Chanzo cha mvua za radi Dar es Salaam na Pwani

Kwani Dar kwa sasa imekaribiana na Sumbawanga au....!!?
Nimemjibu mtu aliyeongea kuhusu radi za huko Mwanza mkuu. Hata Mwanza kuna mafundi sio Sumbawanga tu.
 
Ni afadhali usimame kwenye uwanja mweupe unyeshewe ulowe kisha utakauka badala ya kujikinga mvua chini ya miti na nguzo ndefu, huku ukihatarisha maisha yako bila sababu ya msingi.
Ukisimama kwenye uwanja mweupe ambapo hakuna kilichokuzidi urefu mfano mti au nguzo.

Upo hatarini kupigwa na radi maana itakushukia wewe mwenye urefu kuliko mazingira yaliyokuzunguka hivyo suluhisho ni kulala chini.
 
Mkuu una uhakika na unachosema? Dar inakuwaga na radi tangu zamani ila inategemea mwaka na mwaka. Kama unavyojua radi hutokea pale condition fulani zinapokuwepo, hivyo kila mwaka hazipo ila siyo kwamba hakukuwa na radi.
 
Kwa Ufupi tu, radi ni umeme, kama ulivyo umeme unaoutumia kila siku umeme uko na tabia zake, moja ya tabia zake muhimu ambayo hapa taizungumzia ni ile ya kutafuta shortcut (njia fupi kukamilisha mzunguko wake).

Mfano, kama uko na uwezo wa kutumia vidole vyako viwili (gumba na kinachofatia), kimoja kikashika live wire na kingine kikashika neutral wire kwa wakati mmoja (exactly wakati mmoja), huwezi pigwa na umeme hata kama uko peku (simaanisha ukajaribu), umeme utapita kutokea kidole kimoja na kutokea kidole kingine na hivyo kukamikisha mzunguko.

Habari ya kondoo kupambana na radi ni chai ilokolea, tena katika wanyama wanaoongoza kwa kuuwawa na radi wengi kwa mpigo ni kondoo, mvua ikinyesha kondoo huwa na tabia ya kujirundika pamoja na kulaliana chini ya mti, radi ikipiga hapo mti utashusha umeme kwenye ground na chini kama pameloana hata kama sio pote kwa tabia Yao ya kulaliana wakipigwa wawili watutu unasambaa kwa wengine.

Swala la urefu wa conductor liko wazi, ni sawa na uko na waya wenye umeme na nyaya mbili moja fupi nyingine ndefu na unazisogeza kwenye chanzo cha umeme, it's obvious ndefu ndo itayowahi kufikia umeme.
 
Wakuu, Radi haichagui mahali ikiamua kupiga mahali inapiga tu tena ukute siku hyo inahasira hata uwe wapi itakufuata tu...kiboko ya radi ni Kondoo tu..Mengine ni kuchukua tahadhari na Maombi kwa Mola wako.
Hehe..elimu kaka elimu, radi ni umeme, au ndo nyie mnaoaminigi zile mambo za radi ni kama Jogoo Mwekundu, sa radi inakasirika vipi na kufuata MTU? umeme hata uwe mkubwa vipi bila ya conductor (waya) kuufikisha kwenye TV Katu haiwezi waka, ukikaa sehemu radi imepiga na hakuna conductor huwezi pigwa, hao wa ndani ni wale unakuta imepiga mfano nyuzi 45, 30 uko ndani umesimama kwa dirisha itakupiga kama maeneo ya nje ni wazi hakuna miti.
 
hahaha ! eti radi ni kama jogoo mwekundu au mnyama mwenye miguu sita mwenye uwezo wa kuzalisha umeme hii ni theory ya mwafrika kabla mzungu ajaja na theory yake kuwa radi ni umeme....kwahyo unabisha kondoo hawezi kupambana na radi?
 
kuna watu hapa kisa tu hakusoma sayansi basi atabisha hata vyenye ukweli

binadamu una umeme hilo pia mtakataa jamaa zangu ,sasa ili shot ipige radi itokee ni lazima hasi na chanya zimekutana,na ardhi inapitisha charges za kutosha sasa inapopiga huwa inapiga vitu virefu eneo la wazi ukajisimamisha wewe ndiyo utakua wa kwanza kula chuma,na ndiyo maana tukijenga nyumba zetu tunaweka earthroad ili ikipiga kwenye nyumba umeme unapelekwa ardhini😂
 
Mkuu cheche kivipi mkuu eeh 😄
Ina maana kondoo wenu pembe zao zina material gani hebu tuongoze kidogo
 
hahaha ! eti radi ni kama jogoo mwekundu au mnyama mwenye miguu sita mwenye uwezo wa kuzalisha umeme hii ni theory ya mwafrika kabla mzungu ajaja na theory yake kuwa radi ni umeme....kwahyo unabisha kondoo hawezi kupambana na radi?
Hakuna kitu kama iko.
 
Sawa mkuu. Umedadavua vizuri.
 
Namna ya kuepuka kupigwa na radi ni kutokaa chini ya miti mirefu au nguzo za umeme na kuepuka kutembea peku ndani ya maji wakati mvua inaendelea kunyesha
Hii ni elimu ya kitambo sana labda kama siku hizi haifundishwi mashuleni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…