Chanzo cha Utofauti wa Lugha na Rangi za Watu

Chanzo cha Utofauti wa Lugha na Rangi za Watu

LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2011
Posts
1,639
Reaction score
519
Wanabodi,

Hebu tujadili asili kubwa ya binadamu katika utofauti wa lugha na rangi zetu.

Kwa upande wa rangi, kuna weusi na weupe (kuna wazungu, wachina, wahindi, wakorea na wachapani).

Ndani ya watu wenye rangi tofauti, kumekuwepo na lugha mbalimbali kama kisukuma, kichaga, kihaya,
kizaramo, kiingereza, kihadzabe, kijerumani na kirusi.

Leo nakuja mbele zenu, kwa heshima na taadhima kuwaomba tujadili mwanzo wa lugha na kabila zetu binadamu kwa lengo la kueleweshana tu na wala siyo kutengana.

Asanteni na karibu sana.
 
Yehova akawatawanya juu ya uso wote wa dunia kutoka huko, nao pole kwa pole wakaacha kulijenga lile jiji. Hiyo ndiyo sababu liliitwa jina lake Babeli, kwa sababu huko ndiko Yehova alikuwa amevuruga lugha ya dunia yote.”—Mwanzo 11:8, 9.
 
hizo ni myth tu hazuna ukweli wowote!!
 
tukiweka dini kando kuna maelezo very specific ya kimazingira na kisayansi, mfano rahisi sana ni huu unapopanda ndege kwenye bango la repoti kuna actual flying time na destination flying time, angalia kuna tofauti kubwa, suala la kutofautiana kwa muda linatoa majibu kwa maswali mengi mno
 
Lugha tofauti na pale mnara wa babeli...rangi ni baada ya gharika mmoja wa watoto wa nuhu alikuwa cursed,nahisi ndo tofauti ya rangi ilipotokea.
 
sina ila hizo ni porojo tu...eti walitaka kujenga mnara ili wamfikie aliko mungu, sasa walishakaribia kumfikia ama? Vipi urefu wa huo mnara ulifikia urefu wa majengo ya sasa kama Bhuji Khalifa?

Tayari! Suruali fupi at work....
 
Hapa tutadanganyana tu!
Kunamatheory kibao yanaongelea sababu ya kuwepo kwa rangi tofauti!

Kwamfano:

Materialist wanasema Watu weusi wametokana na nyani!

Wakiristo wanasema watu weusi wametokana na maangamizo!

Waislamu wanasema watu weusi wamezaliwa tu kama vile wazazi wafupi kuzaa mtoto mrefu!
According to Islamic teachings Mwanadamu aliumbwa kwa udongo! Huo udongo ulikuwa ni mchanyiko wa rangi zote walizonazo wanadamu!

Nk nk!
...
Kuhusu lugha iko simple sana!
Kusambaratika kwa watu ktk dunia na lack of communication means imepelekea watu wa jamii moja kubuni maneno ya kutumia ili warahisishe mawasiliano!
 
Apa Nafu Kidogo Umefunguka Tumekuelewa
 
Mungu alivyo-design miili yetu, ina-adapt kulingana na mazingira. Kwa mfano, watu walioishi kwenye sehemu hizi zetu wakapewa pigmentation ya kuwalinda na miale mikali ya jua. Tusipende tu kupokea ngano na kuziamini madhali tu zimetoka kwenye sinagogi.

Mimi ni muumini. Lakini sioni mantiki ya kwamba Mungu alikasirishwa na binadamu waliojaribu kujenga mnara kumfikia, ndiyo akawasambaratisha kwa lugha.

Kanuni za fizikia alizotengeneza Mungu na kiwango cha teknolojia ya wakati hiyo havikuhitaji kabisa Mungu kuingilia upuuzi huo. Mnara ungalibomoka tu na wangesambaratika. Unataka kuniambia wangeweza kujenga mnara hata maili mbili kwenda juu?

Leo hii tunaziona lugha zinasambaa, zinatawanyika katika lahaja na baadae zinakuwa lugha mbalimbali. Wala jambo hili halitokani na watu kujenga mnara au kujaribu kumfikia Mungu.
 
Yehova akawatawanya juu ya uso wote wa dunia kutoka huko, nao pole kwa pole wakaacha kulijenga lile jiji. Hiyo ndiyo sababu liliitwa jina lake Babeli, kwa sababu huko ndiko Yehova alikuwa amevuruga lugha ya dunia yote.”—Mwanzo 11:8, 9.

Ina maana Mungu hakupendezwa na watu wa Babeli waliotaka kutengeneza mnara mrefu ili kumfikia, vipi kuhusu watu wa sasa ambao wanatengeza vyombo vinavyofika hadi Mars? kwanini Mungu aingilie ujenz wa huo mnara hali ya kuwa anajua kuwa hata wajenge vipi hawawezi kumfikia? kwanza teknolojia yao ilikuwa ndogo sidhani kama huo mnara ulikuwa mrefu kule jengo la PPF tower pale posta.
 
Ukitaka kupata jibu LA swali hili kunamasharti ambayo nilazima ukubaliane nayo ilaukiwa namtazamo wakuwa katikati ili uchangie pande zote hatasikumoja huwezi pata jibu. Masharti hayo ni kukubali kuamini Mungu au sayansi ndipo mjadala uendelee.
 
Ina maana Mungu hakupendezwa na watu wa Babeli waliotaka kutengeneza mnara mrefu ili kumfikia, vipi kuhusu watu wa sasa ambao wanatengeza vyombo vinavyofika hadi Mars? kwanini Mungu aingilie ujenz wa huo mnara hali ya kuwa anajua kuwa hata wajenge vipi hawawezi kumfikia? kwanza teknolojia yao ilikuwa ndogo sidhani kama huo mnara ulikuwa mrefu kule jengo la PPF tower pale posta.
Pole sana kijana
 
Hautapata jibu utaishia kuuliza tu. Kuna maswali hayana majibu. Utauliza na kujibiwa na litazaliwa swali ambalo ni vigumu kulijibu. Ili mladi unakula endelea kula.
 
Back
Top Bottom