Chanzo cha kuchokana, kununiana katika mahusiano/ndoa na jinsi ya kukabiliana na tatizo hili

Sio bure utakuwa umelogwa wewe,yaani kila siku ananuna halafu unambembeleza sasa utakuwa umeoa au umeolewa kubembeleza hiyo ni kazi ya mke ukirudi home umechoka anakuliwadha.
 
couple are like products life cycle, needs rejuvenation on decline stage!
 
natumia kamchina ningekugongea LIKE.uko kama mimi,Hata mumewangu aniudhi vipi,baada ya muda najikuta namsemesha.
 
Billie ukitoa sababu moja wengine watajifanya hawahusiki. Hapa nilitaka kila mtu aseme sababu zake kwa bahati kuna mtu tayari kakupa 100% kwa 100% ina maana umemgusa!!
 
Last edited by a moderator:
Billie ukitoa sababu moja wengine watajifanya hawahusiki. Hapa nilitaka kila mtu aseme sababu zake kwa bahati kuna mtu tayari kakupa 100% kwa 100% ina maana umemgusa!!

Pamoja ndugu yangu asante kwa uelewa wako wa hali ya juu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, maudhi ni sababu inayoongoza kwenye kuchokana. Natamani kuandika Zaidi, nikipata muda nitarudi

Wanaume mara nyingi huwa wa mwanzo kuwachoka wanawake hasa kama sio wabunifu! yaani mastress kibao kazini lakini ukija home style ya nyumba iko vile2, hamna kipya na pengine bibie yuko nje anapiga soga na washoga zake!!
Wakati mwengine hamna hata sababu ni jukumu la mwanamke kumuelewa na kumrudisha mumewe katika upendo!

Mwanamke hachoki mpaka mwanaume aanze kuyumba kutoa HUDUMA!!:coffee:
 
Ni kawaida sana mkuu somethinglike that to happen,we are not the same
 
Naomba mwongozo hapa. Mimi nilidhani kuchokana siyo lazima kwa wanandoa. Hata ule uhusiano ambayo si ya kindoa.......
 
Naomba mwongozo hapa. Mimi nilidhani kuchokana siyo lazima kwa wanandoa. Hata ule uhusiano ambayo si ya kindoa.......
Kwa upande wa wanawake kumchoka mwanaume ni hiyo kushindwa huduma (nadhani wanielewa hapa!) kwa upande wa mwanamme kumchoka mwananke inategemea na ubunifu wa huyo mwanamke na pia overspending huchangia kuchosha!
 
Na mwanamke akitaka nimchoke awe anapenda pesa sana, yaani kila muda aombe ombe; pocket digger! Hawezi chukua round huyo namwacha within no time! Lakini pia mwanamke akitaka Mawe yangu asiwe na tabia ya Kuomba omba tu tayari huyo ntakuwa najiresi mwenyewe hadi atashangaa! Pesa ataikimbia!!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Naomba mwongozo hapa. Mimi nilidhani kuchokana siyo lazima kwa wanandoa. Hata ule uhusiano ambayo si ya kindoa.......
Uko sahihi kabisa... kuchokana si lazima iwe kwa wanandoa peke yao bali hata BOy au Girlfriend.
 
elimu ni nzuri sana kikubwa tusimame imara kwenye ndoa na tuaminiane kwa kila hali mengine yatakuwa shwari kabisa
 
Ni mada nzuri mkuu ya kujenga;tumeyashuhudia mengi kama haya na yapo katika jamii yetu.barikiwa
 
Sio bure utakuwa umelogwa wewe,yaani kila siku ananuna halafu unambembeleza sasa utakuwa umeoa au umeolewa kubembeleza hiyo ni kazi ya mke ukirudi home umechoka anakuliwadha.

wala sijalogwa,nina mshukuru Mungu nina moyo wa kusamehe na nina upendo wa kweli.Sipendi nipate shida na sipendi mwingine apate shida.Mume wangu pia ni rafiki angu,siwezi kukaa karibu na rafiki hana raha halafu nione its ok,lazima nitatatua tatizo lake la kununa kwanza ndio mengine yafuate.Ukitaka uishi maisha marefu kuwa na amani na upendo na watu wote!
 
Shukurani
Kwa elimu.
 
Jamani hii hali haipendezi.

Kwa waliopendana na kuishi maisha ya pamoja kwa miaka ..... na bahati mbaya mmoja wenu hawezi kuhama chumba....lakini mnanuniana.. hamuongei... tena bila sababu za msingi....

Maana hata mkiulizwa sababu ya kununiana huko ni nini hakuna mwenye jibu.... mume gubu... mke kiburi....wakija wageni kila mtu anaongea na mgeni kivyake .. hata kama kuna mada inaendelea mnakaushiana..

Acheni hizo... kumbuka wakati ule ulivyokuwa unamhangaikia huyo mwanamke na wewe mwanamke kumbuka jinsi ulivyompenda huyo jamaa..
 
kununiana ndo mapenzi hisia zinachukua nafasi yake zaidi wanunianao ndiyo wapendanao
 
Ni kweli kuna wakati kuna kuna kununiana, lakini isiwe sababu ya kuharibu mahusiano yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…