Pale kwenye mnara wa Babeli (ambao wana akiolojia wamechimbua na kuubani mnara ule ulipojengwa-Iraq ya leo) maandiko yanasema palizuka lugha 70 tofauti tofauti.
Mungu, muumba mbingu na nchi,Yeye anayeutangaza mwisho tangu mwanzo, hakuwachelea kwamba watu wale watajenga mnara umfikie, ila aliwavurugia uneni wao ili dhamira yao ya kutoenda mbali na pale ipotee,alitaka watawanyike waenee duniani kote.Hili la kutawanyika kuijaza dunia alishaliandaa toka mwanzo.Alimwambia Adamu na Hawa enendeni duniani kote mkazae muongezeke mkaijaze dunia.