Chanzo cha mvua za radi Dar es Salaam na Pwani

Kwanni kirefu kipigwe na Radi na sio kifupi( maybe mti) kwaiyo majengo marefu pale posta ni hatari kipindi cha Radi
Nimeuliza kwa niaba yako na nikapata jibu hili:

Hili ni swali zuri sana na ni muhimu kwa usalama wa majengo na watu. Sababu ya radi kupiga vitu virefu zaidi inahusiana na kanuni ya "njia ya mkondo mfupi zaidi" (path of least resistance).

Hapa kuna maelezo ya kitalaamu kwa lugha rahisi:

1. Kwa nini kitu kirefu?​

Radi ni mkondo mkubwa wa umeme unaotafuta njia ya kufika ardhini kutoka kwenye mawingu.

  • Ufupishaji wa Umbali: Hewa ni kizuizi kibaya cha umeme (insulator). Radi inapotafuta njia ya kushuka, inajaribu kupunguza umbali inayopaswa kupita kwenye hewa.
  • Mvuto wa Chaji: Mawingu yanapokuwa na chaji hasi (negative), ardhini kunatokea chaji chanya (positive). Chaji hizi chanya hupanda juu kupitia vitu virefu kama miti au majengo. Kitu kirefu kinakuwa karibu zaidi na wingu, hivyo radi "huona" ni rahisi kuruka kuelekea hicho kitu kuliko kuendelea kusafiri hewani hadi kufika kwenye kitu kifupi.

2. Je, majengo marefu ni hatari?​

Jibu ni: Ndiyo na Hapana. Inategemea na jinsi jengo lilivyojengwa.

  • Ndiyo (Hatari): Majengo marefu yana uwezekano mkubwa wa "kuvuta" radi kuliko nyumba fupi. Kama jengo halina mfumo wa ulinzi, radi inaweza kusababisha moto, kupasua kuta, au kuharibu vifaa vyote vya umeme ndani ya nyumba.
  • Hapana (Salama): Majengo mengi marefu ya kisasa (kama yale ya Dar es Salaam) ni salama sana kwa sababu yanatumia Kikinga Radi (Lightning Arrestor/Rod).

3. Kikinga Radi (Lightning Rod) hufanyaje kazi?​

Hiki ni kifaa cha chuma kinachowekwa juu kabisa ya jengo. Badala ya radi kupiga kuta za jengo, inapiga kile chuma. Chuma hicho kimeunganishwa na waya mnene wa shaba unaopeleka ule umeme wa radi moja kwa moja ardhini (Earthing) bila kugusa sehemu nyingine za jengo.


Ushauri wa Usalama​

Kama uko kwenye jengo refu wakati wa mvua ya radi:

  1. Usiwe karibu na madirisha: Kioo kinaweza kupasuka kutokana na mshtuko.
  2. Kaa ndani: Majengo marefu yenye fremu za chuma au zege imara kwa kawaida hupitisha umeme kwenda ardhini nje ya kuta, hivyo kuwa ndani ni salama zaidi kuliko kuwa nje.
  3. Miti ni hatari: Mti ni "kifaa" kirefu lakini hauna njia ya kupeleka umeme ardhini kwa usalama kama kikinga radi, hivyo unaweza kupasuka au kuwaka moto.
 
Asante kwa maelezo mkuu. Juzi mvua iliponyesha Dar, radi ilipiga ikaharibu mifumo ya umeme hadi circuit breaker ikajizima yenyewe. Ni bora kuzima umeme nyumbani kunapokuwa na radi.
 
Asante sana mkuu. Umeeleza vema sana.
 
Mtaalamu wa hali ya hewa napingana nawewe bila sababu yoyote Ile!

Ila ukija vizuri sababu nitatoa
 
Good
 
kiboko ya radi ni Kondoo tu..Mengine ni kuchukua tahadhari na Maombi kwa Mola wako.

Sema nini, wanangu mnatuchota sanaaaa 😑🀠
Kwamba, "eti kondoo anazuia radi? "

radi, ni umeme mkali unapiga kwa muda mfupi mno (zaidi ya Volts milioni 100, Ampere karib 30,000A, na joto kali sana (that's why sehem iliyopigwa radi directly huwa inaungua)

Radi inapiga fasta kuliko hata spidi ya kufumba na kufumbua jicho (spidi ya chap kwa sekunde 0.1, hii ni haraka mno kuliko spidi ya kufumba na kufumbua jicho ambayo ni 0.3 second)

Sasa imagine, nguvu ya umeme wote huo impige kondoo fastaaaa afu eti uniambie kondoo atashinda.,.. Aiseee πŸ€”

"Guys??" (kwa sauti ya Mwigulu)

Ipo hivi..
Tanesco wanaposafirisha umeme mkoa mpaka mkoa, husafirisha kwa Volts Laki 1-4. (na huu umeme wa tanesco tu ukiwekwa kwa sekunde 0.1, sijui hata kama utapona)

Sasa imagine ule wa radi wenye zaidi ya ampere 30k, na Volts zaidi ya milioni 100.? πŸ€” Calculate nguvu yake hapo.

Na tukumbuke, kondoo anapitisha umeme vizuri sanaaaaaa (ni good conductor wa electricity)

Sasa, fikiria huu mzigo utafanya nini kwenye "Electrons zilizopo kwenye kila Atoms zinazounda Cells zote mwilini za kiumbe hai kama kondoo"


Anyway:
Waulize, Madaktari, Electrical engineers, watu wa Molecular Biology, watakupa jibu nini kitatokea kwenye Misuli, Mfumo wa Fahamu na Moyo.
 
Ila radi za mikoani siyo poa inapiga mpaka unaingia
Wakuu, Radi haichagui mahali ikiamua kupiga mahali inapiga tu tena ukute siku hyo inahasira hata uwe wapi itakufuata tu...kiboko ya radi ni Kondoo tu..Mengine ni kuchukua tahadhari na Maombi kwa Mola wako.
Iv hii inaukweli dawa ya radi ni kondoo
 
Unasemaje wewe???

Yaani kondoo apigwe radi apone?

Unaijua radi vizuri mkuu?

Kiumbe hai hakiwezi kupambana na umeme.
kondoo vs Radi. Huu mpambano huwa mkali usiombe ukashuhudia nyasi zinavopata tabu..mwisho Kondoo anabaki mzima radi inatoweka.
 
Sema Lindi kule Pwani kabisa hakunaga sana radi
Lakini wilaya zake sasa, Radi za Ruangwa na Nachingwea πŸ™Œ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…