Chanzo halisi cha jina Tanganyika

ongeza bando tupate taaluma zaidi tunaopenda kujifunza mambo kumbuka tu uzi bila picha haunogi pia ukianisha mipaka yake vipi ilikua itanoga zaidi asante nawasilisha.
 
Huko mwambao wa Pwani kulipaki mashua nyingi zilizopeperusha Tanga hivyo kufanya Pwani kuitwa Tanga. Sasa wageni wa dizaini ya Vasco waliokuwa wakisafiri Kwa mashua na kufika nchi kavu, walianza kutembea kuelekea porini (nyikani) kuendelea na expropriation yao.
Kutokana na nchi kuwavutia kwa harufu nzuri ya utajiri wa Mali - asiri wakalazimika kutafuta jina la hiyo nchi, na hapo ikawa kuunganisha Tu Pwani na nyikani na kuwa Tanganyika.
 
Wageni wa mwanzo pwani ya pangani waliwauliza watoto waliokua wakicheza baada ya kushuka jahazini walipo waxazi wao,wakajibiwa wameenda nyikani wakaulizwa hapa ni wapi?wakajibu hapa ni tangani(Bandar) ,
 
Chanzo cha jina Tanganyika kwa maana ya Tanganyika Territory ni lile jina la Ziwa Tanganyika ambalo lilipewa jina hilo na David Livingstone hata kabla ya Afrika kugawanywa; kwa hiyo halikutokana na majina ya Tanga na Nyika kama ambavyo watu wengi hutoa tafsiri za harakaharaka. Jina Tanganyika limetokana na lugha ya wamanyema na lina uhusiano na msemo wa "majini huko linakotokea jua." Kuna historia yake niliwahi kuileta hapa kama miaka kumi iliyopita, nitatafuta hizo records kutoka royal historical society tena nikipata nafasi.

Angalia ramani hiyo ya safari za Livingstone 1851 hadi mwaka 1873 inaonyesha Ziwa Tanganyika, hiyo ni kabla mjerumani hajaingia nchini.
 
Nafikiri Tanganyika kwa muktadha wa Ziwa inaweza kuwa ni neno la lahaja linalomaanisha changanyika.

Inawezekana kuna etimology kuhusu maji ya ziwa kuchanganyika.

Just my thoughts.
Nimewahi kusoma hii pia kwenye records za Royal Historical Society; ila jina lile limetokana na Lugha ya Kimanyema.
 
Mark 8/10


Kiranga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanga = kusafiri au kutembea mwendo wa mbali
Nyika = ni uwanda mpana, dunia au ulimwengu
 
Congo DRC na Burundi kuna maeneo yanaitwa Tanganyika,vipi kuhusu hilo mleta mada [emoji2960]
 
Niliwahi kusikiaga mzee mmoja wa pwani akisema Tanganyika maana yake ni Tanga na nyika yake. Yaani Tanga as area na Nyika yake as mainland.

Sent from my CLT-L09 using JamiiForums mobile app
 
Congo DRC na Burundi kuna maeneo yanaitwa Tanganyika,vipi kuhusu hilo mleta mada [emoji2960]
bado huja jenga hoja kwamba itakuwa historia hatuiyamini ukichukua majina hata pemba iko sehemu wanaita kenya ijapokua haihusiani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…