CHANZO CHA VIFO VYA USINGIZINI.
Waslaam wanajf kisima cha maarifa.
Kama kichwa cha Habari kinavyojieleza. Watu Wengi Sana tumekuwa tukijiuliza kwanini mtu analala usiku halafu asubuhi watu wanashudia amefariki?. Au alilala mchana halafu akafia usingizini? Kwanini mtu anafia usingizini? Kwanza napenda kutambua uwepo wa mungu Kwani mungu ndie anayeruhusu kila kitu.
Hata kifo ni mungu anaruhusu iwe usingizini, Katika ajali nk. Dini zote zinathibitisha hili. Haya, twende katika elimu hii ya dunia, Mara nyingi sana tumewasikia madaktari wakitoa sababu ya kifo cha mtu aliyefia usingizini kwamba ni BP, kisukari, mshituko wa moyo nk.
Nitachambua maada hii kwa nadharia Mbili. Ya kwanza ni kumalizika kwa ndoto na ya pili ni kuwa mshindi katika kila ndoto unayoota.
Nadharia ya kumalizika kwa ndoto. Kwanza haiwezekani ukalala bila kuota ndoto. Ndoto yoyote ile unayoota haiwezi malizika yaani huwezi ukaimaliza. Hebu jiulize tangu umeanza kuota ndoto umewahi kuzimaliza? Mara nyingi sana utashangaa tayari kumekucha au umeshitushwa na mama, baba, Mjomba na shangazi(kwa mnaokaa ubalozini). Sasa ukiota ndoto ukaimalizia hadi mwisho hapo ndipo kifo cha usingizini hutokea. Huwezi ukaimalizia ndoto halafu ukaamka tena hai labda Kwa miujiza ya mungu.
Pili, kuwa mshindi katika ndoto. Ndoto yoyote ile unayoota nilazima uwe mshindi.Kwanza jiulize umewahi kushindwa Katika ndoto yoyote ile? Kwa mfano labda umeota unakimbizwa na simba halafu simba akukukamata na kukuua ndotoni basi hata kimwili utakuwa umefariki.
Hapo ilitakiwa wewe ndo uwe mshindi umuue simba au uokolewe na mtu hapo utaamka lakini vinginevyo jina litabadilika. Mfano wa pili umeota unakimbizwa na majambazi wakakukamata na wakakuua basi ujue huo ndo mwisho wako hata kimwili.
Kwa haya machache nakalibisha mjadala #
Mkuu ulivyoanza kuandika na heading nikajua umejipanga utatujuza vizuri,nasoma mwishoni naona unakaribisha majadala?Hayo ni mambo magumu si mepesi,nilitegemea unalo jibu mimi naweza elezea vizuri nikimaliza kusoma kitabu fulani cha watu waliexperince being very close to death.
Lakini hiyo issue yako ya kutoikumaliza ndoto nigusie kidogo tu,mwanadamu ana conscious mind na subconscious mind,hizi haziwezi kudominate kwa muda mmoja.Ukiwa macho conscious mind inatawala,unapokuwa umelala unconscious mind inatawala.Ila elewa unconscious mind inahusika na mambo mengi amabayo kwa wenye imani tunasema ni ya rohoni,ukiwa umelala unaconscious mind inaweza ikakujulisha mambo yajayo kwa njia ya ndoto,au niseme unapoamka unajitahidi kukumbuka ulicho ota,trust me huwa tunaota ndoto nyingi.Mimi kuna mtu aliniambia hatuwezi kukumbuka ndoto zaidi ya tatu ulizoziota usiku mmoja,kama kuna mtu hukumbuka ndoto zaidi ya tatu awe mkweli ili tujielimishe.
Mtu halisi siyo mwili,mtu halisi ni ile nafsi iliyoko ndani ya mwili,ulishawahi jiuliza unapokuwa usingizini yule mtu "nafsi" iliyokuwa active mchana huwa inaenda wapi usiku kuipisha hiyo unconscious mind?Biblia inaita kufa ni kulala uzingizi mzito,kwa hiyo tunapolala usiku tunaonja asilimia ndogo ya kifo that is why unaweza usijue nini kimetokea usiku.
Ukijifunza kabla ya mtu kusinzia moja ya mambo yanayotokea kwenye mwili wa mwanadamu ni mwili kuslow down,kwa mfano mapigo ya moyo yanapungua speed,shughuri nyingi za mwili zinapungua mwishoni ukifikia level fulani tunasema usingizi unakuchukua unasinzia.
Niishie hapo kwa leo,kwa hiyo kama mtu atakufa usingizini sababu ni nyingi inawezekana kuna organ zimefail au kuna kitu tusichokijua(in spiritual real) kimesababisha,madaktari always kuna kitu wao wataona ingawa kinaweza kisiwe sahihi lakini kipo.