Chanzo cha taarifa za kuhujumu nchi zinapaswa kutolewa na nani ili usalama wa taifa waingie kazini?

Chanzo cha taarifa za kuhujumu nchi zinapaswa kutolewa na nani ili usalama wa taifa waingie kazini?

wisedickson

Member
Joined
Jun 2, 2015
Posts
11
Reaction score
2
Kwa Uelewa wangu watendaji kazi wakubwa wa ulinzi wa ndani ya Nchi ni Usalama wa Taifa, na hawa wanapaswa kuwa makini sana na kila kitisho kinachotokea katika nchi kabla hata hakijafika polisi kutokana na mtindo wa mafunzo yao.

Lakini katika Taifa langu Tanzania, Usalama wa Taifa wanawajibika kuilinda serikali mithili ya Ujasusi wa ndani.

Hivi karibuni kumekuwa na hoja zilizotolewa na watu mbalimbali ikiwemo Polepole juu ya ufisadi lakini hakuna hatua iliyochukuliwa

Kuna kipindi fulani pia Marehemu Mengi amewahi kutaja Mafisadi lakini hakuna uchunguzi wala taarifa iliyotolewa kwa umma kuhusu kufatilia uhalali wa taarifa zinazotolewa.

Je, Si wajibu wa TISS kufatilia kila dokezo ili kuweza kuilinda nchi dhidi ya ufisadi?

Nani aatakayetoa taarifa ndo asikilizwe? Na vipi anayepaswa kutoa taarifa akiwa na maslahi na taarifa hiyo?
 
Back
Top Bottom