Chanzo cha upepo

Chanzo cha upepo

Kabla hii mada haijaenda mbali nami nijuzwe
tofauti kati ya upepo na hewa
Hewa(air) ni mchanganyiko wa gas mbali mbali na zenye tabia tofauti. Hata vumbi pia lipo humo kwenye hewa hivyo nayo ni sehemu ya hewa. . .

Upepo ni hewa. Ila hewa hii ina kua kwenye mwendo(inajongea)

Chuku mfano wa maji yakijikusanya sehemu moja mengi. Utaita bwawa/ ziwa/ au bahari. Alafu kuna mto pia ambao wenyewe ni maji yanayo jongea(tembea) kutoka seheme moja kwenda nyingine.

Hivyo kwa mfano wa kengo la kuelewa ila sio sahihi sana una weza kusema upepo kwa hewa ni kama mto ulivyo kwa maji.
 
Mabadiliko ya temperature yakichangiwa na heat katika maeneo tofatuti upelekea low na high pressure hivyo air kuanza kuelekea kwenye low pressure.
 
Kuna MTU anafunguaga vioo vya dunia ikiwa kwenye mwendo. Refer upepo wa kwenye gari
 
Sababu ya upepo/ hewa kujongea ni dunia kujaribu "kubalance" mfumo wake wa mgawanyo wa hewa angani( kwenye atmosphere)

Mfano eneo A hali yake ya joto imeongezeka, hivyo hewa imetanuka(expand) eneo B hali yake ya joto ipo chini.(baridi) na hewa imesinyaa.

Matokeo yake ni kwamba mgandamizo wa hewa eneo B utakuwa mkubwa zaidi ya ule wa eneo A. Sasa anga linajibalance lenyewe kwa hewa kutoka B kwenda A ili kupunguza mgandamizano ulioko B na kupandisha mdandamizano uliopo A.hewa hii inapotembea(jongea) kuhama ndio inaitwa upepo.
 
Ngoja nikumbuke Geography yangu ya form two niliyofundishwa na Mrs. Mbwiluga.

Dunia ni sayari mojawapo iliyopendelewa sana kwa kuwa na tabaka nene la hewa. Katika tabaka hili ndiyo wamo akina Hydrogen, Oksijeni, Nitrogen na wengineo. Kwa hali hiyo, na kulingana na mwl. wangu kipenzi wa Jiografia Mrs. Mbwiluga, HEWA IPO TU KATIKA USO NA ANGA LA DUNIA INAELEA.

Katika hali ya kawaida hewa hii inapaswa kuwa tuliii imetulia (kama chumbani mwako ikiwa hujachochea feni au kiyoyozi) lakini mara nyingi haiwi hivyo kwa sababu dunia yetu ni hai: kuna majira, mawimbi ya bahari, hali ya hewa inayobadilika badilika mf. joto kupanda na kushuka, mgandamizo wa hewa (pressure) kubadilika badilika na kutofautiana kutoka sehemu moja kwenda nyingine n.k. Chanzo cha yote haya ni nishati inayotokana na jua.

Kulingana na Mrs. Mbwiluga, hali ya uwepo wa joto tofauti kutoka sehemu moja kwenda nyingine (mf. bahari vs nchi kavu, milima vs mabonde, msituni vs jangwani, kanda tofauti za hali joto) husababisha pia tofauti katika mgandamizo wa hewa. Tofauti hii katika mgandamizo wa hewa ndiyo husababisha mjongeo wa hewa kutoka eneo moja kwenda sehemu nyingine. Mjongeo huu wa hewa unapotokea ndiyo tunaita upepo; na kwa kawaida upepo huvuma kutoka sehemu yenye mgandamizo mkubwa wa hewa kwenda kwenye sehemu yenye mgandamizo mdogo; na kutegemea na hali ya hewa ya siku hiyo pamoja na natural barriers kama milima, spidi yake inaweza kutofautiana kutoka eneo moja hadi jingine.

Kwa kifupi hivyo ndivyo Mrs. Mbwiluga alivyonifundisha Jiografia form two kuhusu uwepo wa upepo katika sayari yetu hii nzuri iitwayo dunia japo tunaiharibu kwa kasi ya kutisha. Thanks sana mwalimu wangu mpendwa wa Jiografia Mrs. Mbwiluga. Nitakukumbuka na kukuenzi daima!
Dah huyo mwl. wako alikuwa hatari sana, safi.
 
MCHANGO WANGU (MADE SIMPLE)
Atmosphere (anga ama uso wa dunia) umejazwa na hewa (gas) ambayo ipo stationary kabisa (at room temperature) hewa hiyo ni Nitrogen, Oxygen na Noble gases (Hydrogen, hellium etc). Upepo ni hewa inayo tembea.
Naona wote mmejaribu kuelezea lakini sababu kubwa inayo sababisha kuwepo kwa upepo ni mwanga wa jua (Solar energy ) kivipi?
Jua linapopiga katika uso wa dunia linatengeneza joto kutokana na baadhi ya mionzi inayo sharabiwa ardhini na majini japo mingine inakuwa reflected. Kwa kawaida maji ya bahari huchelewa kupoteza joto haraka kuliko ardhini hivyo basi wakati wa usiku kufanya bahari kuwa na joto wakati ardhi huwa ni yabaridi hivyo kutokea kuwa upande wa ardhi huwa na mgandamizo mkubwa wa hewa (high pressure) hivyo hewa hutoka nchi kavu na kuelekea baharini ili kucover ile low pressure iliyopo kule.
Wakati wa mchana bahari inakuwa kwa kiasiflani imesha poa japo sasa inaanza kugain joto taratibu na ardhi inakuwa imepata joto kwa kiasi kikubwa kutokana na mionzi ya jua inayopiga ardhini. Hivyo hewa sasa katika mfumo wa upepo husafiri kutoka baharini ili kuja kupooza joto kali lilioko ardhini.
Kwahiyo kwa kifupi ni kuwa upepo ni hewa inayo tembea kutoka eneo lenye mgandamizo mkubwa (high pressure) kwenda kwenye eneo lenye mgandamizo mdogo (low pressure). Au kutoka sehemu yenye baridi kwenda kwenye sehemu yenye joto.
Ni kama vile gas inayowekwa kwenye mitungi mule ndani kunakuwa na high pressure na low temperature hivyo unapofungua koki utaruhusu gesi itoke automatically kwenda kwenye eneo lenye low pressure yaani nje ya mtungi.
Nadhani kwa kiasi fulani nimeeleweka. Ahsante
Safi.
 
Kwa maelezo hayo inaonyesha ukitaka kujua chanzo cha upepo pia utataka kujua chanzo cha Hewa.
 
Dah huyo mwl. wako alikuwa hatari sana, safi.
Ni mwalimu mzuri sana. Alinifanya nikapenda Jiografia mpaka nikapata A form 4 na 6. Aliweza kuifanya iwe relevant na mazingira yetu na tulikuwa tunatoka nje kwenda ku-examine natural processes laivu. Ndiyo maana amegeuka na kuwa rafiki/mentor/mshauri mkubwa sana.
 
Me naomba kuongeza swali..kwa nn bahari ni ya blue na au anga ni blue.
 
Umenikumbusha Jiografia darasa la sita mkuu: Upepo Mwanana wa nchi kavu na Upepo Mwanana wa Baharini...Nilisahau kulisema waziwazi hili katika comment yangu hapo juu (comment #15). Nadhani tumejaribu kueleza kwa lugha rahisi kabisa na inayoeleweka kuhusu upepo ndiyo maana hata waliokuwa wanaulizia huko nyuma wamepotea. Asante kwa elimu ya bure mkuu.
Sea breeze and land breeze... kwa kimombo.
 
Habarini wana jamvi,

Nimekuwa nikifikiria hili jambo kwa muda lakini nimekosa jibu la kunifanya niamini nnachosikia, nikaona sio mbaya ku share nanyi jamvini huenda kuna mtu ana uelewa wa haya mambo.

Hivi chanzo cha upepo ni nini?!
Mungu wetu wa dsm anaona nyotanyota tu hapa. Ukiona mtu amejibu upepo ni ushuzi muwe na mashaka nae
 
Upepo ni hewa ya kawaida inayokimbia(escaping) kutoka eneo lenye high pressure kuelekea eneo lenye low pressure ili kucreate balance!
 
Back
Top Bottom