Ngoja nikumbuke Geography yangu ya form two niliyofundishwa na Mrs. Mbwiluga.
Dunia ni sayari mojawapo iliyopendelewa sana kwa kuwa na tabaka nene la hewa. Katika tabaka hili ndiyo wamo akina Hydrogen, Oksijeni, Nitrogen na wengineo. Kwa hali hiyo, na kulingana na mwl. wangu kipenzi wa Jiografia Mrs. Mbwiluga, HEWA IPO TU KATIKA USO NA ANGA LA DUNIA INAELEA.
Katika hali ya kawaida hewa hii inapaswa kuwa tuliii imetulia (kama chumbani mwako ikiwa hujachochea feni au kiyoyozi) lakini mara nyingi haiwi hivyo kwa sababu dunia yetu ni hai: kuna majira, mawimbi ya bahari, hali ya hewa inayobadilika badilika mf. joto kupanda na kushuka, mgandamizo wa hewa (pressure) kubadilika badilika na kutofautiana kutoka sehemu moja kwenda nyingine n.k. Chanzo cha yote haya ni nishati inayotokana na jua.
Kulingana na Mrs. Mbwiluga, hali ya uwepo wa joto tofauti kutoka sehemu moja kwenda nyingine (mf. bahari vs nchi kavu, milima vs mabonde, msituni vs jangwani, kanda tofauti za hali joto) husababisha pia tofauti katika mgandamizo wa hewa. Tofauti hii katika mgandamizo wa hewa ndiyo husababisha mjongeo wa hewa kutoka eneo moja kwenda sehemu nyingine. Mjongeo huu wa hewa unapotokea ndiyo tunaita upepo; na kwa kawaida upepo huvuma kutoka sehemu yenye mgandamizo mkubwa wa hewa kwenda kwenye sehemu yenye mgandamizo mdogo; na kutegemea na hali ya hewa ya siku hiyo pamoja na natural barriers kama milima, spidi yake inaweza kutofautiana kutoka eneo moja hadi jingine.
Kwa kifupi hivyo ndivyo Mrs. Mbwiluga alivyonifundisha Jiografia form two kuhusu uwepo wa upepo katika sayari yetu hii nzuri iitwayo dunia japo tunaiharibu kwa kasi ya kutisha. Thanks sana mwalimu wangu mpendwa wa Jiografia Mrs. Mbwiluga. Nitakukumbuka na kukuenzi daima!