Chanzo cha mvua za radi Dar es Salaam na Pwani

Chanzo cha mvua za radi Dar es Salaam na Pwani

Kwani Dar kwa sasa imekaribiana na Sumbawanga au....!!?
Nimemjibu mtu aliyeongea kuhusu radi za huko Mwanza mkuu. Hata Mwanza kuna mafundi sio Sumbawanga tu.
 
Ni afadhali usimame kwenye uwanja mweupe unyeshewe ulowe kisha utakauka badala ya kujikinga mvua chini ya miti na nguzo ndefu, huku ukihatarisha maisha yako bila sababu ya msingi.
Ukisimama kwenye uwanja mweupe ambapo hakuna kilichokuzidi urefu mfano mti au nguzo.

Upo hatarini kupigwa na radi maana itakushukia wewe mwenye urefu kuliko mazingira yaliyokuzunguka hivyo suluhisho ni kulala chini.
 
Wahenga mtakubaliana na mimi 100% kwamba miaka ya nyuma mvua zilizokuwa zikinyesha Dar es salaam hazikuambatana na radi hata kidogo. Tulizoea kusikia matukio ya radi hasa huko Kigoma, Shinyanga, Tabora na mikoa mingine ambako matukio ya watu kuuliwa na radi yalikuwa yakiripotiwa mara kwa mara. Mvua za Dar es Salaam na Pwani zilikuwa za kumbembeleza mtoto alale.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, miaka ya karibuni kumekuwa na radi nyingi sana mikoa ya pwani hasa wakati huu wa mvua za masika. Kwa mfano siku ya leo (18.3.2026) wanafunzi watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo Jiji la Dar es Salaam wameuliwa na radi wakati wakicheza shuleni kwao. Hili limenilazimu, kama mtaalamu wa hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi, kutoa elimu kuhusu chanzo cha kuongezeka kwa matukio ya radi ukanda wa Pwani na Dar tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma. Radi na ngurumo zinazoambatana na mvua za hivi karibuni mikoa ya Pwani na Dar es Salaam zinasababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na kuongezeka kwa unyevu angani wakati wa msimu wa masika. Mvua hizi mara nyingi huambatana na radi kali. Kwa ufupi, chanzo cha kuongezeka kwa radi katika ukanda huu ni:

1. Kuongezeka joto na unyevu angani, hali ambayo husababisha radi na ngurumo.

2. Mabadiliko ya hali ya hewa duniani yamefanya mifumo ya mvua kuwa kali zaidi, ikiwa ni pamoja na kuleta ngurumo, kitu ambacho kilikuwa nadra hapo awali.

Namna ya kuepuka kupigwa na radi ni kutokaa chini ya miti mirefu au nguzo za umeme na kuepuka kutembea peku ndani ya maji wakati mvua inaendelea kunyesha. Ni afadhali usimame kwenye uwanja mweupe unyeshewe ulowe kisha utakauka badala ya kujikinga mvua chini ya miti na nguzo ndefu, huku ukihatarisha maisha yako bila sababu ya msingi.

Nawasilisha.
Mkuu una uhakika na unachosema? Dar inakuwaga na radi tangu zamani ila inategemea mwaka na mwaka. Kama unavyojua radi hutokea pale condition fulani zinapokuwepo, hivyo kila mwaka hazipo ila siyo kwamba hakukuwa na radi.
 
Nataman watoa maelezo wa radi watoke kwenye makundi ya maeneo manne tofauti ili kupata elimu ya kisayansi,kienyeji(kiiman) na natamani watu wa kanda ya ziwa watoe maelezo,kanda ya juu kusini,magalibi na uku pwani nataman wawakilishwe na wataalamu wa hali ya hewa wenyewe na watujibu kisayansi tena kwa mifano hai sio stori zakifizikia
Kwa Ufupi tu, radi ni umeme, kama ulivyo umeme unaoutumia kila siku umeme uko na tabia zake, moja ya tabia zake muhimu ambayo hapa taizungumzia ni ile ya kutafuta shortcut (njia fupi kukamilisha mzunguko wake).

Mfano, kama uko na uwezo wa kutumia vidole vyako viwili (gumba na kinachofatia), kimoja kikashika live wire na kingine kikashika neutral wire kwa wakati mmoja (exactly wakati mmoja), huwezi pigwa na umeme hata kama uko peku (simaanisha ukajaribu), umeme utapita kutokea kidole kimoja na kutokea kidole kingine na hivyo kukamikisha mzunguko.

Habari ya kondoo kupambana na radi ni chai ilokolea, tena katika wanyama wanaoongoza kwa kuuwawa na radi wengi kwa mpigo ni kondoo, mvua ikinyesha kondoo huwa na tabia ya kujirundika pamoja na kulaliana chini ya mti, radi ikipiga hapo mti utashusha umeme kwenye ground na chini kama pameloana hata kama sio pote kwa tabia Yao ya kulaliana wakipigwa wawili watutu unasambaa kwa wengine.

Swala la urefu wa conductor liko wazi, ni sawa na uko na waya wenye umeme na nyaya mbili moja fupi nyingine ndefu na unazisogeza kwenye chanzo cha umeme, it's obvious ndefu ndo itayowahi kufikia umeme.
 
Wakuu, Radi haichagui mahali ikiamua kupiga mahali inapiga tu tena ukute siku hyo inahasira hata uwe wapi itakufuata tu...kiboko ya radi ni Kondoo tu..Mengine ni kuchukua tahadhari na Maombi kwa Mola wako.
Hehe..elimu kaka elimu, radi ni umeme, au ndo nyie mnaoaminigi zile mambo za radi ni kama Jogoo Mwekundu, sa radi inakasirika vipi na kufuata MTU? umeme hata uwe mkubwa vipi bila ya conductor (waya) kuufikisha kwenye TV Katu haiwezi waka, ukikaa sehemu radi imepiga na hakuna conductor huwezi pigwa, hao wa ndani ni wale unakuta imepiga mfano nyuzi 45, 30 uko ndani umesimama kwa dirisha itakupiga kama maeneo ya nje ni wazi hakuna miti.
 
hahaha ! eti radi ni kama jogoo mwekundu au mnyama mwenye miguu sita mwenye uwezo wa kuzalisha umeme hii ni theory ya mwafrika kabla mzungu ajaja na theory yake kuwa radi ni umeme....kwahyo unabisha kondoo hawezi kupambana na radi?
 
kuna watu hapa kisa tu hakusoma sayansi basi atabisha hata vyenye ukweli

binadamu una umeme hilo pia mtakataa jamaa zangu ,sasa ili shot ipige radi itokee ni lazima hasi na chanya zimekutana,na ardhi inapitisha charges za kutosha sasa inapopiga huwa inapiga vitu virefu eneo la wazi ukajisimamisha wewe ndiyo utakua wa kwanza kula chuma,na ndiyo maana tukijenga nyumba zetu tunaweka earthroad ili ikipiga kwenye nyumba umeme unapelekwa ardhini😂
 
radi hata ukiwa ndani inakufuata..mimi bibi yangu iliwahi kumfuata ndani ikamtupia nje..kipindi nipo F3 classmate wangu iliwahi kumrusha toka kibazani mpaka uwani,, na ilipiga ya maana mimi niliyekuwa ndani nilitoka nje kwa wenge namkuta jamaa kalala uwani..Kuna siku tulikuwa tunachunga mifugo mvua ya radi ikaanza tukaona kondoo anapanda kichuguu kwakuwa tulikuwa tumeshaambiwa na wazazi wetu tukiona hvo tukakae mbali ,aiseee ! tulikuwa tunaona kondoo anavopigiza kichwa chake mpaka cheche zinaluka..bahati mbaya siku hyo tulipoteza ng'ombe wawili kwa kupigwa na radi..kwahyo mkuu Nadhani umepata picha kidogo.
Mkuu cheche kivipi mkuu eeh 😄
Ina maana kondoo wenu pembe zao zina material gani hebu tuongoze kidogo
 
hahaha ! eti radi ni kama jogoo mwekundu au mnyama mwenye miguu sita mwenye uwezo wa kuzalisha umeme hii ni theory ya mwafrika kabla mzungu ajaja na theory yake kuwa radi ni umeme....kwahyo unabisha kondoo hawezi kupambana na radi?
Hakuna kitu kama iko.
 
kuna watu hapa kisa tu hakusoma sayansi basi atabisha hata vyenye ukweli

binadamu una umeme hilo pia mtakataa jamaa zangu ,sasa ili shot ipige radi itokee ni lazima hasi na chanya zimekutana,na ardhi inapitisha charges za kutosha sasa inapopiga huwa inapiga vitu virefu eneo la wazi ukajisimamisha wewe ndiyo utakua wa kwanza kula chuma,na ndiyo maana tukijenga nyumba zetu tunaweka earthroad ili ikipiga kwenye nyumba umeme unapelekwa ardhini😂
Sawa mkuu. Umedadavua vizuri.
 
Namna ya kuepuka kupigwa na radi ni kutokaa chini ya miti mirefu au nguzo za umeme na kuepuka kutembea peku ndani ya maji wakati mvua inaendelea kunyesha
Hii ni elimu ya kitambo sana labda kama siku hizi haifundishwi mashuleni
 
Back
Top Bottom