kueleza mzizi wa tatizo, na matatizo mengine mengine yaliyojitokeza ambayo yasingekuwepo basi madhara huenda yangepungua, lakini mwisho kuwe na mpango kazi wakuondoa na kutokomeza hizo ajali.
HATUWAFUNDISHI KAZI! TUNAJARIBU KUWEKA MAONI YETU MAANA NI KAMA MPAKA SASA HAKUNA SULUHU WALA MIPANGO YAKUONDOA HIZI AJALI ZAIDI YAKUMUACHIA MWENYEZI MUNGU AMBAYE AMETUPA AKILI NA MAARIFA ILI TUWEZE KUISHI KWENYE DUNIA HII.
1. Gari ina Km ngapi mpaka sasa?.
2. Gari imenunuliwa lini na wapi?.
3. Historia ya matengenezo ya gari.
4. Gari ina bima ya aina gani?
5. Mmiliki wa Gari anahistoria gani kwenye hii biashara.
6. Dereva ana leseni ya uendeshaji gari.
7. Leseni ya dereva ina Daraja la kuendesha basi la abiria.
8. Dereva ana historia gani kwenye maisha.
9. Dereva ana maradhi ya akili au historia.
10.Dereva ana historia yeyote ya maradhi ya muda mrefu na Afya yake mpaka anakufa?.
11. Utaratibu wa kuajili madereva kwenye kampuni ukoje?.
12. Utaratibu wa kupumzika kwa madereva ukoje kwenye hiyo kampuni?
13. Kampuni ina mafunzo yeyote inayotoa Kwa madereva na mafundi wake?
14. Kampuni ina mafundi waliohitimu na Uzoefu wa hiyo kazi?
15. Elimu na Uzoefu wa dereva ukoje?
14. Hali ya Barabara ilikuwaje wakati wa ajali?
15. Kuna alama zozote zinazotahadharisha Kabla ya mteremko.
Maswali yako mengi, kazi ya uchunguzi ikifanyika Kwa ueledi tunaweza kuziondoa hizi ajali.