Acha upotoshaji wako hapa ,, Tangia tupate Uhuru serikali ya CCM imekuwa ikipambana na maadui ujinga maradhi na umaskini kwa Kasi ya mshale, mfano katika kupambana na umaskini serikali ya CCM imeweka mazingira wezeshi kwa kila mtu kuweza kunufaika na fursa mbalimbali zinazopatikana hapa nchini, serikali imejitahidi kutumia Rasilimali zetu katika kuboresha huduma za kijamii na Miundombinu ambayo imemsaidia mtanzania katika kujikwamua kiuchumi, mfano kwa Sasa mkulima anaouwezo wa kusafirisha mazao yake Hadi sokoni kwa urahisi kabisa
Lakini pia usambazaji wa umeme Hadi vijijini umefungua fursa nyingi za kiuchumi na kusaidia vijana na makundi mengine kuweza kujiajiri kwa urahisi na hivyo kujipatia kipato na kuondokana na umaskini kwa mtu mmoja mmoja,
Katika kilimo pia ambayo Ni secta tegemezi kwa watu wengi serikali imekuwa ikiongeza bajeti mwaka Hadi mwaka mpaka Sasa kufikia billioni Mia Tisa na point, Hali hii imesaidia kuongeza uzalishaji na kupunguza umaskini kwa kaya nyingi hapa nchini, hii Ni pamoja na kuhakikisha mkulima anapata soko la uhakika, lakini pia serikali imekuwa ikitoa Ruzuku kila inapowezekana Kama ilivyofanya kipindi hiki kwa kutoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini na kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni
Katika Elimu nako juhudi za serikali zimekuwa kubwa Sana ikiwa Ni ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi shule za msingi ,kuongeza ujenzi wa madarasa na shule mpya ili kuendana na ongezeko la wanafunzi, vyuo vya Kati na hata vya Elimu ya juu navyo vimeongezwa na serikali, hivyo kutoa fursa kwa vijana wengi kupata Elimu bila shida yoyote, hapa pia serikali imeondoa vikwazo vya kupata Elimu hata kwa wanafunzi wanaotoka familia maskini kwa serikali kufuta ada kuanzia shule za msingi Hadi sekondari, lakini pia serikali imekuwa ikiongeza bajeti ya Elimu ili vijana wengi wapate fursa ya Elimu ya juu
Katika Afya pia serikali imejenga zahanati kwa kila Kijiji na pia vituo mbalimbali vya Afya vimejengwa maeneo mengi hapa nchini ikiwemo 234 vilivyo jengwa hapa majuzi tu, hii imepunguza vifo vya mama na mtoto, lakini pia watanzania wengi Sasa wanapata huduma karibu kabisa na maeneo yao, huduma mbalimbali za kibingwa zimekuwa zikitolewa katika hospitali zetu za Kanda na Taifa ambapo awali wagonjwa walikuwa wanalazimika kwenda nchi za nje na wale wakipato Cha chini walikuwa wanaishia kupoteza maisha,
Mambo iliyoyafanya serikali ya CCM ni mengi Wala siwezi kumaliza kuyaelezea hapa, kikubwa nakushauri tu kuwa nenda kawaambie chadema wenzio kuwa watu wanasema ni aibu kwa chadema kukaa miaka yote na kupokea mamilioni kwa mamilioni Kama Ruzuku lakini mmeshindwa kujenga hata ofisi za makao makuu na kuishia kuzitafuna zote na kulewea mapombe tu, watu pia wanauliza pesa mlizochangisha majuzi za join the chain zipo wapi? Mbona kimya au nazo mmepeleka kwenye pombe?
Mwisho Ni kuwa watanzania Wana Imani na matumaini makubwa Sana na serikali ya CCM chini ya mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani, na kwamba hawana habari Wala mpango wa kuwaunga upinzani uliyojichokea na kukosa ajenda na Sera za kueleweka, wanasema wameshawapuuza kwa Sasa na kuwaacha na ubabaishaji wenu