hata mimi
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 1,356
- 1,442
Habari zenu wanajamii,
Nakumbuka miaka ya nyumanyuma nkiwa mdogo nimewahi kutolewa funza mara kadhaa miguuni na nikawa nikigombeshwa sana kuhusu kuchezea mavumbi, mazingira machafu na majalalani eti ndipo wanapopatikana wadudu hao
Sasa hivi kila nikiwauliza Wazee sababu halisi ya funza wananambia ni Uchafu tena wananambia eti kuwa ile ya miaka ya tisini ilikuwa kama mwishilizio tu wa funza. Wanasema miaka ya nyuma kulikuwa na funza sana haswa maeneo ya Tanga na Manyara (kwingine sijui mana sijaulizia)
Watu wameliwa na funza sana enzi hizo (kwa ninavyohadithiwa na Wazazi) mpaka hawakuweza kuvaa viatu kabisa na wengine walishindwa hata kutembea kabisa.
Halafu tiba yao ilikuwa ni kutumbuliwa miguu na kuwekwa chumvi tu. Kwa wale ambao waliliwa sana na funza kupita kawaida wamekuwa rahisi kutambulika hata kwa sasa kutokana na namna ya kutembea kwao
Sasa mimi kila nikitafakari kuwa sababu ilikuwa ni uchafu naona inapingana na uelewa wangu kwani kama ni uchafu mbona kuna watu wachafu sana hata sasahivi lakini imezidi sana sana utamkuta na chawa tu, kama ni majalalani kuna ambao wanaishi huko kabisa lakini hawana funza!
Pia kama ni jiografia ya eneo (kwamba mavumbi au aina fulani ya udongo) mbona sasahivi hakuna funza? Au jiografia imebadilika?
Naomba kwa mwenye uelewa (kitaalamu) juu ya tatizo hilo la funza kushambulia watu sana enzi hizo atufafanulie hapa
Ahsante.