Chanzo halisi cha jina Tanganyika

Chanzo halisi cha jina Tanganyika

Kabla ya Mwaka 1920 Hakukuweko na nchi ikiitwa Tanganyika Kwa kuwa chini ya utawala wa Kijerumani Tanzania Bara iliitwa Deustche Ost-Afrika, ilikuwa lazima Waingereza kutafuta jina lingine mara baada ya kushika utawala.

Awali katika mwaka 1920, yalipendekezwa majina kadhaa, yakiwemo, “Smutsland”, “Ebumea”, “New Maryland”, “Windsorland”, na “Victoria”, ambayo hata hivyo yalikataliwa yote na Serikali ya Uingereza kutokana na sababu mbalimbali.

Baadaye serikali ya Uingereza ilielekeza yapendekezwe majina ya kienyeji, ndipo yakajitokeza majina “Kilimanjaro” na “Tabora”, ambayo yalifikiriwa lakini hayakuchaguliwa.

Hatimaye jina “Tanganyika Protectorate” lilipendekezwa na msaidizi wa Makoloni na likakubaliwa na Serikali. Inafahamika kwamba, kabla ya ujio wa wageni kutoka Ulaya, wenyeji katika maeneo ya Magharibi mwa nchi waliliita ziwa kubwa lililopo eneo hilo “Ziwa Tanganyika”. Inaelekea hiyo ndiyo sababu kubwa iliyofanya maofisa wa serikali kulikubali jina la Tanganyika kwa sababu lilikidhi matakwa ya sera kwa kuwa lilitokana na majina ya kienyeji.

Halimaye neno “Protectorate” liliondolewa kutoka jina rasmi la ‘Tanganyika Protectorate’, na badala yake likawekwa neno “Territory”.

Kwa hiyo, kuanzia mwaka 1920 hadi uhuru nchi ikajulikana kama “Tanganyika Territory”

Credit: Historia Ya AfrikaView attachment 1470806

Sent using Jamii Forums mobile app
ongeza bando tupate taaluma zaidi tunaopenda kujifunza mambo kumbuka tu uzi bila picha haunogi pia ukianisha mipaka yake vipi ilikua itanoga zaidi asante nawasilisha.
 
Huko mwambao wa Pwani kulipaki mashua nyingi zilizopeperusha Tanga hivyo kufanya Pwani kuitwa Tanga. Sasa wageni wa dizaini ya Vasco waliokuwa wakisafiri Kwa mashua na kufika nchi kavu, walianza kutembea kuelekea porini (nyikani) kuendelea na expropriation yao.
Kutokana na nchi kuwavutia kwa harufu nzuri ya utajiri wa Mali - asiri wakalazimika kutafuta jina la hiyo nchi, na hapo ikawa kuunganisha Tu Pwani na nyikani na kuwa Tanganyika.
 
Wageni wa mwanzo pwani ya pangani waliwauliza watoto waliokua wakicheza baada ya kushuka jahazini walipo waxazi wao,wakajibiwa wameenda nyikani wakaulizwa hapa ni wapi?wakajibu hapa ni tangani(Bandar) ,
 
Chanzo cha jina Tanganyika kwa maana ya Tanganyika Territory ni lile jina la Ziwa Tanganyika ambalo lilipewa jina hilo na David Livingstone hata kabla ya Afrika kugawanywa; kwa hiyo halikutokana na majina ya Tanga na Nyika kama ambavyo watu wengi hutoa tafsiri za harakaharaka. Jina Tanganyika limetokana na lugha ya wamanyema na lina uhusiano na msemo wa "majini huko linakotokea jua." Kuna historia yake niliwahi kuileta hapa kama miaka kumi iliyopita, nitatafuta hizo records kutoka royal historical society tena nikipata nafasi.

Angalia ramani hiyo ya safari za Livingstone 1851 hadi mwaka 1873 inaonyesha Ziwa Tanganyika, hiyo ni kabla mjerumani hajaingia nchini.
1591649185207.png
 
Nafikiri Tanganyika kwa muktadha wa Ziwa inaweza kuwa ni neno la lahaja linalomaanisha changanyika.

Inawezekana kuna etimology kuhusu maji ya ziwa kuchanganyika.

Just my thoughts.
Nimewahi kusoma hii pia kwenye records za Royal Historical Society; ila jina lile limetokana na Lugha ya Kimanyema.
 
Chanzo cha jina Tanganyika kwa maana ya Tanganyika Territory ni lile jina la Ziwa Tanganyika ambalo lilipewa jina hilo na David Livingstone hata kabla ya Afrika kugawanywa; kwa hiyo halikutokana na majina ya Tanga na Nyika kama ambavyo watu wengi hutoa tafsiri za harakaharaka. Jina Tanganyika limetokana na lugha ya wamanyema na lina uhusiano na msemo wa "majini huko linakotokea jua." Kuna historia yake niliwahi kuileta hapa kama miaka kumi iliyopita, nitatafuta hizo records kutoka royal historical society tena nikipata nafasi.

Angalia ramani hiyo ya safari za Livingstone 1851 hadi mwaka 1873 inaonyesha Ziwa Tanganyika, hiyo ni kabla mjerumani hajaingia nchini.
View attachment 1472490
Mark 8/10

Kiranga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya Mwaka 1920 Hakukuweko na nchi ikiitwa Tanganyika Kwa kuwa chini ya utawala wa Kijerumani Tanzania Bara iliitwa Deustche Ost-Afrika, ilikuwa lazima Waingereza kutafuta jina lingine mara baada ya kushika utawala.

Awali katika mwaka 1920, yalipendekezwa majina kadhaa, yakiwemo, “Smutsland”, “Ebumea”, “New Maryland”, “Windsorland”, na “Victoria”, ambayo hata hivyo yalikataliwa yote na Serikali ya Uingereza kutokana na sababu mbalimbali.

Baadaye serikali ya Uingereza ilielekeza yapendekezwe majina ya kienyeji, ndipo yakajitokeza majina “Kilimanjaro” na “Tabora”, ambayo yalifikiriwa lakini hayakuchaguliwa.

Hatimaye jina “Tanganyika Protectorate” lilipendekezwa na msaidizi wa Makoloni na likakubaliwa na Serikali. Inafahamika kwamba, kabla ya ujio wa wageni kutoka Ulaya, wenyeji katika maeneo ya Magharibi mwa nchi waliliita ziwa kubwa lililopo eneo hilo “Ziwa Tanganyika”. Inaelekea hiyo ndiyo sababu kubwa iliyofanya maofisa wa serikali kulikubali jina la Tanganyika kwa sababu lilikidhi matakwa ya sera kwa kuwa lilitokana na majina ya kienyeji.

Halimaye neno “Protectorate” liliondolewa kutoka jina rasmi la ‘Tanganyika Protectorate’, na badala yake likawekwa neno “Territory”.

Kwa hiyo, kuanzia mwaka 1920 hadi uhuru nchi ikajulikana kama “Tanganyika Territory”

Credit: Historia Ya AfrikaView attachment 1470806

Sent using Jamii Forums mobile app
Tanga = kusafiri au kutembea mwendo wa mbali
Nyika = ni uwanda mpana, dunia au ulimwengu
 
Congo DRC na Burundi kuna maeneo yanaitwa Tanganyika,vipi kuhusu hilo mleta mada [emoji2960]
 
Niliwahi kusikiaga mzee mmoja wa pwani akisema Tanganyika maana yake ni Tanga na nyika yake. Yaani Tanga as area na Nyika yake as mainland.

Sent from my CLT-L09 using JamiiForums mobile app
 
Congo DRC na Burundi kuna maeneo yanaitwa Tanganyika,vipi kuhusu hilo mleta mada [emoji2960]
bado huja jenga hoja kwamba itakuwa historia hatuiyamini ukichukua majina hata pemba iko sehemu wanaita kenya ijapokua haihusiani
 
Back
Top Bottom